07/01/2026
PUMZIKENI KWA AMANI😭💔
Jimbo kuu katoliki la Nairobi linaomboleza kufuatia kifo cha Katekista James Njoroge Kabari, mkewe Teresia na wanao wawili; Michael Kabari mwenye umri wa miaka 6 na John Mark Kabui mwenye mwaka 1 kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Karai, Naivasha, gatuzi la Nakuru.
Mwanao Clare Wairimu anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi Women kufuatia majeraha aliyopata kutokana na ajali hiyo.
Raha ya milele uwape Ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie, wapumzike kwa amani, Amina.