Dirayasamia

Dirayasamia Tanzania Online Media SUPA18 is a soon to be launched socio-media site.

It will be firmly introduced in the year 2013 after claimming a great foundation-That's the main goal this year. The term “SUPA” basically implies how the site will be so diverse in various socio aspects so as to satisfy the public demands,meaning the fans/supporters/members in the site & “18” symbolizes the basic age of most expected customers; that's to say only the 18 and above will be allowed

to join in. SUPA18 will comprise of Live charts,uploads and downloads of mp3/4; clips uploads and video downloads; celebrity stories; stuff's/crew's activities; movies infos; sports news; global news & many more……
Priority will be offered to businessmen and women to advertise on supa18's site in order to widen the market or even introduce new deals/products on their sales. Offers to new talents will be available,including;publicizing and improving your status by arranging different events and topics so as to expose them off. All that we need from you,the public is support so as we can attain this maiden dream altogether as one.
“If we intergrate we can make it as all BUT if we disintergrate we can lose it all”
For further info try to contact;
ELIYA JAMES LYAMBA- 0719744615
RODRIQUE ROMIO FELIX- 0653763632
SHEBBIE NNKO- 0653934313.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka taji la maua kwenye mnara wa kumbukumbu w...
25/06/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka taji la maua kwenye mnara wa kumbukumbu wa Mashujaa Mjini Maputo ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, tarehe 25 Juni 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa ...
25/06/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo tarehe 24 Juni, 2025 Maputo, Jamhuri ya Msumbiji ambapo anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zitafanyika kesho katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

Jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Sami...
24/06/2025

Jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha utekelezaji wa mikakati ya kukuza uchumi wa viwanda nchini umezaa matunda kwa asilimia kubwa sana ndani ya miaka 4 ya Uongozi wa Rais Samia.

Mikakati hiyo ni pamoja na viwanda vya ndani kutoa ajira kwa watanzania ili kuchochea mauzo nje ya nchi, mchango huo umeongezeka kutoka 8.1% mwaka 2023 hadi 12.8% 2024.

Mikakati mingini ni Mauzo ya Bidhaa za Teknolojia ya juu, nje ya nchi mchango huo umeongezeka kutoka 25% 2023/24 hadi 36% 2024/25
Kwa ujumla sekta ya viwanda inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta ustawi wa uchumi kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuunda ajira, kuvutia uwekezaji na kuongeza pato la nchi.

23/06/2025

Ndani ya kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanzisha juhudi za kuboresha upatikanaji wa Gesi Asilia hasa kwa matumizi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, ili kuboresha Afya ya Wananchi na kulinda mazingira nchini.

Amezindua mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia kwa kipindi cha miaka 10 toka 2024 hadi 2034, ikiwa na lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Pia Ameanzisha Miradi ya Miundombinu ya gesi asilia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka kisima cha Ntorya hadi kituo cha madimba kilomita 34. Miradi hii inalenga kuongeza uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.

Kwa kushirikiana na Sekta Binafsi imetoa mkopo kwa wauzaji wa Gesi ili kujenga vituo vya kujaza gesi vijijini. Hii ni sehemu ya juhudi mhe. Rais kuhakikisha Nishati ya Gesi inasambaa Mjini na Vijijini.

Katika uongozi wa miaka 4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha Juhudi za kuima...
23/06/2025

Katika uongozi wa miaka 4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha Juhudi za kuimarisha Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania tangu alipoingia Madarakani mwaka 2021 ikiwemo kufungua vyombo vya Habari ambavyo vilivyokuwa vimefungiwa na kuagiza kuondolewa kwa vikwazo vya kiutawala kwa vyombo vya habari,lakini pia kuanzisha kongamano la maendeleo ya sekta ya Habari.

🇹🇿 DARJA LA JP MAGUFULI – NI ZAIDI YA DARAJA!Daraja hili si tu kivuko cha kuunganisha pande mbili za nchi, bali ni alama...
23/06/2025

🇹🇿 DARJA LA JP MAGUFULI – NI ZAIDI YA DARAJA!
Daraja hili si tu kivuko cha kuunganisha pande mbili za nchi, bali ni alama ya uwezo wetu k**a taifa wa kupanga, kutekeleza, na kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati.

Ni matokeo ya maono ya viongozi wetu na uthubutu wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza dira ya maendeleo ya nchi yetu.

Leo tunajivunia miundombinu ya kisasa, kesho tunavuka na kuunganika zaidi k**a taifa moja.

🇹🇿
🔨

MRADI WA MAJI BUTIMBA 💧Wananchi zaidi ya 450,000 sasa wanapata maji safi na salama kupitia mradi wa maji Butimba!Huu ni ...
23/06/2025

MRADI WA MAJI BUTIMBA 💧
Wananchi zaidi ya 450,000 sasa wanapata maji safi na salama kupitia mradi wa maji Butimba!

Huu ni ushahidi wa dhamira ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za maji zinawafikia Watanzania wengi zaidi mijini na vijijini.

✅ Maji safi kwa wote
✅ Afya na ustawi wa jamii
✅ Hatua kubwa kuelekea maendeleo ya kweli

Tunaendelea kuweka mkazo kwenye miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

🇹🇿
🔨
💦

💧 MRADI WA MAJI LAMADI - SIMIYUChini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi mkubwa wa maji Lamadi...
23/06/2025

💧 MRADI WA MAJI LAMADI - SIMIYU
Chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi mkubwa wa maji Lamadi umefanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu!

✅ Wananchi 85,000 wamenufaika moja kwa moja
✅ Upatikanaji wa maji umefikia 97%
✅ Tumefikia lengo – Tumepita matarajio!

Mama Samia anaendelea kutatua changamoto za maji nchini kwa vitendo.
Tanzania Ya Samia ni ya vitendo, si maneno! 🙌.

🇹🇿
🔧
💦

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofan...
22/06/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watemi wa kabila la Wasukuma mara ...
21/06/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watemi wa kabila la Wasukuma mara baada ya kutembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.

Shamrashamra wakati wa Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Bujora, Kisesa Mko...
21/06/2025

Shamrashamra wakati wa Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Bujora, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dirayasamia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share