02/06/2025
🚨Fiston Kalala Mayele
Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Fiston Kalala Mayele, ameendelea kuandika historia barani Afrika baada ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya CAF Champions League 2024/2025, akiwa na klabu ya Pyramids FC ya Misri.
Mayele aling’ara kwenye michuano hiyo kwa kufunga mabao muhimu yaliyoiwezesha Pyramids kufika fainali na hatimaye kutwaa ubingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, katika mchezo wa kusisimua uliomalizika kwa ushindi wa goli 2-1 nakufanya mchezo kuwa na jumla ya magoli 3-2.
Tangu ajiunge na Pyramids kutoka Young Africans SC ya Tanzania, Mayele ameonyesha kiwango bora na mshik**ano mkubwa na kikosi hicho, akivutia mashabiki wengi kwa uwezo wake wa kufumania nyavu.
Tuzo hii ni ushahidi wa mafanikio yake binafsi, lakini pia ni heshima kwa wachezaji wa Afrika Mashariki wanaoendelea kung’ara katika anga za kimataifa.