17/07/2025
Msimu wa 2011 alijiunga kutoka polisi morogoro akiwa na miaka 19 tu na alicheza SIMBA kwa misimu miwili tu na kutokana na juhudi zake na kipaji chake SIMBA waliamua kumfungulia Dunia ambapo walimuuza kwenye klabu ya Cannes ya ufaransa ila huko mambo hayakumuendea sawa ndipo azam wakaenda kumnunua ambako alichezea azam kwa misimu mitatu 2014-2017
Shomari alikuwa na kiwango bora akiwa azam na SIMBA waliendelea kumtolea macho na msimu wa 2017 rasmi walifanikiwa kumchomoa na akarudishwa nyumbani ambako alicheza kwa juhudi, kujitolea na kwa kiwango cha juu sana
Toka 2017-2025 tayari shomari keshaitumikia SIMBA kwa miaka 8 na ameendelea kuwa ni kipenzi cha wanasimba wote na ameendelea kuipambania SIMBA kwa Jasho na damu
Kwa Sasa ana miaka yake 33 ila kutokana na kiwango chake na nidhamu yake bora SIMBA wanaendelea kumpa heshima kwa kumuandalia mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia SIMBA
na cha kufurahisha zaidi kwenye misimu yote shomari ajawai kuweka ugumu wala kuisumbua simba wakati wa kusaini mkataba mpya mara zote anaipa kipaumbele simba na amekuwa mtiifu sana kwa SIMBA
True legend π«‘π«‘π«‘π«‘π«‘