30/08/2024
[8/21, 11:53 PM] jongo: *HATIA YA MJI*
Kuna kitu kinaitwa hatia ya MJI,
MJI wako unaweza ukaingia kwenye hatia tu kwa makosa ya watu,au mtu mmoja,
Kwa kukosa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni,
Warumi 5:12
[12]Kwa hiyo, k**a kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Dhambi iliingia kwa kukosa mtu mmoja na Mauti ikawafikia wote ,adhabu ya dhambi ulimwengu mzima ulikabiliwa ,
Kuna mambo yanafanyika ndani ya MJI wako yanapelekea wote mwingine kwenye hatia ,
Kuna baadhi ya miji mnajikuta mnaitumikia adhabu kwa kwa hatia MJI ,
Unajua hatuna utaratibu wa KUMULIZA Mungu pale unapotaka kwenda Kuishi mahali,
Huwa tunajiendea tu ,haya ni mambo ya msingi sana kuyajua,
Nimeenda mahali Rea wameweka umeme kila nyumba wameweka nguzo mlangoni lakini hakuna aliechukua umeme,
Umeme wakati huo kuchukua ni 27000,
Uchumi wao wakulima wa viazi,
Sasa naomba tafakari umeme mlangoni Kijiji chote kila mmoja nguzo mlangoni lakini hakuna aliefanikiwa kuingiza umeme,
Umeme umeingizwa shuleni na nyumba ya MWALIMU basi,
Kuna mahari flani vijana wakifikisha umri flani wanakufa ,miaka 35 hawavuki hapo ,
MJI wamebaki wazee,kufanya utafiti walimzika chifu na kijana na kijana ,
MJI ukapokea hatia ya kumwaga Damu,
Vizazi vilivyo faata vikaendelea kumtumikia adhabu ya hatia,
Ni mambo mengi tunakumbana nayo yana chanzo chake,
Kuna miji ambayo wenyewe ni ulevi tu ,
Vijana wadogo unakuta wameharibika ishu ni pombe ,unaanza kukemea pepo kumbe pombe Ina uhalali,
Kuna sehemu zingine Roho ya uzinzi ,unaanza kuwalaumu vijana kumbe hio Roho Ina uhalali,
Wakazi wa njia mnajikuta watoto wenu wanaitumikia adhabu hio kumbe ni hatia ya MJI ,
Pata mda Muulize Mungu mambo Gani yalifanyika hapo zamani kilicho pelekea MJI uingie kwenye hatia,
Wewe ni Nuru mpendwa sisi ndio tunapaswa kubadili ulimwengu huu,,
Sisi tu mawakili wa kristo,
Lazima tufanyike Nuru,changamoto tumekosa umoja,
Baada ya kujisema Mimi WAKILI wa kristo ,
Tunapaswa kukaa katika nafasi,
Ombea MJI wako,Ombea mkoa wako,Ombea inchi Yako,
Lakini ni vema Muombe Mungu akufunulie MJI wako unatumikia adhabu Gani? Naamini ufunuo utakupa na mlango wa kutokea hapo,
Bila ufunuo ni vigumu kushughulikia na jambo usilo lijua ,
Mwanzo 13:13
[13]Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.
Hapo inazungumzwa sodoma,maandiko yanasema watu wa sodoma walikuwa wabaya wenye kufanya dhambi nyingi,
Miji k**a sodoma hapa Tanzania haipo,
Kuna maeneo mengi uovu umekithiri,ishu ni neema tu inatufunika,
Je tunachukua hatua Gani wananuru wa eneo Hilo ,
Chukua hatua k**a Danieli ,
NAOMBA kila mmoja apate nafasi ya KUMULIZA Mungu hatia ILIYOMO kwenye eneo unalo ishi,eneo la kazi ,eneo la ibada ,
Unahangaika kutafuta upako kumbe eneo mlilo Jenga kanisa
Ilikuwa NGOME ya wachawi ,ilikuwa madhabahu,je mmeshilikisha Mungu kuziangusha madhabahu ya baali ,bila Mungu hapo usitegemee K**a Kuna mambo ya kiroho yatasogea hapo hakuna,
Ustawi wa uchumi,wa inchi hutegemea wanachi kiwango chako Cha utii juu ya Mungu,hakuna ustawi wa uchumi KIBIBLIA kinyume na utii wa kanuni na Taratibu za kiungu,
Hakuna kulaumi uchumi ,uchumi Ili ustawi kibiblia lazima wananchi wake wafundishwe utii juu ya Mungu na kutoa ,mafanikio mengine kinyume na biblia Mimi hayo hayanihusu,
Nasema Ili jamii ustawi kiuchumi lazima ifundishwe utii juu ya Mungu , ifundishwe kumtolea Mungu ,hakuna mafanikio kinyume na hapo KIBIBLIA,yapo mafanikio au ustawi wa uchumi kinyume na biblia upo ,Mimi nasema ustawi wa uchumi wa inchi kiblia,
Ifike mahali viongozi ,washika nafasi za juu ,tupate wenye hofu ya Mungu,ambao watawafundisha wanachi wao Kuishi maisha ya utii,watawafundisha maisha ya kufanikiwa kiblia,
Wanachi wakifanikiwa ichi imefanikiwa,
Hatukai kwenye nafasi Ili kuombea inchi zetu,tupate viongozi walio kusudiwa ,niwakati wa majira ya uchaguzi sasa Muombe Mungu atupe viongozi alio wakusudia ,
HATIA ya MJI mara nyingi inaweza ikatokana na kiongozi,
Kiongozi anae waongoza inategemea yupo chini ya Mungu yupi?
