16/02/2023
Rashford mshambuliaji hatari Ulaya.
Meneja wa Barcelona Xavi Hernandez amemwagia sifa mshambuliaji wa Manchester United Rashford kuwa ni miongoni mwa wafunga magoli hatari kwa sasa Ulaya.
Pia Xavi amempongeza Erik ten Hag kwa kuiboresha na kuimalisha klabu ya Manchester United huku akimfanya Marcus Rashford kurudi kwenye ubora wake.
Kwa sasa Rashford amefunga mabao 13 katika mechi 15 tangu kombe la dunia lilivyomalizika. Idadi hiyo ya magoli inamfanya Rashford kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi bara la ulaya kwa kipindi hicho.
Kocha huyo wa Barcelona ameongeza kuwa wanatahadhari kwa wachezaji wote United na hasa mshambuliaji Rashford aliyepo kwenye kiwango cha juu kwa sasa.
Barcelona inawaalika Man united usiku wa leo Alhamis kwenye michuano ya Europa League ngazi ya mtuano.