05/12/2024
BUNDA.
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini BUNDA (BUWSSA) imetambulisha mradi mpya wa maji katika kata ya Wariku Halmashauri ya mji wa bunda.
Mradi huo unatarajia kugharimu shilingi bilioni 1,620,121,364.90 mpaka kukamilika kwake , utekelezaji wake ni wa muda wa miezi sita umeanza tarehe 1 mwezi wa 12 , 2024 mpaka tarehe 31 mwezi wa 5 ,2025 hadi sasa umefikia asilimia 8.
Akitambulisha mradi huo Katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Kamkenga ,Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini bunda ,Esther Gilyoma amesema kupitia wizara ya maji inaendelea kutekeleza na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama pia mradi huo utaenda kunufaisha jumla ya wakazi 33,088 katika kata ya wariku.
Gilyoma amesema kuwa kazi zitakazotekelezwa katika mradi huo ,uchimbaji wa mtaro km 40, ununuzi wa bomba,ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita 200,000,ununuzi wa pampu ya kusukuma maji ,na tayari mzabuni ameshapeleka bomba za maunganisho mapya kwa wateja mia moja hamsini
Naye Katibu Tawala wilaya ya bunda SALUM MTELELA kwa Niaba ya mkuu wa wilaya ya bunda, ametoa tahadhari kwa watu wote wanaojipanga kuhujumu miundombinu inayotekelezwa na serikali amesema kuwa serikali haita sita kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kufanya hivyo
KWA upande wa wakazi wa kata ya wariku wameishukuru serikali kwa kuleta mradi huo ambao utawasaidia kupata maji kwa wakati hasa nyakati za kiangazi .
Mradi huo ukikamilika utasaidia maeneo ya nyandago, kamkenga, kangetutya, na mumanyago kupitia tangi lenye ujazo wa lita 200,000 linalojengwa shule ya msingi wariku mtaa wa mumanyago .