15/12/2025
MAPITO YANGU
Sehemu ya 1
Victor, nimechoka sana, ebu niache. Ntakupa kesho na sipo sawa. Mimi nnaumwa, au wewe unaniona niko sawa? RINA acha kunizungua. Unaelewa wewe? Yaani acha kunizingua kabisa. Kwahiyo unataka humu ndani wewe ule bure, uvae bure, au sio? Sitaki upumbavu. Panda kitandani unipe. Sitaki kutumia nguvu kabisa. Nimechoka sasa, kwanini lakini? Aseeee, sikumaliza hata maneno nikapigwa kibao kikali. Daah, yaani kuchoka kumbe ni kosa nalo? Tena ni kosa kubwa mpaka naadhibiwa. Ila huyu kaka jamani. Akaniambia sikia nna tamaa na wewe. Mbona jana sijakushika? Oyaa, usinivuruge, vua nguo, kaaa pale juu ya kitanda. Mnadhani nafanyaje sasa? Nikavua nguo kwa kinyonge sana, nikapanda kitandani. Nikalala chali.
Victor naye akavua nguo zake. Akanipanda kwa juu, akaanza kushughulika na mimi. Aseeee, sijawahi kusikia raha yoyote kushiriki tendo na huyu mwanaume. Always ni huwa k**a ananinyanyasa tu, wala hakuna cha zaidi. Nikamwacha akajihudumia mpaka aliporidhika. Akaninuka, akavaa suruali yake tu ya chini. Nguo nyingine akabeba akatoka chumbani kwangu. Aseeee, moyo unauma sana. Ni mwaka sasa tangu niolewe na huyu mwanaume. Sio tu mwanaume, Victor ni mume wangu wa ndoa. Nimefunga naye ndoa kabisa ya kanisani. Yaani yeye ni mume na mimi ni mke. Ila acheni tu. Ngoja nijitambulishe kwenu.
Mimi naitwa Marina Frank Justine. Wengi wamezoea kuniita Rina. Mimi bwana, baba na mama walifariki nikiwa kidato cha sita. Na shuleni nilikuwa nna akili kweli kweli. Ila wazazi walipofariki, hata kidato cha sita sikufanikiwa kumaliza sababu ya ada. Maana ndo ilikuwa naingia kidato cha sita na wazazi wanafariiki. Nilikuwa nasoma shule ya private hapa hapa mkoani Morogoro. Na ndo nilipokuwa naishi na wazazi. Ila sasa baada ya kufariki, shoga yenu nikachukuliwa na shangazi. Aseeee, shangazi yangu ni mlevi mbwa. Mnajua ni mlevi! Yaani kwanza nilikuwa nateseka sana. Yeye ndo alikuwa anaiba nguo zangu anaenda kuuza, anapata pesa ya kunywea pombe. Yaani badala anisaidie yatima, ndo akawa anazidi kunididimiza. Aseeee, alikuwa na wanawe 2. Na wao akili zao k**a za mama yao jamani. Nimeishi nao kwa shida sanaaa. Ila shangazi yeye alikuwa anaishi Moro vijijini huko.
Sasa shangazi ndo aliniletea huyu mchumba eti niolewe. Sikuwa nataka kuolewa kabisa. Sababu k**a msichana bado nilikuwa nna ndoto zangu. Ila wapi, unadhani walinisikiliza? Sababu mnajua, Victor bwana ni mwanaume ambaye ana pesa zake mno. Na ni mfanya biashara mkubwa. Hapo Morogoro mjini kila mtu anamfahamu. Alipokuja kwa shangazi kusema anataka kunioa, yaani shangazi hakujiuliza. Wala hakuniuliza, ni moja kwa moja ilipitishwa ndoa. Niliumia sana. Na k**a masihara nikaolewa nikiwa na miaka 19 tu. Ndo nikakutana na huyu mwanaume. Wala sikuelewa kwanini alinioa maana hata yeye hakuwa ananipenda kabisa. Na haya ndo yanayonitokea kwenye hii ndoa, ambayo mpaka muda huo nilikuwa nna mwaka 1 natesekaaaa.
