Hasanaatu TV

Hasanaatu TV Page hii inahusu kusambaza Yalio mema na Kukumbushana kwa yanayo tuzunguka katika jamii

𝗠𝗔𝗛𝗠𝗢𝗨𝗗 𝗠𝗔𝗬𝗘𝗟𝗘(FISTON  MAYELE)Mshambuliaji wa zamani wa Yanga {Raia wa DRC Congo} ambae kwa sasa anakipiga Kwenye klabu ...
16/07/2025

𝗠𝗔𝗛𝗠𝗢𝗨𝗗 𝗠𝗔𝗬𝗘𝗟𝗘
(FISTON MAYELE)
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga {Raia wa DRC Congo} ambae kwa sasa anakipiga Kwenye klabu ya Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele amebadilisha dini kutoka kuwa Mkristo na sasa ni Muislamu

Ripoti zinaeleza kuwa Mayele amebadilisha dini miezi sita iliyopita na hata kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan alikuwa akijumuika na wenzake waliofunga

Uamuzi wa Mayele kubadili dini ulisababishwa na wachezaji wenzake wa Pyramids FC, haswa Ramadan Sobhi na Karim Hafez, na inaripotiwa kuwa maamuzi hayo aliyafikia kipindi cha mwezi wa Ramadhani.

Baada ya kubadilisha dini kwa sasa Mayele hatambuliki k**a Fiston Mayele bali amechagua jina la Mahmoud na hivyo anaitwa Mahmoud Mayele.

Anasema Allaah (ﷻ) Mtukufu:

{ إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ }

"Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,"

{ وَرَأَيۡتَ ٱلنَّاسَ يَدۡخُلُونَ فِي دِينِ ٱللَّهِ أَفۡوَاجٗا }

"Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,"

{ فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُۚ إِنَّهُۥ كَانَ تَوَّابَۢا }

"Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba".

[Surat An-Nasr: 1-3]

Ungana nasi kwa habari sahihi
na zenye uhakika

Follow Us



Fahamu yalio mema

16/07/2025

UPDATES

INNA LILLAHI WA INNA
ILAIHI RAJIUN

MSIBA MKUBWA !!

AMEFARIKI {15-07-2025}
HAFIDH MKUBWA WA QUR'AN TUKUFU NA KIJANA ILIYE ITUMIKIA QUR'AN NA KUIFANYIA KAZI HAFIZ
SOW
KUTOKA NCHI YA COTÉ D'IVOIRE, PIA ALIKUA MSHINDI WA 1 KWENYE MASHINDANO MAKUBWA YA QURANI TUKUFU MWAKA JANA { 2024} YALIO ANDALIWA NA Al-Hikma Qur'an Competition CHINI YA USIMAMIZI WA SHEIKH NURDIN Kishki Jijini Dar es salaam nchini Tanzania

Hakika kifo ni fumbo, tuishi katika misingi anayo iridhia na kuipenda Allah, hakika kijana ameondoka akiwa na umri mdogo kwanza ndo Ana umri wa myaka 15 na sababu ya kifo chake ni maradhi ya muda mfupi, tunataraji kheri na mafikio mazuri kutokana na utukufu wa Qur'an aliyo ibeba katika kifua chake, hakika alikua kijana mwenye mfano wa kuigwa hasa katika ulimwengu wa Qur'an, kwani alishindana Mashindano mengi ya Qur'an ndani na nje ya nchi yake na alikua akiibuka mshindi Alhamdulillah...

ALLAH Amrehemu na amsamehe alipo teleza na Allah ajaalie Quran iwe ni utetezi wake Aamiin

Ungana nasi kwa Habari
Sahihi na za uhakika

Subscribe & follow Us




To Allah we belong and to him we all shall return.
We are saddened to announce the death of our Dear brother, Qari Ibrahim Sow from Ivory Coast,

He was the winner of the Tanzania International Quranic competition just last year 2024.
He is well known for his powerful recitation and participation in many international and local Quranic competitions.

May Allah Overlooked his mistake and grant him the highest part of Jannah.

