Habari Za Nyarugusu CAMP

Habari Za Nyarugusu CAMP Ukurasa unaotoa taarifa za Kambini Nyarugusu kwa sekta zote. Kuna wakati tunaenda kitaifa & kimataifa

🛑 : Kagame ampokea raïs mstaafu wa Kenya kujadili kuhusu amani mashariki mwa DRCRaïs wa Rwanda, Paul Kagame alimpokea ra...
12/07/2025

🛑 : Kagame ampokea raïs mstaafu wa Kenya kujadili kuhusu amani mashariki mwa DRC

Raïs wa Rwanda, Paul Kagame alimpokea raïs wa mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta jioni ya hiyo Ijumaa Julai 11, 2025 katika kijiji cha Urugwiro ambapo inasemekana kuwa mazungumzo yao yalilenga kujadili kuhusu vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC.

Katika kikao chao, mazungumzo ya Uhuru Kenyatta anayetajwa kuwa mmoja wa Wapatanishi wa EAC-SADC kwa mchakato wa kuleta amani mashariki mwa DRC na mwenyeji wake Pal Kagame yalijikita zaidi kwenye juhudi zinazoendelea ili kufanikisha kuleta suluhu kwa mzizo huko Kivu Kaskazini na Kusini pamoja na kutafuta njia za kuleta amani ya kudumu na kufafanua sababu za msingi za mzozo usioisha huko Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩.
..✍🏼Unahisi undani wa kikao hicho cha wawili hao ulikuwa kutafuta suluhu ili kurejesha amani mashariki mwa DRC ao yapo mengine yao ya nyuma ya pazia?

🛑 : Congo yataka maelezo kutoka Uganda kuhusu kufunguliwa kwa mpaka wa BunaganaSerikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Co...
12/07/2025

🛑 : Congo yataka maelezo kutoka Uganda kuhusu kufunguliwa kwa mpaka wa Bunagana

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inataka maelezo kutoka kwa serikali ya Uganda, kuhusu kufunguliwa kwa mpaka wa Bunagana, katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23.

Kufuatia kikao cha Baraza la Mawaziri, Wizara ya Mambo ya nje, imetakiwa kutafuta majibu kutoka kwa serikali ya Uganda, ni kwanini mpaka huo ulifunguliwa tena wiki hii, bila ya kuwepo kwa maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mpaka wa Bunagana ulifunguliwa tena siku ya Alhamisi, na maafisa wa serikali ya Uganda, katika eneo hilo ambalo tangu mwezi Juni mwaka 2022 kwa sababu za kiusalama, lipo chini ya waasi wa M 23.

Ripoti zinasema, mpaka huo ulifunguliwa baada ya maagizo ya Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba baada ya maelekezo ya rais Yoweri Museveni, ili kufungua tena fursa hasa za kibiashara kati ya nchi hizo jirani.

Tangu kufungwa kwa mpaka wa Bunagana, wenyeji wa Bunagana kutoka pande zote mbili, kulisababisha ukosefu wa ajira na kuanza kusababisha umasikini kati ya raia wa kawaida.

: Ukurasa wa Facebook wa RFI Swahili Julai 12, 2025

12/07/2025

Salamu wafuasi wangu wapya! Nina furaha kuwa nanyi! Hamisi Madingu, Pro Jonas Ambogo, George Jackson Kilampala, Bambo Victor, Psako Frank, Ntahomvukiy Asman, Ôleho Manyassa, John Bernard JB, David Oliviye, Issa Portas

😭 : Mzee wa Hewa Bora Bar afariki dunia Jamii ya wakimbizi na wakaaji wa kijiji cha P1, zone ya 6 inayo masikitiko makub...
12/07/2025

😭 : Mzee wa Hewa Bora Bar afariki dunia

Jamii ya wakimbizi na wakaaji wa kijiji cha P1, zone ya 6 inayo masikitiko makubwa ya kutangaza kifo cha baba yao na mjomba wao Baganda Take aliyekuwa akijulikana zaidi kwa jina la Hewa Bora ambaye ameaga dunia usiku wa kuamikia Jumamosi hii Julai 12, 2025 kwenye hospitali kuu ya kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma.

Mmoja wa ndugu wa marehemu aliyetupa taarifa hii ya kifo amesema kuwa Mzee Baganda Take aliyewayi kuwa Mwalimu kwenye shule za sekondari huko Baraka na Kambini Lugufu amefariki baada ya kusumbuliwa na magonjwa ya presha, kisukari na moyo kwa zaidi ya miaka 6 ambapo familia ilijitahidi kumtibisha ila haikuwezekana hatimaye Mungu kaamua kumpumzisha.

