Emmanuel Otto

Emmanuel Otto Media and Advertisers Broadcasting & Media Production

21/08/2026

TUNDU LISSU ANAISHIA HAPA KWA LEO.

Nilisimamisha masomo ya Masters ili kuja kushiriki uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, for the record, Jimbo la Singida Kusini.

Ukiachia ushiriki huu, vilevile nimeshiriki kwenye masuala ya uchaguzi k**a wakili wa wagombea ubunge wa chama au wabunge waliochaguliwa wa chama tangu mwaka 2005.

Napenda kuamini kwamba kwenye masuala ya kesi zinazohusu uchaguzi ni mjuaji, mjuaji kweli kweli, mjuaji kuliko mawakili wengi hapa nchini.

Kuna majaji wa mahak**a hii na Mahak**a ya Rufani wamejifunza mengi kutoka kwangu. Na kusema hivi sio kujitapa, bali ni kusema tu nafahamu sheria nyingi zinazohusiana na uchaguzi.

Nje ya ujuzi wa sheria kutokana na kuwa wakili, kuanzia mwaka 2021 mpaka wakati nak**atwa mwaka jana, nimefanya utafiti mkubwa sana kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi, sio tu sheria bali mfumo mzima.

Tangu enzi za ukoloni mpaka leo hii.

Nisingekuwa napotezewa muda Ukonga, ningeshaandika kitabu kuhusu mfumo wa uchaguzi wa nchi hii na machafu yake.

Kwa sababu ya ufahamu wote huo wa masuala ya uchaguzi, nimekuwa mstari wa mbele kabisa kupambania mfumo mpya na huru wa uchaguzi.

Hakuna hoja yoyote ya uchaguzi ya CHADEMA ya miaka hii kumi ambayo haijapitia kwenye mikono yangu.

Shauri limeahirishwa mpaka Jumatatu.

21/08/2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA

Na mimi ni Makamu Mwenyekiti ninayewakilisha bara zima la Afrika.

Waheshimiwa Majaji, ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima, wa heshima kubwa ndani ya nchi hii na kimataifa.

Na heshima niliyo nayo ni kwa sababu ya msimamo wangu wa kupigania haki, demokrasia na utawala wa sheria. Sio kwa sababu nyingine.

Waheshimiwa Majaji, mwezi Mei 2011, nilipewa tuzo ya heshima ya kuwa Mwenza wa Kimataifa (International Fellow) wa Chuo Kikuu cha Bridgeport, kilichopo Jimbo la Connecticut nchini Marekani.

Sababu ya heshima hiyo ni muhimu kuwekwa kwenye rekodi ya mahak**a.

Walisema ni kwa sababu ya kupigania haki za binadamu, mazingira na demokrasia katika nchi yake ya Tanzania na barani Afrika.

Waheshimiwa Majaji, mwezi Desemba 2020, nilitunukiwa heshima nyingine na IDU, tuzo inayoitwa Bush–Teature Award for Freedom.

Na sababu yake ni muhimu kuwekwa kwenye ushahidi:

“Tundu Lissu, umekuwa ni kielelezo cha msimamo thabiti wa kupigania haki, demokrasia na utawala bora katika nchi za Afrika.”

Ni muhimu iingie kwenye ushahidi kwamba, hata pamoja na mashtaka haya, pamoja na kukaa gerezani muda wote huu, heshima yangu katika nchi hii na duniani haijapungua; na, in fact, imeongezeka.

Waheshimiwa Majaji, taasisi nyingi sana za kitaifa, kikanda na kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Madola, zimesema haya mashtaka ni mashtaka ya kisiasa; hakuna cha uhaini wala jinai yoyote. Ni siasa.

Na wamedai niachiliwe huru bila masharti yoyote.

Baraza la Haki za Binadamu la kimataifa, sio tu limedai niachiliwe bila masharti, bali nilipwe fidia kwa usumbufu wote na changamoto zote nilizopata tangu kufunguliwa kwa mashtaka haya.

