MESA9 TV Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de MESA9 TV, Chaîne de télévision, Democratic Republic of the.

07/09/2024
07/09/2024

Wilaya ya Kilindi ni kati ya wilaya 10 za Mkoa wa Tanga katika Tanzania. Imepakana na wilaya ya Handeni upande wa mashariki, Mkoa wa Kilimanjaro upande wa magharibi-kaskazini na Mkoa wa Morogoro upande wa kusini.

Mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 236,833 walioishi katika kata 20 za wilaya hiyo.

Makao makuu ya wilaya yapo Kata ya Songe.

KATA ZA WILAYA YA KILINDI

Bokwa
Jaila
Kibirashi
Kikunde
Kilindi
Kilwa
Kimbe
Kisangasa
Kwediboma
Kwekivu
Lwande
Mabalanga
Masagalu
Mkindi
Msanja
Mvungwe
Negero
Pagwi
Saunyi
Songe
Tunguli

13/07/2024

Nikitu Gani ambacho hutakisahau ulikifanya wakati wa janga la covid 19 ?
Follow &like@mesa9tv

Changamoto Gani umekutananayo wakati unatuma maombi ya ajira kwenye MFUMO wa ajira wa ajira portal ???
13/07/2024

Changamoto Gani umekutananayo wakati unatuma maombi ya ajira kwenye MFUMO wa ajira wa ajira portal ???

18/05/2024
ASKOFU MKUU AKABIDHI MABATI KITUO CHA POLISI NKINGA TABORA Askofu Mkuu Mch. Stevie Mulenga kwa niaba ya halmashauri kuu ...
18/05/2024

ASKOFU MKUU AKABIDHI MABATI KITUO CHA POLISI NKINGA TABORA

Askofu Mkuu Mch. Stevie Mulenga kwa niaba ya halmashauri kuu ya kanisa amekabidhi mabati 130 kwa mkuu wa wilaya ya Igunga Mhe Sauda Mtondoo kwaajili ya jengo la kituo cha polisi kilichopo Nkinga wilayani Igunga.

Askofu Mkuu ametoa mabati hayo ikiwa ni ahadi walio toa kwa kituo cha polisi cha Nkinga machi mwaka huu walipokuwa wakifanya vikao vya halmashauri kuu ya kanisa ambapo Mkuu wa kituo alifika kuzungumza na Halmashauri kuu na kuomba kuchangiwa mabati kwaajili ya ukamilishaji wa kituo cha polisi Nkinga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe Sauda Mtondoo ameshukuru kanisa kwa kushiriki katika ujenzi wa kituo hicho cha polisi na kufungua mlango kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia .

Nae k**anda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema ni jambo zuri kuona kanisa linashiriki katika kuunga mkono serikali katika ujenzi wa Taifa.

Mabati hayo yenye thamani ya zaidi ya milioni nne yamekabidhiwa mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora, viongozi wa dini, chama ,serikali na wanakijiji wa Nkinga.
Follow na like page yetu

17/05/2024

Makamu Mwenyekiti wa Tundu Lissu akikagua gari lake ambalo alikuwa amelipanda siku aliyejeruhiwa kwa risasi na leo Mei 17, 2024, Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limemkabidhi gari hilo.

Lissu alipigwa risasi Septemba 7, 2017

 : Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), umerejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye mwongozo wa Taif...
08/05/2024

: Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), umerejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye mwongozo wa Taifa wa matibabu lakini hazikuwemo kwenye Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIST) ambapo umezijumuisha dawa hizo kwenye Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.
NHIF imeeleza hayo kupitia taarifa yake kwa umma ambapo imeeleza kuwa hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini.
Kutokana na maboresho hayo, Mfuko wa Taifa Bima ya Afya unawahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa nchi nzima na endapo kutakuwa na changamoto za kiutekelezaji.
Follow page yetu

Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kitakachoondoka kesho Jumatano Mei 8, 2024 kuelekea Saudi Arabia kwa michezo miwi...
07/05/2024

Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kitakachoondoka kesho Jumatano Mei 8, 2024 kuelekea Saudi Arabia kwa michezo miwili ya Kirafiki na Sudan

Toa maoni yako kwenye comment section na like na kufollow page yetu
07/05/2024

Toa maoni yako kwenye comment section na like na kufollow page yetu

  Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema ameeleza kuwa hakuna vita ya nafasi ya kugombea Urais nda...
06/05/2024

Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema ameeleza kuwa hakuna vita ya nafasi ya kugombea Urais ndani ya Chama hicho katika uchaguzi ujao huku akisema amewahi kumsikia Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu akiweka wazi kuwa hawezi kuchukua fomu ambayo imeguswa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe

Kumekuwa na mijadala mitandaoni ikieleza kuwa kuna mvutano wa nani agombee nafasi ya urais ndani ya chama hicho

"Nimeona andiko la BOB Wangwe na maandiko mengine ya watu wengi pamoja na ushauri wake.Jibu langu kwenu ni hili, tukiwa Arusha mahali fulani kwenye mazungumzo yetu ambapo nilikuwepo pamoja na Kamanda Wenje, Heche,Msigwa na Mkti F.Mbowe, Mh Lissu aliongea maneno haya "

“ Nanukuu “ Kaka , Mwenyekiti , ulibeba chupa ya damu nisife wkt nimeshambuliwa kutoka Dodoma ukiwa umesimama kwenye ndege mpaka Nairobi,na ulikaa Nairobi na wenzako hawa muda wote wa matibabu yangu , siwezi kuchukua fomu utakayogusa kwenye Chama hiki,tusiruhusu wapambe watuharibie CHAMA "

"Maneno haya niliyasikia Mimi, Heche, Msigwa, Wenje na Mwenyekiti Mbowe.Hakuna vita kwenye nafasi ya Urais CHADEMA isipokuwa kuna wapambe wajinga na CCM haswa ktk muelekeo wa siasa 2024/2025" ameandika Lema kwenye kitandao ya kijamii
Follow na like page yetu kupata updates zaidi

Tupe uzoefu na uelewa wako  kwa kutoa comment hapo chini tujifunze kutoka kwako(Follow na like  page  mesa9tv)
05/05/2024

Tupe uzoefu na uelewa wako kwa kutoa comment hapo chini tujifunze kutoka kwako
(Follow na like page mesa9tv)

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, leo May 05,2024 amewasilisha katika Mahak**a Kuu ya Tanzania ma...
03/05/2024

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, leo May 05,2024 amewasilisha katika Mahak**a Kuu ya Tanzania masijala ya Arusha ombi la kuiondoa rufaa No.155 ya Mwaka 2022 aliyokuwa ameikata dhidi ya Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake saba ya kudaiwa kujipatia Tsh. milioni 90 kwa Mfanyabiashara Francis Mroso.

Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi hiyo ya Uhujumu uchumi No.27 ya mwaka 2021 katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha iliyosikilizwa na kuamuliwa na Hakimu Patricia Kisinda.

Wakili wa Sabaya Moses Mahuna amesema Sabaya hana lengo la kudai fidia na kilichofutwa ni rufaa iliyotokana na kesi na kwa sasa yupo huru na hana kesi yeyote na kwamba kwa mujibu wa Mahak**a yenyewe Sabaya kwa sasa hana rekodi yoyote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria na kumfanya kumalizana rasmi na Mahak**a.

Kufuatia hatua hiyo Sabaya anakuwa na sifa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
(Follow page yetu mesa9tv)

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, Lissu amedai kuna pesa  zinatembezwa na baadhi ya wagombea wa uchaguzi...
03/05/2024

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, Lissu amedai kuna pesa zinatembezwa na baadhi ya wagombea wa uchaguzi ngazi ya kanda ya Nyasa ili kushawishi wapiga kura wawachague, huku akihoji kwa nini katika masuala mengine ya msingi watu hawatoi pesa lakini kwenye uchaguzi zinaonekana.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Alhamisi kwenye viwanja vya Mwembetogwa, mkoani Iringa, Lissu amesema; “Tuna uchaguzi ndani ya chama chetu sisi wenyewe na wakati nakuja hapa Iringa jana na juzi kulikuwa na mtafaruki mkubwa sana sijui k**a mnafahamu? Kuna pesa nyingi ajabu kwenye uchaguzi huu mnafikiri inatoka wapi na itatuacha salama?”

26/04/2024

updates

Adresse

Democratic Republic Of The

Téléphone

+255683971996

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque MESA9 TV publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L'entreprise

Envoyer un message à MESA9 TV:

Partager