Sehemu ya 2
Kwanza Victor hakuwa anataka nitoke niende kokote kule. Naweza kusema mimi ni mtu wa ndani tu. Tena ndani kwake ana ulinzi mkali. Kuanzia getini mpaka ndani. Victor ni k**a mfanyabiashara wa vitu haramu naweza kusema. Maana niligundua anajihusisha na biashara za siri na haramu japo ana kampuni kubwa ya bidhaa anayoimiliki. Huyu kaka ukimuona ni very smart ila ana roho mbaya sijapata kuona. Victor kunipiga ni kawaida. Anapiga vibaya sana. Sitamanigi kumuudhi kwa chochote. Kiukweli hii ndoa kwangu ni mateso. Mimi sitoki nje. Na nikitoka ni kwa dharura sana, tena ni lazima ntakuwa na yeye may be. Amealikwa party na wenzie, na anatakiwa kuwa na partner ndo atanichukua. Na sio mara zote anakuwa na mimi. Labda k**a anafukuzia deal la biashara ili asionekane muhuni ndo ntaenda nae. Mimi nikiumwa ilikuwa Daktari anakuja kunitibia sio mimi kutoka. Hapo nilipokuwa nakaa hakuwa anakanyaga yeyote hata ndugu yangu. Na wala mimi sijawahi kumuona ndugu yeyote wa Victor. Wala sielewi chochote kumhusu kuhusu ndugu zake. Yaani shangazi alinitupa mimi.
Victor hakuwa mkubwa sana. Kipindi ananioa mimi huyu kaka alikuwa na k**a miaka 35. Mimi nna 19. Ila sasa ni k**a kanioa kujituliza kingono. Mimi sifanyi kazi yoyote kwake. Ana wafanyakazi wawili wa kiume. Ndo wanafanya kazi zote. Mimi kazi yangu ni kumburudisha yeye tu. Na hakuna siku ananiacha. Atalala na mimi kila siku. Yaani mara chache chache sana, ndo anakuwa ananiacha hapo hayupo nyumbani. Ndo napona. Victor haelewi nna umwa, haelewi nipo katika siku zangu. Haelewi chochote na hajali kitu. Yeye akitaka mimi nimpe tu. Naumia sanaaaaa juu ya huyu mwanaume.
Kingine Victor hataki nizae. Ameshanitoa mimba 4 tangu tumefunga ndoa. Issue anataka tendo la ndoa muda wote na anamwagia ndani ila hataki nizae. Nawezaje? Nikidaka mimba tu, anaitwa nesi anakuja kunitoa. Aseeeee, nilikuwa ni mwanamke wa kuumia sana. Ila sina sauti. Siwezi kuongea wala kusema, namuogopa Victor kuliko nyoka. Maana Victor mara kwa mara huwa anaongea na simu kisha anawapa watu amri za kutisha. Aseeeee, huyu mwanaume acheni! Naweza kusema niliishi na mtu mwenye tabia za hatari. Yote haya ni shangazi ambaye anapewa pesa kutuliza. Sifikirii hata k**a alikuwa ananiulizia mimi na hayo ndo yalikuwa maisha yangu.
