18/11/2024
Jinsi ya Kuishi na Mtu Ambaye Anakukatisha Tamaa Kila Kitu
Kila mkiongea, anatafuta namna ya kukufanya ujione k**a hufai, akitumia maneno k**a “huna akili,” “huwezi kufanikiwa,” “nilikuambia hiki kitu hakiwezekani,” au “acha mambo ya kijinga.” Anatafuta kasoro kwenye kila kitu unachofanya na hajawahi kuona mazuri yako; kila wakati ni mapungufu tu.
(1) Kwa Nini Anafanya Hivi? Je wewe ni Mjinga kweli?
Hili ni swali la kwanza na la muhimu kujiuliza. Mtu huyu anaweza kuwa hajiamini mwenyewe. Inawezekana alikulia kwenye familia iliyokuwa ikimkatisha tamaa au ametokea kwenye mazingira yenye changamoto, k**a umaskini au mapungufu ya kimaumbile yanayomtesa, na hivyo hawezi kujithamini. Alishawahi kudharauliwa na Mwanamke/Mwanaume wake wa zamani!
Anahisi umemzidi kila kitu, na kwa akili zake, anaamini ukifanikiwa zaidi kuliko yeye utamdharau au kumuacha. Kwa hiyo, anajaribu kukushusha ili ujione k**a hufai.
(2) Tambua Thamani Yako, Furahia Mafanikio Yako!
Unapaswa kujua kuwa thamani yako ni sawa na pesa kwa mfano elfu kumi, hata k**a watu wakisema ni chafu, inanuka, haina thamni, hainunui chochote bado haibadilishi thamani yake. Jitambue kuwa unaweza kufanya biashara, kazi yako ni bora, na unajitambua mwenyewe. Maoni yake hayawezi kubadilisha ukweli huo.
Fanya mambo kwa ajili yako, na si kwa kumfurahisha yeye, kwa sababu kadri unavyojaribu kumfurahisha, ndivyo anavyozidi kukudharau. Fanya mambo kwa ajili yako!
(3) Weka Mipaka ya Mambo Unayomuambia Usitangaze sana mafanikio yako kwake.
Anapokuona hutafanikiwa, muache aendelee kuwa na mawazo hayo. K**a unataka kupanua biashara yako, fanya kimyakimya na usimwambie malengo yako yote. Wakati mwingine, muache aone matokeo tu.
(4) Kuwa na Malengo Yako na Fanya Kazi na Wanaokuunga Mkono!
Weka malengo yako ya kibinafsi na fanya kazi kwa ajili ya hayo malengo. Tafuta watu wanaokuunga mkono, hata k**a ni marafiki zako, dada yako, au mtu mwingine ambaye unajua atakuelewa na atakutia moyo. Hii itakusaidia kutegemea maoni yeny