07/08/2026
Ujumbe wa msanii Sapologuano Odenumz Yakutumba kwawale waliyo kuwa wakiongeye mengi sana kuhusu yéyé kuto kufika msibani kwa hayati
👇
🗣️Puuzeni habari wanazozisambaza watu mitandaoni kwamba sikuenda kumzika msani mwenzangu
Kwanini watu hawakosi maneno? Kila siku maneno mengi.
Muda mwingi nilikuwa kimya sana. Sikutaka kuongea, ila nimeona niongee sasa.
Nimeona habari zimetembea sana. Wengi wakizusha kwamba sikuwepo msibani kumzika msani mwenzangu, kaka yangu, ndugu yangu .
Hiyo ni maneno ya kuzusha tu. Wala huwezi kuwakataza watu kuongea wanavyojisikia.
Mimi nilifika msibani na nilihudhuria taratibu zote za kumpumzisha ndugu yangu.
Sikuenda msibani ili nipige picha au video niposti kuwa nilikuwa msibani.
Pale ni msibani, na msiba una heshima yake.
Ambao walikuwa wanalala msibani pale waliniona, kwa maana nilikuwa ninalala pale msibani kwa siku kadhaa, na nilihudhuria mambo mbalimbali kwenye msiba.
Sisi Waafrika hatuna moyo wa kushindwa kuhudhuria misiba ya wapendwa wetu waliotutangulia. Maana wametangulia wao, nasi tutafuata, kwa maana hiyo ndiyo njia yetu sote.
Tuache maneno mengi ya kuongeaongea. Cha muhimu ni kumuombea Mungu ndugu yetu aendelee kupumzika mahali salama 🙏🏻