30/05/2024
Usiku wa manane .... 03
Palipo kucha mganga akamuomba asiondoke akae apo hapo Kwa siku tatu Betty alikubali na ukumbuke hapo chakula mganga π anakula k**a kawaida π€£π€£π€£π€£basi baada ya siku kuisha Betty akaludi biashara yake ikiwa ya kawaida sana sio k**a ilichangamka kiviile hapana, akawa ana shangaa vipi mbona maokoto hayaji k**a alivyokuwa anatalajia akaludi Kwa mganga mganga akamwambia Kuna dawa ya kuwekewa siku Saba oooh Betty akasema ujinga huuu basi wakajibishana pale mganga π akamfanya bubu hapo hapo Betty na akamwambia nilikuwa nakutamani sana Toka unasoma shule na Mimi ndio nilikutia Giza usipate ajira selikalini Wala kwenye kampuni ili ubaki hapa hapa na ukitaka kupona na kuwa salama ni Bora ukubali uwe mke wangu wa sita upo dada? πππππ Betty alilia sana hata hakiweza kusema mdomo unafunguka lakini maneno hayatoki alikuwa analia Kwa uchungu tu basi ikabidi akubali π±π±π±π± huku moyoni akiwa ana sikitika sana inakuwaje hivi jaman yaani awe mke wa kibabu kizeee uwiii ππππalilia, yule mganga akamfumbua mdomo akasema chumba chako nishakuandalia utalala na Mimi mpaka hizo siku Saba na hao marafiki zako watakuja kwako na watakushangilia zaidi ya zamani, basi Betty akakubali π’π’π’ aka kaa pale mpaka siku ya Saba kweli alipo ludi nyumbani marafiki zake walimshangilia sana na walimpenda mnooo lakini hakuwa na furaha Tena na hayo maisha aliumia moyoni hapo usoni alitabasamu akaenda Kwa mama yake akamwambia kuwa anataka kuolewa, mama yake akamwambia mwanangu ni jambo jema lakini kwann usisimame kwanza kibiashara mpaka hata mwakani ndio uolewe? Betty alilia sana huku akimwambia mama yake hapana mama Mimi nimepata mwanaume anayenipenda kweli nataka kuolewa we mwambie baba jumatano wanakuja kuleta barua ya uchumba, mamayake akauliza kwani uyo kijana ni nan? Ni WA hapa mtaani au?
Betty alimtazama mama yake kwa uchungu asijue amwambie vipi ila alilia sana πππππ machozi ya uchungu yalimtoka sana, mara mlangoni ikasikika odiii mama Betty akamkaribisha alikuwa ni bi zubeda .
Mama Betty; karibu mama karibu ndani
Bi zubeda: hata sihitaji karibu Yako uyo mtoto wako Betty upo?
Mama Betty; ndio yupo ndani
Bi zubeda akaingia ndani Kwa fujo akafika akamkaba nguo Betty.
' wewe ndio unajifanya mtamu sana kuliko Wana wake wote tulio olewa na mume wangu sio?' ... Betty hakujibu kitu mama Betty akapata jawabu kuwa mwanae anaolewa na Mzee uwiii alipigwa mwanoooo wa hatari ,
Mama Betty; mwanangu umekosea nn wewe jaman ?
Betty; mama ngoja nikuelezee
Bi zubeda; hakuna Cha kuelezea hapa Sasa nakupa siku tatu uachane na mume wangu tuo olewa tumetosha Mimi k**a bi mkubwa naongea wewe ni k**a mjukuu wangu huwezi kuwa mke mwenzangu Sasa k**a unataka kushindana na Mimi endelea kuja kulala Kwa mume wangu...
Mama Betty akazimia hapo hapo maana hakuamini maneno ya bi zubeda ππ majirani wamejaa dirishani maana sauti ya bi zubeda ilikuwa juu sana, Kisha bi zubeda akaondoka Kwa mbwembwe na tambo , majirani wakaingia ndani kumsaidia mama Betty huduma ili akae sawa hapo Betty analia tu Hana la kufanya...
Sasa mtaa mzima unajua k**a Betty anatoka kimapenzi na Mzee ally mganga maalufu Kwa Ile kata π±π±π±ni aibu Kila mja anaongea lake mara ukute na mtaji kautoa uko Kwa mganga na wengine ooh Betty apikiagi mwiko anapikia mkono wa mtoto ππππalilia akafungua kibanda maana wateja walimkimbia, akaludisha na chumba alichokuwa amepanga akakusanya vitu vyake akaludi nyumbani kuishi Kwa mama yake,
Wiki ikapia Betty atoki kutembea anaona aibu Kwa maneno yalivyo zagaa, basi siku Moja akaja kijana wa kwanza wa familia ya Mzee ally mganga anaitwa salumu akafika akamsalimia mama Betty lengo ilikuwa kuja kuleta barua ya uchumba wa baba yake, mama Betty akagoma kuipokea akasema hapana msubiri babake aje Mimi sipokei hii laana ...... itaendelea