
17/07/2025
Waratibu na wazimamizi wa uchaguzi,wametakiwa kujiepisha na makundi sogozi ya Whatsapp katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuepuka kutuma taarifa za siri zisizopaswa kutumwa kwa watu wengine.
Tahadhari hiyo imetolewa leo Julai 17,2025 Mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro na Mjumbe wa tume ya uchaguzi Dkt.Zakia Abubakar wakati akifunga semina ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo,maafisa uchaguzi na maafisa manunuzi 119 kutoka mkoa wa Kilimanjaro na Tanga.
“Hivi sasa yapo makundi sogozi ya whatsapp ,jitajidini katika kipindi hiki myapunguze ili msije kukosea kutuma taarifa yoyote katika makundi hayo ambayo haikutakiwa kutumwa kwao,kwa kuanza kutoa taarifa za siri ambazo tume haikukupa maelekezo kuzitoa katika utekelezaji wa kazi zako maana yake utakuwa umetenda kosa chini ya sheria ya kanuni za uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani za mwaka 2025 na utawajibika kwa kosa hilo” alisema Dkt.Zakia
Aidha amewataka washiriki hao kutafsiri mafunzo hayo kwenye usimamizi wa shughuli za kila siku za masuala ya uchaguzi kwa kuanza na vikao kwa vyama vya siasa,utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge na kuhakikisha utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wenyewe ngazi ya udiwani unafanyika kwa mumujibu wa sheria,kuhitisha na kuratibu k**ati za upangaji wa ratiba za kampeni na kuhitisha k**ati za maadili iwapo kuna changamoto zitajitokeza wakati wa kampeni.
“Katika maeneo mbalimbali tuliyopita wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura tuliona changamoto ya kutobandikwa kwa mabango yanayopaswa kubandikwa ili kumuelekeza aliyekuwa anasifa za kuandikishwa na wadau wengine kufika mahali palipo na kituo hivyo tunasisitiza changamoto hiyo isitokee tena katika kipindi hiki cha uchaguzi hivyo mabango,orodha za majina na matangazo zinabandikwa kwa kulingana na kalenda ya utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi ili kuepusha malalamiko na ukiukwaji wa masharti na sheria za kanuni za uchaguzi” alisema Dkt.Zakia
Cc ✍️