Basi alivyotoka chumbani kwangu, nikajua kaenda chumbani kwake maana hatulali pamoja sisi. Na nashukuru silali naye daah. Mwanaume anatosha huyu. Yaani ukimuona kwa nje na kwa ndani anatisha sana Victor. Basi nikainuka kinyonge sana, nikaenda kuoga. Nikatoka, nasikia mlango unagongwa. Nikatoka nakuta ni Bige. Huyu Bige ni moja wa house boy humu ndani. Akaniambia: "Madame nikuletee chakula ndani ama nikakutengee mezani?" Nikasema: "Nimeshiba leo, sijisikii kula kabisa." Akasema: "Sawa madame. Ila ungekula kidogo." Mimi sikutaka maongezi, nikabamiza mlango wangu. Nikavaa zangu, nikajilaza kitandani. Nishika tumbo langu maana tayari nishagundua nna mimba nyingine. Na lazima Victor atoe hii mimba. Mpaka kuna muda nilikuwa nahisi kabisa Victor atakuwa ana ushirikiano fulani na hizi mimba anazozitoa ni k**a dhabihu. Sikuwa namuelewa kabisa. Na naanzaje kumuuliza, namuogopa mno. Yaani Victor anatisha. Akirudi humu ndani kila mtu anaogopa. Aseeee, acheni tu haya maishaaaa. Sikuwa na jinsi tu. Basi nikavuta shuka langu nipumzike tu. Ila niliwaza sana, haya maisha mpaka lini? Inamaana ntazeeka nikiwa mtumwa wa ngono? Niliwaza kabisa kutoroka, na ikiwezekana nimuokoe huyu mtoto.
Sehemu ya 3
Basi nikajipumzisha zangu tu. Namuelewa Victor, akishanitumia huwa hajali chochote kuhusu mimi. Nimekula ama sijala ni sawa. Anakuwa busy na mambo yake na maisha yake. Kwa muda wote huo ambao nimekaa naye, sijawahi kumuelewa Victor. Hata napenda nini, hata anapenda kufanya nini. Hata rafiki yake wa karibu simjui. Victor ni mtu wa peke yake peke yake. Na mara nyingi anakuwa ni mtu wa hasira tu. Ndo yupo hivyo. Mimi kupigwa naye ni dakika 2. Namuogopa sana huyu mwanaume sijawahi kuwa na raha naye hata siku moja. Na bikra mimi akatoa yeye ila wapi. Hakuna jipya yaani.
Basi nikalala nikiwa na mawazo sana. Asubuhi nikaamka mapema, nikaoga na nikavaa vizuri. Nguo huwa ananinulia sana tu. Ila huwa anaagiza watu wananiletea. Hata nikitaka kutoka nae, ataniagizia nguo na mtu wa make up. Yaani kwake pesa haijawahi kumsumbua kabisa. Na pesa tu anayo. Basi nikakaa tu kitandani maana sikutaka kuonana naye hii asubuhi kabisa mimi. Maana najua huwa anakunywa chai aende kazini. So nikatulia sana. Mpaka saa 3 ndo nikatoka sasa. Nikamuuliza Mike, kwamba ameshaondoka huyu? Mike akaniambia: "Ndio madame." Huyu Mike naye pia ni house boy. So kuna house boy wawili mmoja ni Mike na mwingine ni Bige na wote naelewana nao tu. Na wanaona shida ninazopitia kwa huyu baba. Ila na wao ndo wapo kimya. Ila hapo huyu Mike huwa anaenda na kurudi, ila Bige ndo kila siku na masaa 24 yupo. Na hii nyumba ni kubwa na ya kifahari sana. Yaani ya kifahari, mbona nikisema huyu baba ana pesaaaa, aseeee ana pesa kweli.
Basi Mike akaniambia: "Ndio ameshaondoka." Ndo nikaenda mezani nikachukua yai moja tu nikala nikaacha. Wala sikujisikia kula tena. Nikaenda chumbani kwangu kupumzika. Mchana nilipitisha chakula nikasema ntakula jioni. Aseee, hapo yote ni mawazo juu ya hii ndoa. Yaani sikuwa na mwili wangu kabisa. Nilikonda kiukweli kwa mawazo. Na ndoa hii ilikuwa ngumu sana. Hapo nimekaa, na jua akirudi tu anakuja kutaka kukidhi tamaa zake. Na hana muda wa kumuandaa mwanamke. Yaani ni ananiingilia tu mpaka anakuwa ananichana huku chini. Aseee, acheni!