Msiba wa mzee Baganda Take ama Hewa Bora umewekwa nyumbani kwake kwenye plot ya 21 klasta ya 7 katika kijiji cha P1, zone ya 6 na mpango wa mazishi yake utatangazwa hapo baadaye.

Uongozi wa Ukurasa huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na walimu pamoja na wanakijiji cha P1 kwa kumpoteza mpendwa wao. Mungu azidi kuwafariji na kumpumzisha marehemu Hewa Bora kwa amani.

⚽ : Mkongomani mwengine raia wa Fizi atarajiwa kutua Azam FCAzam FC inatajwa kuiwinda saini ya mlinzi wa kulia wa Al Hil...
10/07/2025

⚽ : Mkongomani mwengine raia wa Fizi atarajiwa kutua Azam FC

Azam FC inatajwa kuiwinda saini ya mlinzi wa kulia wa Al Hilal Omdurman ya Sudan, Steven Ebuela Ehebelo raia wa DRCongo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi.

Inaelezwa kuwa Steve Ebuela Ehebelo ni chaguo la kocha mpya Florent IBENGE kwa sababu wamewahi kufanya kazi pamoja.

Pia Azam wana wasiwasi kumpoteza mlinzi wao wa kulia Lusajo Mwaikenda anaehusishwa na Simba SC.

Kwa muonekano huo wa kizibo hicho kikali lazima watu wa Fizi wajivunie Fizi yao kwa kuonyesha kwamba wanaweza.

Utakumbuka kuwa, beki Steve Ebuela Ehebelo toka tarafani Fizi, Jimboni Kivu Kusini nchini 🇨🇩 alikuwa amesahini mkataba wa miaka 5 kuichezea klabu ya Al Hilal D1 ya nchini Soudan 🇸🇩 na hii ni tangu Januari 2023.
..✍🏼Kama mdau wa soka na mzaliwa wa DRC 🇨🇩 unadhani Steve Ebuela Ehebelo ambaye ni mwamba toka tarafani Fizi atakuja kufanya vizuri na kujizolea sifa k**a Inonga?

🛑 : Baadhi ya Wakimbizi wanaosubiri safari za kwenda nchi ya 3 waitwa Alhamisi kwa njia ya simu kwenye Ofisi za 𝗖𝗪𝗦 inay...
10/07/2025

🛑 : Baadhi ya Wakimbizi wanaosubiri safari za kwenda nchi ya 3 waitwa Alhamisi kwa njia ya simu kwenye Ofisi za 𝗖𝗪𝗦 inayofanya kazi na 𝗥𝗖𝗦 jirani na shule ya Ahadi kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma.
..✍🏼Unahisi kuitwa kwa Wakimbizi hao wanaosubiri kusikia taarifa za safari ya nchi ya 3 kuna heri ao ndio kwenda kuwaongezea presha?

🛑 : Raïs wa Rwanda adai kuwa Tshisekedi hakuchaguliwa bali aliitwa ofisini na kupewa madarakaRais wa Rwanda Paul Kagame,...
10/07/2025

🛑 : Raïs wa Rwanda adai kuwa Tshisekedi hakuchaguliwa bali aliitwa ofisini na kupewa madaraka

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amedai kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi aliitwa ofisini akakabidhiwa madaraka. Amedai mchakato huo ulishuhudiwa na marais wa nchi tatu.

Lakini historia inaeleza kuwa Tshisekedi, alichaguliwa tarehe 31 Machi 2018, kukiongoza chama cha UDPS, baada ya baba yake Étienne Tshisekedi wa Mulumba, kufariki dunia tarehe mosi Februari 2017.

Chama hicho pia kilimteua Felix Tshisekedi kugombea urais katika uchaguzi wa Desemba 2018.

Na tarehe 10 mwaka 2019, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo na kuendelea na jukumu la kuiongoza Kongo.
..✍🏼 Unadhani maneno haya ya Raïs Paul Kagame aliyozungumza mwanzoni mwa wiki hii yana nguvu yoyote kimataifa kwa kuchochea ili raïs Félix Tshisekedi aondolewe madarakani na dola?

⚽ : PSG Yaitandika Real Madrid 4 kavu katika nusu fainali ya kombe la dunia la vilabu🇫🇷 PSG 4️⃣➖️0️⃣ Real Madrid 🇪🇸Timu ...
09/07/2025

⚽ : PSG Yaitandika Real Madrid 4 kavu katika nusu fainali ya kombe la dunia la vilabu

🇫🇷 PSG 4️⃣➖️0️⃣ Real Madrid 🇪🇸

Timu kubwa ya Real Madrid imepoteza matumaini ya kupitia hata kombe 1 msimu huu baada ya kula kichapo kibaya cha 4️⃣ - 0️⃣walichotandikwa na mafundi na bingwa wa Ufaransa, PSG kwenye nusu fainali ya kombe la dunia la vilabu, pambano lililoshuhudiwa Jumatano hii Julai 9, 2025
Mabao yote ya PSG yamefungwa kwenye dakika hizi na wachezaji wafuatao:
⚽️ 06’ Fabian Ruiz
⚽️ 09’ Ousmane Dembélé
⚽️ 24’ Fabian Ruiz (Brace)
⚽️ 87’ Sergio Ramos

✅ Kimekuwa kiwango cha juu kabisa kutoka kwa Paris Saint-Germain wakiishushia kipigo kikali Real Madrid na kutinga fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kwa kishindo!