Naomba iingie kwenye ushahidi kwamba nchi za Jumuiya ya Ulaya zimesimamisha misaada kwa Tanzania kwa sababu ya mashtaka haya.

Na Marekani imesimamisha misaada takribani dola milioni 700, kwa mujibu wa taarifa zangu, kwa sababu ya mashtaka haya.

Kwa sasa, Bunge la Marekani linajadili mswada wa kuwawekea vikwazo Serikali ya Tanzania na viongozi wake kwa sababu ya mashtaka haya.

Waheshimiwa Majaji, dunia haiwezi kukupigania hivi k**a wewe ni mtu wa hovyo hovyo.

Dunia haiwezi ikakupigania hivi k**a wewe ni mhalifu.

Dunia inakupigania kwa sababu wewe ni mtu wa heshima.

Waheshimiwa Majaji, shtaka dhidi yangu linahusu kauli niliyotoa tarehe 3 Aprili 2025 kuhusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Nilichotaka kusema, Waheshimiwa Majaji, ni kuwa shtaka linahusu uchaguzi.

Mimi nina uzoefu mkubwa sana na masuala ya uchaguzi wa Tanzania.

Nilipiga kura mara ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 1985, nikiwa na umri wa miaka 18.

Na kati ya mwaka huo 1985 na mwaka jana, nimeshiriki katika uchaguzi mkuu aidha k**a mgombea au mpiga kura katika chaguzi zote, isipokuwa uchaguzi wa mwaka 2000 na maafa yale ya mwaka jana.

Nimeshiriki katika kila uchaguzi mkuu tangu mwaka 1985, isipokuwa mwaka 2000 na mwaka jana; mwaka 2000 kwa sababu nilikuwa nafanya kazi Marekani, na mwaka jana nilikuwa gerezani.

Kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Uingereza, nilirudi Tanzania kuja kugombea.

21/08/2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA

Na nilitumikia nafasi hiyo hadi tarehe 29 Juni 2019.

Ilikuwaje nikatumikia kabla ya kipindi kuisha?

Narudi kwenye tarehe 7 Septemba 2017, ambapo nikiwa Dodoma kwenye vikao vya Bunge, nilifuatwa kutoka Bungeni mpaka kwenye makazi yangu rasmi na kushambuliwa kwa risasi, risasi nyingi sana, na watu ambao Serikali ya Tanzania inawaita watu wasiojulikana.

Kufuatia shambulio hilo, nilikimbizwa Hospitali ya Dodoma na siku hiyo hiyo nikasafirishwa Nairobi, Kenya, ambako nilikaa hospitalini mpaka tarehe 4 Januari 2018.

Baada ya hapo nilipelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven.

Nilikuwa nikihudhuria matibabu mpaka Januari 2022. Kati ya Nairobi na Ubelgiji nilifanyiwa operesheni 25; operesheni 17 katika Hospitali ya Nairobi na operesheni nane katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven.

Waheshimiwa Majaji, mkiona navuta mguu na kuchechemea, ni kwa sababu ya tukio hilo.

Nikiwa hospitalini, tarehe 29 Juni 2019, aliyekuwa Spika wa Bunge, marehemu Job Ndugai, alitangaza kunifuta ubunge, kwa kuwa nilikuwa mtoro na sijaonekana Bungeni kwa miaka miwili.

Miaka miwili inafika, hajui nilipo. Ndiyo maneno aliyoyasema.

Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea nisimalize term ya pili ya ubunge wangu.

Na kwenye hili niongeze, kwa sababu ni muhimu katika kesi hii: licha ya kuwa Mbunge na kuumizwa vibaya nikiwa Bungeni, Bunge na Serikali ya Tanzania ilikataa kata-kata kulipa gharama za matibabu. Sikupewa hata senti moja ya matibabu, licha ya sheria ya uendeshaji wa Bunge inayoelekeza kuwa Mbunge akipata changamoto yoyote ya kiafya ana haki ya kutibiwa na Bunge. Bunge lile lilikataa.

Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa naelezea masuala ya personal record, kipindi nikiwa Bungeni nilikuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, effectively kiongozi namba mbili katika uongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wa kwanza akiwa Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani, ambaye wakati huo alikuwa Mheshimiwa Mbowe.

Vilevile, Waheshimiwa Majaji, nilikuwa msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa masuala ya Katiba na sheria, masuala ya Muungano, pamoja na Mwanasheria Mkuu Kivuli (Shadow Attorney General).

Waheshimiwa Majaji, Mahak**a irekodi kuwa nimefanya kazi yangu ya ubunge kwa uaminifu mkubwa na kwa umahiri.

Kipindi hicho, kuanzia 2011 hadi 2014/2015, nilikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Na kwa kipindi hicho, Waheshimiwa Majaji, Bungeni niliongoza harakati za kupigania Katiba mpya na mfumo huru wa uchaguzi. Kilichonileta hapa kwa ushahidi wangu si uhaini, bali ni mgogoro mkubwa wa kisiasa wa kupigania Katiba mpya na mfumo huru wa uchaguzi.

Tuliongoza mapambano haya Bungeni kwa uaminifu mkubwa na umahiri.

Nje ya ubunge, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika tangu mwezi Machi au Aprili 2017 mpaka Septemba 2017 niliposhambuliwa.

Nilichaguliwa na mawakili wa nchi hii kuwa Rais wao.

Hauwi Rais wa Chama cha Mawakili wa nchi hii k**a wewe ni mtu wa hovyo hovyo, laini laini.

Nje ya uongozi wa mawakili wenzangu, hapa nilipo, Waheshimiwa Majaji, ni Makamu Mwenyekiti wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani, kwa Kiingereza International Democrat Union (IDU).

Shirikisho linalounganisha zaidi ya vyama 80 vya siasa around the world.

IDU ni muunganiko wa vyama vya kidemokrasia kutoka takribani nchi 80 mbalimbali duniani; Ulaya, Afrika, Amerika na Asia, ikiwepo vyama kadhaa vinavyotawala duniani.

Ni Makamu Mwenyekiti wa IDU na mjumbe wa K**ati yake Kuu ya Kitaifa.

21/08/2026

ANAENDELEA TUNDU LISSU

Na ndiyo tarehe muhimu, waheshimiwa majaji. Tutairudia tena baadaye.

Kabla ya hapo, nilikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMA, takribani kuanzia Julai 2004 nilipojiunga na chama hadi karibu Novemba 2011.

Na nafasi hiyo ilinifanya vilevile kuwa mjumbe wa K**ati Kuu ya chama asiye na kura.

Kwa ushahidi huu, nimekuwa katika uongozi wa CHADEMA katika ngazi ya juu kabisa kwa takribani miaka 20.

Nje ya uongozi wa chama, nimeshikilia nafasi nyingine za uongozi, k**a ifuatavyo:

Mwaka 2010, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010, nilichaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri, nikiiwakilisha Jimbo la Singida Mashariki, siku hizi linafahamika k**a Ikungi Mashariki.

Na nilichaguliwa kwa tiketi ya CHADEMA.

Nilirejea kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

21/08/2026

MAHAKAMA IMEREJEA TUNDU LISSU ANAENDELEA KUPELEKA MOTO.

Waheshimiwa Majaji,

K**a ambavyo nimesema, mimi ni kiongozi wa chama cha siasa kilichoandikishwa rasmi kwa mujibu wa sheria.

Nafasi yangu ya sasa na nafasi niliyokuwa nayo wakati haya yanatokea ni nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Nimekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA tangu tarehe 22 Januari 2025. Kwa maneno mengine, nimekaa kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chama kwa takribani wiki tano au sita, ndipo nikak**atwa na kushtakiwa kwa kosa hili.

Na hilo nitaonyesha maana yake nini baadaye. Kwa sasa, rekodi ni hivyo hivyo.