Basi hii siku mpaka saa 3 usiku nikasikia kimya. Ndo nikatoka chumbani sasa. Nikamkuta Bige. Akaniambia: "Vipi madame?" Nikasema: "Kwani huyu hajarudi?" Akasema: "Hapana madame. Leo wala hajarudi na mpaka muda huu saa 3 labda haludi maana anarudigi saa 12 kamili jioni, unamkuta home." Aseee, hii siku nikafurahi kweli kutokurudi kwake. Nikatamani hata apate ajali ya gari afeeeee huko. Yaani nilikuwa namuombea mambo mabaya tu, huo ndo ukweli. Basi nikatoka zangu nikala chakula cha usiku. Ndo nikaenda zangu kupumzika. Na kweli hii siku nililala mpaka asubuhi salama kabisa. Mzee si hayupo.
Basi asubuhi nikaingia bafuni. Nikaoga vizuri. Ile natoka tu namkuta Victor kakaa kitandani kwangu kisha kashika bastola anaitazama. Aseeee, niliogopa sana, yaani nilishtuka mno. Victor akaniambia: "Unaiogopa hii silaha? Wala usikonde. Hii imetoka kufanya kitendo cha hatari usiku wa kuamkia leo. Na wala sio wewe Rina. Naomba haki yangu. Maana jana sijakuk**ata kabisa." Aseeee, nikamsogelea tu. Akanivua nguo na yeye akavua. K**a kawaida akaniparamia. Akanishughulikia mno. Mpaka akakojoa akaniacha, akavuta bastola yake akaingia ndani. Aseeeee, huyu kaka, huyu ataniua mimi!
Sehemu ya 4
Basi aliporidhika sasa akaniacha. Kisha akaniangalia sana, nikashtuka mbona hili jicho? Akaniuliza: "Una mimba?" Aseee, nikashtuka tena. Nikasema: "Hapana." Akaniuliza: "Unanidanganya mimi?" Nikasema: "Victor mimi sina ndugu, naomba kuzaa plsss." Victor akasema: "Kelele! Mpumbavu wewe. Nani kamwambia mimi nataka mtoto, mjinga wewe? Kwanini unajiachia mpaka unazaa, mbwa wewe? Nimesema sitaki unizalie nini, huelewi?" Nikabaki naumia tu. Hapo hapo akampigia simu nesi wake. Akamwambia: "Oyaa njoo ufanye kinachomhusu kwa huyu mwanamke, kabeba tena mimba."
Aseeeee, akainuka kwa hasira akatoka chumbani kwangu kavimba kweli kweli. Nikabaki nimekaa kitandani tu huku nalia. Maana daaah, haya mambo haya! Basi haikupita hata dakika 30, nesi akaja alafu ni mdada tu. Akanipa vidonge vya usingizi. Nikazima, akanitoa tena na hii mimba. Ilikuwa ni mimba yangu ya 5. Niliposhtuka nililia sana. Yule nesi akaniambia: "Unalia nini? Ebu acha kujiachia kwake. Mtu hataki kuzaa na wewe, atakuwa anakuuliwa watoto kila siku, mwisho atakuja kukua na wewe mwenyewe. Poleee. Au unadhani atakupenda huyu kwa kumzalia?" Aseeee, Victor namjua. Sio wewe tu, hata hawala zake wa huko nje wote anawatoa mimba. Na mimi ndo nawatoa mimba. Nikamwambia: "Nashindwa namzuiaje sasa?" Yule dada akaniambia: "Sikia nikwambie. Nakuweka kijiti, atakuua huyu." Nikasema: "Sawa." Basi akaniweka kweli kijiti. Akaniamba: "Hapa hutazaa tena, poleee." Nikasema: "Asante." Yule nesi akaondoka zake. Aseeee, niliumwa wiki 2. Kutoa mimba sio suala dogo. Huo muda wote naumwa, huyu mwanaume hakuwa na muda na mimi kabisa. Na hakuwa hata anajulia hali kabisaaa. Siku hiyo ndo kidogo nimeanza kupata afadhali. Khee, naona ndo kaja chumbani kwangu sasa.