Foe more
Subscribe & follow Us

UPDATESHABARI NJEMA KUTOKA JIJINI BUJUMBURA NCHINI BURUNDIHATUA NZURI KUTOKA KWA SHEIKH  .NA UONGOZI WA  Baada ya kufany...
13/07/2025

UPDATES

HABARI NJEMA KUTOKA JIJINI BUJUMBURA NCHINI BURUNDI

HATUA NZURI KUTOKA KWA SHEIKH .
NA UONGOZI WA

Baada ya kufanya Ziara yaki Da'awah nchini Burundi kwa siku kadhaa, Leo Alihitimisha Ziara yake kwa tukio kubwa na Lakihistoria nchini humo, na hayo yamefanyika akiwa sambamba na M***i wa Burundi (Pichani na Sheikh kishki) Tukio Hilo ilikua ni kufungisha ndoa ya kihistoria ya watu mia moja (100) kupitia taasisi yake ya .

Katika Siku ya leo Jumapili ya tarehe 13/07/2025.
Ndani ya Jiji la

Allah Amlipe Sheikh kila la kheri
Napia kila aliye shiriki katika
Kukamilika kwa Jambo Hilo
Allah amlipe kheri kwa nia njema

Jiunge nasi kwa Habari za
Kheri na zenye uhakika





Fahamu yalio mema.

25/06/2025

Alhamdulillah Tumeingia katika mwaka mpya wa kiislam_Muharram 1447 H

EID MUBARAKA kwa Waislamu wote Duniani   Ungana nasi kwa mengi zaidi
05/06/2025

EID MUBARAKA
kwa Waislamu
wote Duniani




Ungana nasi kwa mengi zaidi

SIKU 10 ZA MWANZO KATIKA DHUL HIJJAH _______________________{} "KUMI LA MWANZO LA DHUL-HIJJAH" 👇Katika siku hizi kumi, k...
28/05/2025

SIKU 10 ZA MWANZO
KATIKA DHUL HIJJAH
_______________________

{} "KUMI LA MWANZO LA DHUL-HIJJAH" 👇

Katika siku hizi kumi, kuna: 👇🏾

1- Siku ambayo kufunga ni makubaliano ya wote, nayo ni siku ya Arafah.

2- Siku ambayo haifungwi kwa makubaliano ya wote, nayo ni siku ya Eid (Yawm an-Nahr).

3- Na kuna siku ambazo kuna tofauti ya maoni, nazo ni zile siku nane za mwanzo.

Kauli iliyo na uzito zaidi ni kuwa inapendelewa kufunga siku yoyote inayowezekana kati ya hizo, kwa kuwa ni miongoni mwa matendo mema.

Mtume ﷺ amesema:

> "Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko katika siku hizi (kumi)."

Wakasema: Hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Akasema ﷺ:

> "Hata jihadi, isipokuwa mtu aliyetoka na nafsi yake na mali yake, kisha asirudi na chochote (yaani, akapoteza vyote kwa ajili ya Allah)."
(Riwaya ya Bukhari)

Kazi bora kabisa ya ibada katika siku hizi, ambayo wanazuoni wote wamekubaliana kuwa ni sunna, ni kutamka dhikr kwa sauti kubwa, yaani kumkumbuka Allah kwa sauti.

Allah Ta'ala amesema:

> (“…na walitaje jina la Allah katika siku maalumu…”) — Al-Hajj: 28

Ibn Abbas (r.a) amesema:

> "Siku maalumu ni siku kumi za Dhul-Hijjah."

Na Ibn Umar na Abu Hurairah (r.a) walikuwa wakitoka kwenda sokoni katika siku hizi na wanatoa takbira kwa sauti, na watu wengine walikuwa wakitakbiri kwa kusikia takbira zao.

(Riwaya ya Bukhari kwa njia ya ta’liq lakini ni yenye hukumu ya kuaminika)

Miongoni mwa takbira sahihi zaidi ni hizi mbili:

(1) . Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, la ilaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahil-hamd.

(2) . Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar kabīrā, Allahu a‘lā wa ajall, Allahu Akbar wa lillāhil-hamd.

Ungana nasi kwa elimu na mengi mazuri na sahihi kabisa Kisha Share kwa wengine


Fahamu yaliyo mema

UKUMBUSHO KUHUSU HIJJAH
30/04/2025

UKUMBUSHO KUHUSU HIJJAH


𝗦𝗛𝗘𝗞𝗛 𝗦𝗪𝗔𝗟𝗘𝗛 𝗔𝗟 𝗙𝗔𝗪𝗭𝗔𝗔𝗡 Shekh Abdul Aziz Ibn Baz (Allah Amrehem), alipoulizwa ni nani tumuulize baada yako, akajibu: "Al...
26/04/2025

𝗦𝗛𝗘𝗞𝗛 𝗦𝗪𝗔𝗟𝗘𝗛 𝗔𝗟 𝗙𝗔𝗪𝗭𝗔𝗔𝗡

Shekh Abdul Aziz Ibn Baz (Allah Amrehem), alipoulizwa ni nani tumuulize baada yako, akajibu: "Al-Fawzan"..