Waheshimiwa Majaji, kabla sijachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, nilishikilia nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia Desemba 2019 mpaka Januari 22, 2025, nilipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Kabla ya hapo nilikuwa Mwanasheria wa CHADEMA na mjumbe wa K**ati Kuu ya Chama, kati ya mwaka 2010 hadi 2017, specifically hadi tarehe 7 Septemba 2017.

Share zaidi Update hizi WATU WASOME.

21/08/2026

MASHAIDI WA TUNDU LISSU WANAPANDA KIZIMBANI LEO.

Jaji Ndunguru:

Tumesikiliza pande zote mbili.

Na upande wa Serikali wanasema hawana pingamizi kwa mashahidi wa 8 hadi 11. Kwa sababu hawa John Heche, John Mnyika na Brenda Rupia, kwa kuwa hawana pingamizi, waendelee na ushahidi.

Wakati tunaendelea kufanyia kazi uamuzi kuhusu hao mashahidi 7 wengine, Mahak**a ipewe muda itaamua.

Lissu: Mheshimiwa Jaji, niliomba ruhusa ya kushauriana na mashahidi na mawakili.

Kimsingi, Mheshimiwa Jaji, siyo mazungumzo marefu, lakini Mahak**a ijue sijazungumza nao tangu mwaka jana Novemba. Nizungumze nao, halafu tuendelee.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka kuna lolote la kusema?

Wakili wa Serikali: Hakuna pingamizi.

Lakini tunaomba Mahak**a iahirishwe hadi Jumatatu ili kumpa muda wa kujiandaa.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, mimi nipo sensitive sana na maombi ya kuahirisha-ahirisha sana.

Mimi nina mwaka mmoja na nusu gerezani.

Naunga mkono pendekezo la health break, lakini k**a mtaridhia, Waheshimiwa Majaji, naomba tuanze. K**a nilivyosema, mimi nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Kimsingi, hata sisi tunaona twende health break, halafu turudi kuendelea.

Muda wa health break ndiyo utaongea na mawakili wako na mashahidi wako bila kuathiri mambo ya kiusalama.

Mahak**a imeahirishwa.

21/08/2026

WAWILI WA SERIKALI ANAENDELEA

Hoja ya kwamba hawakuandikwa anajua utaratibu wake. Hoja ya kwamba aliwataja, hawakuandikwa, ni hoja ya afterthought baada ya sisi kusema yeye hakusema kabla.

K**a wewe ni mjuvi wa sheria, baada ya kuseviwa ukitakiwa kuanza kujiuliza, je, nilivyowataja vimeandikwa?

Kwa hiyo hoja ilipaswa ifanyiwe kazi kabla ya kusikilizwa, na siyo issue ya kutia huruma.

Rekodi za Mahak**a ndizo zinasema mashahidi hawa hawakutajwa.

Mheshimiwa, kutaja mashahidi wakati wa PH siyo takwa la kifungu cha 281.

Lakini pia siyo takwa la kifungu cha 198.

It has been a practice.

Kwa kuwa yeye hakutaja, sisi hatuku-pre-empty tukasema tuone je, ata-comply kifungu cha 281.

Kwamba kwa sababu aliwataja katika PH na nyie mkaandika, basi ndiyo atawaita.

Maneno ya kwamba msikane uamuzi wenu.

Tumepitia maamuzi yenu, hakuna order yoyote kwamba amewataja mashahidi.

Hapakuwa na order juu ya mashahidi.

Hapakuwa na comment ya upande wa mash*taka kuhusu mashahidi.

Ndiyo maana nasema mnatishwa.

Sheria zipo tu.

Mlikuwa wabunge mkashindwa kurekebisha.

LISSU: “Waheshimiwa Majaji...”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa, naomba kuifuta hiyo, imenitoka tu. Hata nyie nina imani hamjasikia. Naomba kuendelea.

“Kwamba suala la Serikali kutishika au kutotishika ni immaterial.