roho chini ya mungu wa kiongozi alie madarakani ndio zinawaongoza,
AHSANTE Yesu neema ya Mungu imetufunika Tanzania ,Kuna Siri kubwa mno hapo sio SoMo lake Huko,
Kumbukumbu la Torati 32:7
[7]Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi;
Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;
Wazee wako, nao watakuambia.
Kuna mambo mengi sana
Naomba tuishie hapo Mungu atusaidie na utuwezeshe Amen
[8/31, 1:08 AM] jongo: KUMSIKIA MUNGU
1 Samweli 3:4-10
[4]basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.
[5]Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.
[6]BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.
[7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
[8]BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto.
[9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
[10]BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile k**a kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.
Hapa tunajifunza habari ya samweli juu ya kumsikia Mungu ,
Samweli alikuwa akiitwa na Mungu lakini kiwango chake Cha kumsikia Mungu kilikuwa kidogo ,hakuwa na ufahamu wa kutosha wa kuweza kumsikia Mungu ,
Maandiko yanasema
1 Samweli 3:9
[9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
KUMBE kumsikia Mungu kunafundishika,
Je upo tayari kufundishika? Je umemuomba Mungu akupe Eli wako?
1 Samweli 3:10-11
[10]BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile k**a kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.
[11]BWANA akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.
Kiwango chetu Cha ufahamu ni KIZUIZI Cha kumsikia Mungu,
Kiwango chetu Cha ujazo wa neno wa Neno ni KIZUIZI kumsikia Mungu
1 Samweli 3:7
[7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
Tunapaswa tuwe na ujazo wa kutosha wa Neno Ili tumsikie Mungu ,
Ndani ya Neno Kuna uhai na uzima,
Ndani ya Neno Kuna Kweli na Kweli inatuweka huru,
Ndani ya Neno Nuru na Nuru inatuangaza kila tupitapo
Ndani ya Neno Kuna sauti ya Mungu,
Neno la Mungu ni mawazo ya Mungu,
Ndani ya Neno Kuna Maisha ,
Kiwango chako Cha ujazo wa Neno ni sawa na kiwango Chako Cha Mungu Kujifunua kwako,
Hautaweza kumsikia Mungu zaidi ya kiwango chako Cha ujazo wa Neno ,
Neno Ndilo linalo funua Siri za Mungu,
Neno ni mawazo ya Mungu,
Ufahamu wako juu ya Mungu HAKUTAKUWA zaidi ya kiwango Cha ujazo wa Neno ndani Yako ,
Kiwango Cha ujazo wa Neno ndani Yako ni ukuta wa kiwango Cha ufahamu wako,
Kiwango Cha ujazo wa Neno ni kizuizi Cha kumsikia Mungu
Ili uvuke ukuta wa kiwango chako Cha ufahamu lazima kiwango Cha ujazo wa Neno kiongezeke,
Kiwango Cha ujazo wa Neno kikiongezeka ,kiwango Cha ufahamu juu ya Mungu kitaongezeka pamoja na kiwango Cha kumsikia Mungu kitaongezeka ,kwani Neno la Mungu ndani Kuna sauti.
NAWATAKIA USIKU MWEMA
MUNGU AWABARIKI