23/09/2025
🔥"THE SHADOWS OF NAIROBI"🔥
EPISODE 8
Tulikuwa tumeshuka street, tukitembea faster kuliko kawaida, lakini wale wasee bado walikuwa nyuma yetu. Si kwa umbali sana, si karibu sana. Ile type ya follow yenye inakufanya ujue hii game haiko soft.
Nairobi usiku ilikuwa busy matatus zikihonk, vibanda vya chips zikifuka moshi, na maboys wa mtaa wakipiga freestyle pale corner. Ilikuwa perfect cover, lakini pia ilikuwa perfect hunting ground.
“Lucy,” nikamwhisper, “hatuwezi enda straight home. Tutaingia ndani ya crowd tupotee.”
Nilimshika mkono, tukapiga shortcut ndani ya estate ndogo pale Globe roundabout. Tukapitia kwa mtaa wa vibanda, tukijipenyeza kati ya watu. Lucy alikuwa anahema, lakini alikuwa soldier. Hakulia, hakupanic alishikilia tu mkono wangu tight.
Niligeuka kidogo, nikaona wale wasee bado wako nyuma, lakini sasa wamegawanyika wawili wawili, wakijaribu kutukata.
Brain yangu ikawork overtime.
“Ok, option moja tunaingia kwa mat basi, tupotee tu,” nikasema.
Bahati ikacheka matatu ya rongai ikafika pale stage, ikipiga ngoma za latest gengetone. Tukakimbia ndani, tukakaa nyuma kabisa. Driver akarusha accelerator, na vile tukaingia highway, niligeuka—wasee walikuwa kwa pavement, wakiangalia matatu, lakini hii ilikuwa too late. Tulikuwa tumewashinda.
Lucy akapumua kwa nguvu, akishika kichwa. “Wafwana… hii life siwezi handle peke yangu. Nilijua sooner or later hii itaingia kwa maisha yako, lakini sikuwa najua itakua fast hivi.”
Nikamuangalia, nikasema kwa tone ya soldier:
“Lucy, chill. Wacha tukufeel hii moment. Nairobi ni yetu tonight. Hata k**a shadows ziko nyuma yetu, mi niko na wewe.”
Akaniangalia, macho yake yakiwa na mchanganyiko wa fear na tenderness. Akanishika mkono tight, akasema softly:
“You don’t know what you’ve signed up for, Wafwana. But I’m glad it’s you.”
Matatu ilipiga turn, ikashuka kwa barabara ya Mbagathi, na vile maboys walipiga kelele na ngoma ziliendelea, mimi na Lucy tulijua game imebadilika. Hii sasa ilikuwa survival, na hakuna kurudi nyuma.
Like, drop any comment or emoji to unlock episode 9👇👇👇
Thanks for reading