“Ndiyo maana tukaenda mbali kwamba anasema kusudia kuwa cross dhidi ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri.

“Sisi hatujatishia Mahak**a, bali tumeona Mahak**a itumie mamlaka yake kuona hawa mashahidi siyo wa muhimu.

“Suala la kutishika au kutokutishika ni immaterial.

“Mahak**a iangalie umuhimu wa ushahidi.

“Na uzuri, Mshtakiwa amefunguka, ameeleza anachotaka kuitia ni nini.

“Tukaenda mbali, tukataja vifungu vya Katiba.

“Yale maneno ‘kwa niaba ya Rais’, sijui kwanini hayatafsiriwi sawasawa.

“Kwa tafsiri rahisi, k**a yule alifanya kwa niaba ya Rais, ni wazi kwamba kile alichofanya alifanya kwa niaba ya Rais.

“Kwa sababu yule ni mfanyakazi wake.

“Sijui kwa nini anasema anataka kunyongwa, adhabu zipo nyingi, ikiwemo conditional discharge. Sijui kwanini hazitajwi.

“Mashahidi wakiitwa, ndiyo tunasema hawawezi kuitwa kuwa examined kutoka upande mwingine baada ya subordinates wao kutoa ushahidi.

“Wao walishasema kwamba palikuwa na kuvunja amani.”

Lissu: “Hilo, Waheshimiwa Majaji, naomba kulijibu kwa sababu hilo ni kosa tofauti na ninalosh*takiwa la kutishia amani.”

Nassoro Katuga: “Sijasema umevunja amani. Nimesema narejea, k**a mashahidi waliopita wameongea hivyo, huwezi kuwaita mabosi wao ukawauliza tena kutoka upande wako.

“Waheshimiwa Majaji, hoja ya hawa mashahidi 7 kwamba wakipewa summons hawatokuja, sisi tulijikita kwa Mheshimiwa Rais pekee.

“Wengine wakiitwa wakikataa, itatoka arrest warrant.

“Sasa sisi tunasema Mahak**a lazima itoe summons inayotekelezeka.

“Na Mshtakiwa amesema kwamba Rais asipokuja, Mahak**a haiwezi kutoa arrest warrant. Sasa hiyo summons ya nini, au just for cosmetics tu?

“Waheshimiwa Majaji, nimeshawishiwa ku-issue summons kwa Rais nikirejeshwa kwenye Kesi ya Mahalu.

“Lakini Marehemu Mkapa alikuwa mstaafu wakati anaenda kutoa ushahidi, tofauti kumfananisha na Rais wa sasa ambaye yupo madarakani.

“Ni mazingira ambayo ni tofauti.

“Lakini ni utashindwa, Mheshimiwa Rais mwenyewe.

“Lakini hatuelezwi kwamba Mahak**a iliangalia materiality ya ushahidi wake?

“Kila kesi itaamuliwa kwa mazingira yake.

“Hata sisi tunasema hawa Makamu wa Rais mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu, tunaangalia dhumuni lake na umuhimu wa ushauri wake.

“Ingekuwa vifungu vilivyotumika dhidi ya Serikali vingekuwa the same, basi.

“Waheshimiwa, kwa upande wangu naona niishie hapa.”

Wakili wa Serikali Mkuu, Mwinuka: “Nilitoa ufafanuzi kuhusiana na sheria ya Masuala ya Rais, Sura ya 9. Mshtakiwa anasema kifungu cha 9 na 10 vinapaswa kusomwa kwa pamoja.”

21/08/2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUPELEKA MOTO MAHAKAMANI

Hoja ya kwamba hawakuandikwa anajua utaratibu wake. Hoja ya kwamba aliwataja, hawakuandikwa, ni hoja ya afterthought baada ya sisi kusema yeye hakusema kabla.

K**a wewe ni mjuvi wa sheria, baada ya kuseviwa ukitakiwa kuanza kujiuliza, je, nilivyowataja vimeandikwa?