Akaniambia: "Nimekuja kupata huduma leo." Khaaa! Nikasema: "Kwani Victor, hujui k**a nnaumwa? Si umetoka kunitoa mimba kuwa kwa maslahi yako. Hata sijapona vizuri, unataka tena hayo mambo? Sitaki!" Victor akaniangalia kisha akasema: "Ebu ongea tena sijakusikia, na umenivimbishia sauti kabisa mimi sio?" Nikasema: "Bwana nimechoka, k**a vipi niue tu!" Akasema: "Okey." Akanisogelea akanikaba kweli kweli. Nyie, mpaka pumzi ilikuwa inataka kukata. Ndo akaniacha, nikaanza kutweta na kukohoa sana. Na nikawa nahemea juu juu. Akasema: "Vipi? Nikumalizie kukukuua? Na uzuri shangazi yako nikimpa pesa tu, wala haulizi tena kuhusu wewe." Nikabaki namuangalia tu. Maana hana masihara huyu mwanaume kabisa. Kananiambia: "Vua nguo. Nimelipa mahari mimi kukuoa. Tena shangazi yako alitaka pesa kubwa mno. So usinivuruge. Issue zako za kuumwa hazinihusu, sababu nilishakueleza kuwa usibebe mimba. So k**a umebeba mimba, basi mimi sihusiki, full stop." Nyie, huyu baba ni mwenye ukatili.
Hamuwezi amini. Sijapona vizuri akaniingilia tena kwa muda mrefu. Niliumia sana. Yaani sanaaaa. Aliporidhika akavaa zake akasepa. Niliona huyu mwanaume ni muuaji, atakuja siku moja kuniua kabisa. Nikaona huyu nimuue mimi. Nikaona ngoja huyu ntamuua siku sio nyingi. Basi nikaenda kuoga nikavaa kisha nikatulia chumbani kwangu nikiwaza sana nimfanye nini huyu mwanaume ili niwe huru na maisha yangu. Maana mimi kutoka tu siruhusiwi yaani maana walinzi wanakijua hilo. Yaani mimi ni ndani, mimi hata simu sipewi yaani. Na sina simu kabisa. Nipo k**a mtumwa tu. Na sina raha ya maisha yoyote ninayoipata.
Sehemu ya 5
Basi mimi nilipotoka kuoga sasa. Nikatoka zangu sebuleni tu ata nije kuangalia TV. Ile nafika sebuleni nakuta yupo Victor. Alikuwa anaangalia mpira ila k**a usingizi umempitia hivi. Aseee, sikuhoji. Nikaingia jikoni nikavuta kisu. Kisha nikatoka sebuleni. Nikamsogelea taratibu. Kisha haraka nikataka kumchoma. Wee, yaani ile ghafla akafumbua macho akanidaka kile kisu. Nikawa najitahidi kumshindilia ila wapi, kanisukuma. Akaniambia: "Daah, umefikia pabaya sana! Wewe ndo unataka kuniua mimi? Wewe unataka kuniua, nakuuliza?" Nikasema: "Ndio nataka kukuua. Na k**a nimekukosa leo, basi siku yoyote nakuua, nakwambia! Sikupendi, nakuchukia sana, mshenzi wewe! Unafanya maisha yangu kuwa ya mateso mno!" Victor akacheka kisha akavuta glasi yake ya pombe. Akanimwagia usoni. Kisha akniuliza: "Unaota au bado nikumwagie nyingine?" Nikanyamaza kimya. Akaniambia: "Leo umenikosea sasa ntakuonesha." Akanivuta nakwambia. Nikawa nagoma ila akawa ananiburuza kwa nguvu. Nikawa nasema: "Sitaki jamani, niache! Niache!" Kwani ndo alinisikiliza? Akawa kanipeleka nje ya nyumba kuna chumba kingine kidogo. Halafu kubaya mno. Sikuwahi kuingia ila niliogopa maana nilikuwa naona mpaka michirizi fulani ya kutisha. Victor akaniambia: "Sikupigi wewe. Ntakuua halafu ntakosa demu mwenye mwili mzuri k**a yako. Ila utakaa humu kwa siku 5." Aseee, akanifungia kisha akanizimia na taa.