Shekh Muhammad Ibn Uthaymiyn (Allah Amrehem) alipoulizwa ni nani tumuulize baada yako, Akajibu: "Muulize Al-Fawzan."
Aliwahi kusema: Moyo hutulizwa na fatwa za Sheikh (maana yake Al-Fawzan)...

Huyu ndiye Sheikhul Islam (Shekh wa Uislamu) katika zama hizi na ni katika wenye elimu kubwa Alhamdulillah ...

Allaah Amlinde Sheikh wetu mbora, mwanachuoni na Doktor Muhammad Swaleh bin Fawzan Al-Fawzan, Allah Amzidishie umri na Aziongoze hatua zake, yeye na masheikh wote watetezi wa Sunnah . Aamiyn🤲

𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗙𝗕 𝗣𝗔𝗚𝗘

Eid Mubaaraka to all MuslimsAllah atupokelee matendo yetu
29/03/2025

Eid Mubaaraka to all Muslims
Allah atupokelee matendo yetu



MWANDAMO WA MWEZI KWA WATAALAMU WA ELIMU YA NYOTAMakala hii Imeandikwa na mtaalamu bingwa Dkt Swalaah AamirTafsiri ya Ki...
28/02/2025

MWANDAMO WA MWEZI KWA WATAALAMU WA ELIMU YA NYOTA

Makala hii Imeandikwa na mtaalamu bingwa Dkt Swalaah Aamir

Tafsiri ya Kiswahili:

Mwandamo wa Mwezi wa Ramadhani 1446 Hijria - 2025 Miladia

1. Kwanza: Kwa mujibu wa hesabu za falaki
Mwezi mwandamo utakuwa upo baada ya jua kuzama siku ya Ijumaa tarehe 29 Shaaban. Kwa hivyo, kwa wanaotegemea hesabu za falaki, Ramadhani itaanza Jumamosi, Machi 1.

2. Pili: Kwa mujibu wa kuona kwa macho
Mwezi mwandamo unaweza kuonekana kwa macho usiku wa Jumamosi katika nchi za Afrika na Amerika.
Katika eneo la Rasi ya Kiarabu, utaweza kuonekana kwa kutumia darubini, na hivyo Jumamosi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mwezi huo utadumu angani kati ya dakika 20 hadi 32, kulingana na nchi mbalimbali. Urefu wake utakuwa takriban nyuzi 5, na pembe ya kujitenga takriban nyuzi 7. Umri wa mwezi utakuwa saa 14 au zaidi, kulingana na eneo la mtazamaji.

Hali ya kuona mwezi katika Asia ya Mashariki:
Mwezi mwandamo hauwezi kuonekana katika nchi nyingi za Asia ya Mashariki k**a China, Malaysia, na Indonesia. Kwa hivyo, ikiwa nchi hizi zinashikilia sharti la kuona mwezi kwa macho ndani ya mipaka yao, Ramadhani itaanza Jumapili.
Hata hivyo, ikiwa wanatumia hesabu za falaki au kufuata mtazamo wa walio wengi kwamba mwandamo mmoja unatosha kwa dunia nzima, basi Ramadhani itaanza Jumamosi pia.

Muhtasari

Nchi zinazotegemea hesabu za falaki: Ramadhani inaanza Jumamosi.

Nchi zinazotegemea kuona kwa macho:

Mwezi hauonekani kwa macho katika Asia ya Mashariki → Ramadhani inaanza Jumapili.

Mwezi unaonekana kwa macho katika Afrika na kwa darubini katika Rasi ya Kiarabu → Ramadhani inaanza Jumamosi.



البث المباشر لجائزة تنزانيا الدولية للقرآن الكريم في دورتها الثالثة عشرة ٢٠٢٥هLive The Tanzania International Holy Quran...
23/02/2025

البث المباشر لجائزة تنزانيا الدولية للقرآن الكريم في دورتها الثالثة عشرة ٢٠٢٥ه
Live The Tanzania International Holy Quran Award 13th Season 2025

🔴 LIVE MASHINDANO YA DUNIA YA QURAN TUKUFU, 2025 _ KWA MKAPA DSM FEB 23Follow Us On:INSTAGRAM: https://www.instagram.com/miladu_tv/FACEBOOK: https://www.fac...

11/02/2025

Address


Telephone

+27724656380

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hasanaatu TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Hasanaatu TV:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share