
03/03/2022
Kulingana na takwimu zilizotolewa jana na shirika linaloshughulika na maswala ya wakimbizi duniani , nchi ya Poland imeongoza kwa kupokea wakimbizi wengi zaidi kuliko nchi zingine amabazo zipo jirani na Ukraine.
Takwimu hizo zinaonyesha kwamba wakimbizi zaidi ya laki tano wamekimbilia nchi ya Poland, idadi ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na nchi zingine.
Nchini ya Hungary imepokea wakimbizi zaidi ya laki moja, ikifuatiwa na Jamuhuri ya watu wa Moldova ambayo imepokea wakimbizi zaidi ya elfu 90.
Mataifa mengine ya Ulaya, yamepoke idadi ya wakimbizi 88,147 kwa ujumla wake, huku nchi zingine k**a vile Slovakia, Romania, Nchi za umoja wa Urusi, na Belarus zimepokea idadi ya wakimbizi isiyozidi 72,200.
Aidha, UNHCR imesema kuna uwezekano mkubwa kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi katika nchi hizo kadiri muda unavyozidi kwenda.