
25/03/2024
Israel imekubali kuwaachilia wafungwa mia saba (700) hadi mia nane (800) wa Kipalestina badala ya mateka arobaini (40) wa Israel ambao bado wanashikiliwa na Hamas.
Iwapo watafanikiwa, mabadilishano hayo yatakuwa sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, ambayo yameingia mwezi wa tano (5) sasa.