08/07/2025
MABINGWA WA LIGI KUU BURUNDI AIGLE NOIR WAKWEA P**A KWENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI.
Timu ya Aigles Noirs CS kutoka mkoa wa Makamba imeondoka Jumanne, Januari 8, 2025, kuelekea Afrika Kusini ambako inaenda kujiandaa na msimu wa 2025-2026.
Wawakilishi hao pia wa Burundi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika wataweka kambi ya takribani wiki tatu na kucheza mechi za kirafiki na baadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu Burundi.
Msimu mpya wa ligi kuu Burundi utaanza Agosti 22, kabla ya hapo, Aigle Noirs CS itacheza na Flambeau du Center mnamo Agosti 16 katika mchezo wa Super Cup..
Kufikia sasa, Aigle Noir ndiyo timu pekee nchini Burundi ambayo husafiri kwenda nje ya nchi kujiandaa na mashindano mbali mbali.
Itakumbukwa kuwa mwaka wa 2024, kabla ya kuanza kwa ligi kuu Burundi, Aigle Noirs CS alikuwa imeweka kambi nchini Tanzania.