09/09/2026
Prof. Hamadi Iddi Boga ni mwanasayansi, msomi na kiongozi wa umma kutoka Kwale County, mwenye utaalamu mkubwa katika Microbiology na Microbial Ecology.
Prof. Boga alizaliwa tarehe 3/12/1967 Diani-Mwaroni, Kwale County. Alianza elimu yake shule ya Mvindeni Primary School, kabla ya kujiunga na Voi Secondary School kwa masomo ya sekondari.
Mwaka 1990, alihitimu BSc in Botany and Zoology – First Class Honours kutoka Kenyatta University. Baadaye alipata MSc in Microbiology/Botany kutoka chuo hicho hicho.
Mwaka 2000, alipata PhD in Microbiology/Microbial Ecology kutoka University of Konstanz, Germany 🇩🇪. Pia alifanya utafiti wa baada ya udaktari (Postdoctoral Research) katika Max Planck Institute, Germany🇩🇪, kati ya mwaka 2005 na 2006.
Prof. Boga amekuwa na safari ndefu katika sekta ya elimu ya juu na utafiti. Alifanya kazi Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT), akipanda katika nyadhifa mbalimbali hadi kufikia cheo cha Professor of Microbiology/Microbial Ecology.
Katika safari yake ya uongozi wa kitaaluma, aliwahi kuwa:
• Chairman, Department of Botany – JKUAT- 2002
• Director, Institute of Biotechnology Research - 2005
• Dean, Faculty of Science - 2007
• Principal, JKUAT Taita Taveta Campus 2007 - 2009
• Founding Principal, Taita Taveta University 2009 - 2012
• Acting Vice Chancellor, Taita Taveta University 2012 - 2016
Mwaka 2018, Prof. Boga aliteuliwa kuwa (Katibu) Principal Secretary, State Department for Agricultural Research katika Wizara ya Kilimo. Chini ya Serikali ya Uhuru Kenyatta
Baadaye alihudumu pia katika State Department for Crop Development and Agricultural Research.
Katika uwanja wa kimataifa, Prof. Boga amehudumu katika taasisi mbalimbali zinazohusika na utafiti, kilimo na maendeleo.
Taarifa ya mwaka 2026 kutoka European Union Delegation Kenya inamtaja k**a Vice President for Program Delivery katika Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), akihusika na usimamizi wa programu zinazolenga kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo barani Afrika.
Pia amewahi kuhudumu katika bodi za taasisi za utafiti na maendeleo ya kilimo, zikiwemo ICIPE (International Centre of Insect Physiology and Ecology) Ni taasisi ya kimataifa ya utafiti wa sayansi ya wadudu na ikolojia Na ICRAF International Centre for Research in Agroforestry. ICRAF pia inajulikana k**a World Agroforestry na inafanya utafiti kuhusu miti, kilimo-mseto (agroforestry) na mazingira.
Kwa ujumla, Prof. Hamadi Iddi Boga ana karibu miongo mitatu (30 years) ya uzoefu katika sayansi, elimu ya juu, uongozi wa vyuo, sera za kilimo, utafiti wa maendeleo ya kilimo na uhusiano mwema na mashirika Na mataifa ya nje.