
08/07/2025
Ripoti zinaeleza kuwa Winga na Nyota wa Simba SC, Kibu Denis ameanza majaribio ya wiki mbili kwenye moja ya klabu kubwa inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani (MLS).
Klabu hiyo inataka kumtazama kwa ukaribu nyota hiyo kabla ya kutuma ofa ya kwanza Simba.
Inaelezwa kuwa raia huyo wa Tanzania anataka kucheza Ligi ya Marekani ili aweze kuwa karibu na familia yake, pia winga huyo ana ofa zingine kutoka kwa Mabingwa wa Morocco na Kombe la Shirikisho Afrika RS Berkane, MC Alger ya Algeria na Al Ahli Tripoli ya Libya.
Ikumbukwe Kibu amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Simba,hivyo hatoondoka bure Msimbazi.
*Simba mpo tayari kujenga timu tena msimu ujao Yanga wakibeba Makombe yao?π
*