Mshambuliaji wa PSG, Gonzalo Ramos baada ya kufunga bao dhidi ya Real Madrid alishangalia kwa staili ya kushika pad ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Marehemu, Diogo Jota aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Pumizika kwa amani, DIOGO 🕯️🕊️

🗓️ Jumapili, Julai 13
🏆 Fainali: Chelsea 🆚 PSG

🔥 Ni moto wa London dhidi ya mabingwa wa Paris! Unahisi nani ataibuka kwa mara ya kwanza kuwa bingwa wa dunia?

🛑 : Anayetapeli watu kwa jina la Wakala wa zamani Jean-Claude azidi kuwaliza wengi kambiniMtu anayetapeli watu kwa kutum...
03/07/2025

🛑 : Anayetapeli watu kwa jina la Wakala wa zamani Jean-Claude azidi kuwaliza wengi kambini

Mtu anayetapeli watu kwa kutumia majina ya Jean Claude aliyekuwa Wakala Mkuu eneo la Madukani G1 amezidisha kasi kwenye kutapeli watu kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma.

Chanzo chetu cha siri kilichowasiliana na Jean Claude Nakunge Watangila kimesema; "Huyo mwizi anatumia namba mbili za Voda nazo ni +255759085709 na +255765970093 na ameshawaliza wengi akiwemo Mzee Masopo wa G2, Espe wa K2, mwanaume wa E1 na wengine kibao wa huko Marekani ambapo amekuwa akiwatapeli kati ya shilingi laki mbili na laki nne.

Kutaka kujuwa kuhusu alichozungumza Jean Claude Nakunge Watangila, chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake lianikwe kimesema; "Jean Claude anawasii watu kuwa makini maana yeye hajaombi mtu pesa tangu afikie Marekani na hatumi mtu kwa kuomba pesa kwa jina lake. Kwa hiyo atakayepigiwa simu ao kuandikiwa meseji yoyote ya kuomba pesa kwa jina la Jean Claude ampigie kwanza kwenye namba yake ya +1315264-6465 ao atumie akaunti yenye majina yake ya Jean Claude Nakunge Watangila badala ya akaunti ile yenye jina la Jean Claude pekee."

"Mimi sihusiki na wizi huo wala simtumi mtu, k**a watu hawatakuwa makini; basi watalizwa wengi kwa sababu huyo mwizi anawasiliana na watu wangu wa karibu sana ambao hawasiti kumpa hela"; Jean Claude Nakunge Watangila amesema akiwa na hasira kali kuhusu tapeli huyo aliyeanza kuibia watu kwa jina lake tangu mwezi Aprili mwanzoni.
..✍🏼 Tukiacha njia ya kusambaza taarifa hii kwa ndugu, jamaa na marafiki; unaona ni njia gani nyingine inayoweza kusaidia ili kukomesha utapeli huo unaofanywa na mtu huyo ambaye mpaka sasa hajajulikana?
Tuandikie kwenye maoni kwa faida ya wengine.

😭 : Mwanamke mwengine raia wa DRC aaga dunia huko New YorkJimii ya wakongomani waishio nchini Marekani inayo masikitiko ...
30/06/2025

😭 : Mwanamke mwengine raia wa DRC aaga dunia huko New York

Jimii ya wakongomani waishio nchini Marekani inayo masikitiko masikitiko ya kutangaza kifo cha bibi yao, mama yao na shangazi yao ajulikanaye kwa jina la 'YALA BÚLAKO mke wa Bashi'abulela na mtoto wa Basimukindji aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Jumatatu hii Juni 30, 2025 huko jijini Buffalo mjini New York nchini Marekani.

Taarifa hii ya kifo cha 'YALA BÚLAKO imetolewa na Dunia Mcinde'wa ambaye ni Mwenyekiti wa Babondo mjini New York ambapo amesema kuwa marehemu alikuwa mgonjwa kwa miaka ya kutosha huku akiwaomba Babondo wote walio mjini humo kuambatana na kushirikiana pamoja ili kumzika mpendwa wao k**a lilivyo zoezi la kabila hilo huko Marekani.