Kwa hiyo hoja ilipaswa ifanyiwe kazi kabla ya kusikilizwa, na siyo issue ya kutia huruma.

Rekodi za Mahak**a ndizo zinasema mashahidi hawa hawakutajwa.

Mheshimiwa, kutaja mashahidi wakati wa PH siyo takwa la kifungu cha 281.

Lakini pia siyo takwa la kifungu cha 198.

It has been a practice.

Kwa kuwa yeye hakutaja, sisi hatuku-pre-empty tukasema tuone je, ata-comply kifungu cha 281.

Kwamba kwa sababu aliwataja katika PH na nyie mkaandika, basi ndiyo atawaita.

Maneno ya kwamba msikane uamuzi wenu.

Tumepitia maamuzi yenu, hakuna order yoyote kwamba amewataja mashahidi.

Hapakuwa na order juu ya mashahidi.

Hapakuwa na comment ya upande wa mash*taka kuhusu mashahidi.

Ndiyo maana nasema mnatishwa.

Sheria zipo tu.

Mlikuwa wabunge mkashindwa kurekebisha.

LISSU: “Waheshimiwa Majaji...”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa, naomba kuifuta hiyo, imenitoka tu. Hata nyie nina imani hamjasikia. Naomba kuendelea.

“Kwamba suala la Serikali kutishika au kutotishika ni immaterial.

“Ndiyo maana tukaenda mbali kwamba anasema kusudia kuwa cross dhidi ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri.

“Sisi hatujatishia Mahak**a, bali tumeona Mahak**a itumie mamlaka yake kuona hawa mashahidi siyo wa muhimu.

“Suala la kutishika au kutokutishika ni immaterial.

“Mahak**a iangalie umuhimu wa ushahidi.

“Na uzuri, Mshtakiwa amefunguka, ameeleza anachotaka kuitia ni nini.

“Tukaenda mbali, tukataja vifungu vya Katiba.

“Yale maneno ‘kwa niaba ya Rais’, sijui kwanini hayatafsiriwi sawasawa.

“Kwa tafsiri rahisi, k**a yule alifanya kwa niaba ya Rais, ni wazi kwamba kile alichofanya alifanya kwa niaba ya Rais.

“Kwa sababu yule ni mfanyakazi wake.

“Sijui kwa nini anasema anataka kunyongwa, adhabu zipo nyingi, ikiwemo conditional discharge. Sijui kwanini hazitajwi.

“Mashahidi wakiitwa, ndiyo tunasema hawawezi kuitwa kuwa examined kutoka upande mwingine baada ya subordinates wao kutoa ushahidi.

“Wao walishasema kwamba palikuwa na kuvunja amani.”

Lissu: “Hilo, Waheshimiwa Majaji, naomba kulijibu kwa sababu hilo ni kosa tofauti na ninalosh*takiwa la kutishia amani.”

Nassoro Katuga: “Sijasema umevunja amani. Nimesema narejea, k**a mashahidi waliopita wameongea hivyo, huwezi kuwaita mabosi wao ukawauliza tena kutoka upande wako.

“Waheshimiwa Majaji, hoja ya hawa mashahidi 7 kwamba wakipewa summons hawatokuja, sisi tulijikita kwa Mheshimiwa Rais pekee.

“Wengine wakiitwa wakikataa, itatoka arrest warrant.

“Sasa sisi tunasema Mahak**a lazima itoe summons inayotekelezeka.

“Na Mshtakiwa amesema kwamba Rais asipokuja, Mahak**a haiwezi kutoa arrest warrant. Sasa hiyo summons ya nini, au just for cosmetics tu?

“Waheshimiwa Majaji, nimeshawishiwa ku-issue summons kwa Rais nikirejeshwa kwenye Kesi ya Mahalu.

“Lakini Marehemu Mkapa alikuwa mstaafu wakati anaenda kutoa ushahidi, tofauti kumfananisha na Rais wa sasa ambaye yupo madarakani.

“Ni mazingira ambayo ni tofauti.

