13/09/2026
Msanii wa Bongo Flava Marioo, amefanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki 2026 (Best Male East Africa) katika tuzo za African Regional Music Awards (AFRIMMA) zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 13, 2026, jijini Dallas, Texas huko nchini Marekani.
Tuzo hizo zilitolewa katika tamasha la AFRIMMA Music Fest lililofanyika kwenye Uwanja wa Annette Strauss Square, AT&T Performing Arts Center, Mbali na kushinda tuzo hiyo, pia alikuwa miongoni mwa wasanii ambao wametoa burudani kali katika Tamasha hilo huku akipewa -support ya JITU Dj D-Ommy đčđż(InterNational Dj) kutoka CROWN DJs.
Kwenye tuzo hizo Marioo alikuwa akiwania na wasanii wakubwa East Africa wakiwemo Watanzania
đčđż Diamond Platnumz (Tanzania)
đčđż Juma Jux (Tanzania)
đčđż Mbosso (Tanzania)
đčđż Barnaba (Tanzania)
đ°đȘ Bien (Kenya)
đșđŹ Eddy Kenzo (Uganda)
đșđŹ Joshua Baraka (Uganda)
đȘđč Lij Michael (Ethiopia)
đžđž Single Dee (South Sudan)