Mpaka sasa mpango wa mazishi ya Bi. 'YALA BÚLAKO bado kujulikana na mahali ambako msiba wake ulipowekwa huko kambini Nyarugusu bado kujulikana ila Bwana Mcinde'wa ameonyesha mipango mingine itatolewa hapo baadaye.

Uongozi wa Ukurasa huu unatoa pole kwa familia iliyompoteza mpendwa wao, Mungu azidi kuwafariji na kumpumzisha marehemu kwa amani, amina.

😭 : Mwanaume wa kijiji cha F2 afariki bila kuumwaJamii ya wakimbizi na wakaaji wa kijiji cha F2, zone ya 2 inayo masikit...
28/06/2025

😭 : Mwanaume wa kijiji cha F2 afariki bila kuumwa

Jamii ya wakimbizi na wakaaji wa kijiji cha F2, zone ya 2 inayo masikitiko makubwa ya kutangaza kifo cha baba yao na mjomba ajulikanaye kwa jina la Mmúnga Ba'iye ao Baba Chaku aliyefariki kifo cha kustaajabisha kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma.

Chanzo cha kifo cha Mmúnga Ba'iye kinatatanisha maana wapo wanaosema kuwa alikuwa anaumwa homa akawa pia anakunywa pombe bila kula chakula. Kutaka kujuwa mengine ya ndani zaidi, Kiongozi mmoja wa klasta kijijini F2 ambaye jina halijatajwa amesema; "Kifo cha Baba Chaku kinatisha sana juu hajagonjwa ila tulishtuka kusikia mtu aliyekuwa kwenye pombe jioni hii eti ameanza kujitupa na kulalamika tumbo kukata sana. Hibi bitu habieleweki."

"Baba, hakuna bya kufichana; banasema alikuwa zake sawa asubuhi na mchana yote. Ilipofika jioni, akaenda apate chupa sehemu, tulishtuka kuambiwa hali ya Baba Chaku ni mbaya saa hii. Hapakuwa kingine, tukaambizana tumkimbize hospitalini ila niliona alikuwa ameshakata roho"; amesema msiri wetu mwengine ambaye ni mkaaji wa F2.

Hivyo ndiyo jinsi ambavyo Mmúnga Ba'iye maarufu kwa jina la Baba Chaku anayetajwa kuacha mjane na mayatima zaidi ya 10 alivyofariki ambapo inasemekana kuwa mwili wake umepelekwa nyumbani kwake kwenye klasta ya 1 ya kijiji cha F2, zone ya 2 ila mpango wa mazishi yake bado kutangazwa.

Uongozi wa ukurasa huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wanakijiji cha F2 kwa kumpoteza mpendwa wao ; Mungu awafariji na kumpumzisha Baba Chaku kwa amani.

🛑 : 'Ni Habari za Uongo' - Rwanda yazungumzia uvumi kuhusu afya ya Rais KagameJeshi la Rwanda limesema kuwa kauli iliyod...
25/06/2025

🛑 : 'Ni Habari za Uongo' - Rwanda yazungumzia uvumi kuhusu afya ya Rais Kagame

Jeshi la Rwanda limesema kuwa kauli iliyodai kuwa afya ya Rais Paul Kagame iko "hatarini sana" ni Habari za Uongo.

Kauli hiyo ambayo haijafahamika asili yake, imekuja baada ya taarifa mbalimbali kuibuka kuhusu afya ya Rais Kagame baada ya kutoonekana hadharani kwa takribani wiki tatu.

David Himbara, kiongozi wa upinzani anayeishi uhamishoni na mshauri wa zamani wa masuala ya kiuchumi wa Kagame hivi karibuni amekuwa akidai kuwa Rais Kagame ni mgonjwa, na kwamba yuko Ujerumani.

Gazeti la Rwanda la Taarifa lilimnukuu msemaji wa serikali Yolande Makolo akisema kuwa Rais Kagame ni binadamu k**a kila mtu, ambaye huchukua muda kupumzika.

Gazeti hilo linamnukuu Makolo akisema: "Rais yuko vizuri na anapumzika kawaida." Kutoonekana kwa Rais Kagame hivi majuzi kumetolewa maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii na katika mazungumzo ya faragha.

BBC imejaribu kuwasiliana na ofisi ya Rais kuhusu madai hayo, lakini hadi sasa haijafaulu.

Wakati wengi wakiendelea kuhoji madai hayo, jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali taarifa hiyo na kusema ni 'habari ya uongo'

Rais Kagame alionekana hadharani kwa mara ya mwisho tarehe 6 mwezi huu alipokaribisha kikundi kutoka Shule ya Hope Haven Christian School mjini Kigali, Rwanda.

: Ukurasa wa Facebook wa BBC Swahili

Address

Mapumulo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari Za Nyarugusu CAMP posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share