“Lakini ni utashindwa, Mheshimiwa Rais mwenyewe.

“Lakini hatuelezwi kwamba Mahak**a iliangalia materiality ya ushahidi wake?

“Kila kesi itaamuliwa kwa mazingira yake.

“Hata sisi tunasema hawa Makamu wa Rais mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu, tunaangalia dhumuni lake na umuhimu wa ushauri wake.

“Ingekuwa vifungu vilivyotumika dhidi ya Serikali vingekuwa the same, basi.

“Waheshimiwa, kwa upande wangu naona niishie hapa.”

Wakili wa Serikali Mkuu, Mwinuka: “Nilitoa ufafanuzi kuhusiana na sheria ya Masuala ya Rais, Sura ya 9. Mshtakiwa anasema kifungu cha 9 na 10 vinapaswa kusomwa kwa pamoja.”

21/08/2026

TUENDELEE

Mahak**a ipo kimya. Majaji wanateta.

Jaji Ndunguru: “Tuendelee.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, tuanze na kauli ya mwisho ambayo Mshtakiwa amemalizia, kwamba msitoe uamuzi kwa kuogopa hawa waendesha mashtaka. Maneno haya yamesemwa ili kuitisha Mahak**a, ili isitoe uamuzi sahihi.

“Tusiende sana huko, ila Mahak**a itaangalia k**a anaweza kuitisha Mahak**a, anaweza pia kuitisha Serikali.

“Waheshimiwa, vifungu vya sheria vipo, not for cosmetics. Tumeialika Mahak**a katika vifungu, siyo katika vitisho. Mahak**a haipaswi kuacha kutumia vifungu vya sheria ili kumfurahisha mtu.

“Sisi tunasema mashahidi hawakutajwa Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kumbukumbu zipo na ndizo zinatumika. Na kumbukumbu ambazo Mshtakiwa alipewa.

“Mshtakiwa akisema leo alisema haikuandikwa, haisaidii. Kusema kwamba nikisema na haipo katika kumbukumbu za Mahak**a ni kutaka kutia huruma, na huruma siyo malezi.”

MAHAKAMA INAGUNA.

Jaji Ndunguru: “Naomba tutulie.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa, vifungu hivi vingekuwa siyo upande wa Jamhuri, ingekuwa vitamu. Nimevitaja vifungu hapa, Mshtakiwa hajavitaja vifungu wala kuvipinga.”

Lissu anasimama.

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, reference yoyote aliyosema kuwa natisha Mahak**a na kwamba naomba huruma, viondolewe. K**a hakuna sehemu nimesema natishia Majaji au kutaja maneno ‘huruma’, viondolewe. K**a vitabaki, nitaomba kujibu.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, natoa tafsiri k**a alivyokuwa anatoa tafsiri. Yeye kasema kwamba msitoe uamuzi kwa kuogopa mawakili wa Serikali. Kwa maneno haya, nafasiri kwamba anatishia Mahak**a.”

WATU WANAZOMEA.

Jaji Ndunguru: “Naombeni tutulie. Hata k**a Wakili anasema usicholipenda, vumilia. Tukikupoint, tutakuchukulia hatua. Naomba tuendelee.”

Nassoro Katuga: “Asante, Waheshimiwa Majaji.

“Mimi nimetoa kifungu na kueleza kwamba hao mashahidi hawapo katika kumbukumbu za Mahak**a. Hoja ya kwamba alisema hawakuandikwa, yeye anajua utaratibu wake.

“Mshtakiwa anajiwakikisha kwa sababu ni mjuvi wa sheria.”

21/08/2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA ANAPIGA SANA LEO.

Wakili Nassoro Katuga kasimama anasema kwamba Lissu anafanya rejoinder na analeta vitu vipya.

Mahak**a inacheka.

Lissu: Mheshimiwa Jaji, mimi na-reply objection yake baada ya mimi kutaja mashahidi.

Jaji Ndunguru: Tuwa wasikivu, hata k**a jambo hulipendi. Tuendelee.