Aseeee, kile chumba ni kinatosha yaani. Kwanza mchana ni giza, usiku ni giza kisha kinanuka harufu mbaya. Na hakina dirisha huko. Nilipiga kelele kweli kweli za uoga. Ila wapi! Nyie, nilijibanza pembeni kabisa naogopa. Natetemeka. Nahisi k**a nauliwa. Kile chumba kilikuwa kinatisha mnooo. Niliogopa sana mimi. Mungu wanguu. Nilikaa mle mpaka asubuhi k**a masihara. Na serious nilikaa siku 3 tu nilichoka mno. Yaani nilichoka. Njaa inauma na mle k**a kuna hali ya kutisha. Aseee, mpaka siku ya 5, ndo Victor alikuja kunifungulia. Akaniburuza mpaka nje. Hata nguvu sina na bado sikuwa sawa kiafya. Akaniambia: "Ukijaribu kuniua tena, na wewe ndo utakuwa mwisho wa maisha yako, mpumbavu wewe!" Aseeee, akiniacha hapo hapo njeeee. Akaondoka zake kazini. Na Mike na Bige ndo walikuja kunisaidia wakaningiiza mpaka chumbani. Nikajikokota nikaenda kuoga kwanza. Maana na mimi nilikuwa k**a nanuka vibaya. Yaani nilielewa kuwa kile chumba Victor anafataga vitendo vya ukatili. Nyie naishi na mwanaume gani huyu?
Nilipotoka kuoga nikavaa vizuri ndo kina Bige wakanipa uji kwanza. Maana sikuwa nimekula chochote kwa siku 5. Aseee, acheni kabisaa. Nikanywa uji. Nikatibua tumbo. Nikaenda kutapika uji wote. Nilipotapika sasa nikaona nipumzike tu. Nikanywa dawa nikalala maana tayari k**a nilishaanza kuhisi nna homa kali. Aseee, nililala siku nzimaaa mimi. Jioni kabisa ndo kina Mike waliniletea chakula cha maana. Nikala. Kisha Mike aliomba kuongea na mimi sasa. Huyu Mike ni k**a mimi umri wake ila Bige ni mkubwa kwangu. Mike akaniambia: "Pole sana madame." Nikasema: "Asante." Mike akaniambia: "Madame kuwa mpole. Huyu mtu ni hatari zaidi ya unavyohisi wewe. Kwanza humu ndani ana kamera. Kwa mfano hapa anaona k**a nipo chumbani kwako nnaongea na wewe." Nikashtuka nikasema: "Kumbe!" Akasema: "Ndio. Ila nahisi asikii sauti. So huwa namwambiaga nakusikiliza tuu utulie na ache kumsumbua, ila tulia. Sisi tunamjua na kumuelewa sana Victor atakua kweli. Na wewe bado ni mdogo na una malengo yako. Wewe tulia, mimi ntakusaidia kutoroka hapa. Na ntakupa mbinu za kumtoroka." Nikasema: "Ntashukuru sana Mike. Ntashukuru mno." Akaniambia: "Sawa nipo pamoja na uwe na amani." Nikasema: "Sawa." Kisha Mike akaondoka.
Aseee, hapo nilipata tumaini jipya mimi. Nikaona k**a ntatoloka itakuwa safi kabisa. Nikasema ntaenda mbali wallah, huyu kaka hatakaa akaniona mimi. Basi hapo nikapata amani kabisa. Nikabaki nimejilaza kitandani huku nimetabasamu kweli kweli. Nikiona tumaini jipya na kujichomoa kwa huyu firauni mshenzi kabisa, muuaji.