Lissu: Mheshimiwa Jaji, kwa sheria za Tanzania hakuna utaratibu wa mtu kutoa ushahidi kwa niaba ya mtu mwingine.

Hakuna utaratibu wa Rais kutolewa ushahidi na mtu mwingine.

Ndiyo maana kifungu cha 9 na 10 cha Sheria ya Masuala ya Rais kinasema hiyo summons utapeleka kwa wasaidizi wake.

Ingekuwa Rais anatoa ushahidi na mtu mwingine, sheria ingesema hivyo, siyo?

Kwa hiyo, ushahidi wa kina Mahamba ni ushahidi wao, wala siyo kwa niaba ya mtu mwingine.

K**a Rais anaona kuna irrelevance, muache aseme yeye, atoe ushahidi yeye, wala siyo wewe from the bar.

Waheshimiwa Majaji, kesi ya Jacob, ambayo k**a nimewasikia sawasawa, Wakili Job Mrema amesema Hakimu anayo mamlaka ya kukataa kuita shahidi pale ambapo shahidi hana uhusiano na kesi iliyopo Mahak**ani, ili mradi Hakimu aandike sababu za kumkataa shahidi.

Waheshimiwa Majaji, hii kesi ina uhusiano gani na Mahak**a hii?

Hii kesi ya Mahakimu ina uhusiano gani na Majaji kujifunza kwa Mahakimu?

Pia inasema k**a ushahidi hauna uhusiano na kesi.

Je, katika kesi kubwa kuliko zote, kesi ya uhaini, kesi inayohusu Baraza la Usalama haina uhusiano?

Je, kesi ya Serikali inayodaiwa kutishiwa haina uhusiano na Baraza la Usalama?

Je, Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Majeshi na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, hawa wote wajumbe wa Sekretarieti, kwamba haina uhusiano na uhaini?

Hata k**a kesi ya Jacob ipo sahihi, lakini katika kesi hii haipo sahihi.

Kwa sababu niliowataja wana uhusiano wa moja kwa moja.

Mheshimiwa Jaji, nimalizie kuwa:

Hakuna sheria inayozuia mashahidi niliowataja wasipelekwe summons.

Akikataa, ni swala jingine.

Na wengine wote hao wanaweza kupelekewa summons.

Pili, Waheshimiwa Majaji, ushahidi wao ni muhimu sana.

K**a kweli kulikuwa na matishio kwa Serikali yanayodaiwa, waseme.

Tatu, Waheshimiwa Majaji, nawaombeni msimamie kauli zenu.

Mlisema niwatajie majina ya mashahidi ninaotaka kuwaita, nikawataja na mkawarekodi.

Imefika wakati wa kutekeleza mlichokirekodi, na wakati ni sasa.

Ni sasa hivi.

Ni watu wakubwa sana, ndiyo.

Lakini hizo nafasi zinazowapa ukubwa ndizo zinahitajika kuja kueleza ukweli.

Kwenye sheria za nchi hii, watuhumiwa wa makosa ya jinai wana haki ya kutendewa FAIR TRIAL.

Wana haki ya kuwezeshwa na Mahak**a mashahidi kuitwa.

K**a hamuwezi kuwaita mashahidi kwa hofu za waendesha mashtaka wa Serikali, basi hakutakuwa na FAIR TRIAL.

K**a hakutakuwa na FAIR TRIAL, ni Mungu tu ndiye anajua Mahak**a itaonekanaje kwa kuzuia mashahidi.

Lindeni haki za msh*takiwa, lindeni hadhi ya Mahak**a na lindeni FAIR TRIAL.

NIMEMALIZA...

Mahak**a ipo kimya kidogo.

Majaji wanaendelea kuandika.

TAFADHARI NAOMBA KILA MTU ASHARE UPDATE HIZI KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.

NA MAGROUP YOTE YA WHATSSAP.

Address

Belfast

Telephone

+255788189018

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Emmanuel Otto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Emmanuel Otto:

Shortcuts

Share