09/10/2025                                                                            
                                    
                                                                            
                                            Romuald Rakotondrabe Kocha Mpya wa Yanga, Yanga SC Yamteua Romuald Rakotondrabe Kuwa Kocha Mpya | Achukua Mikoba ya Romain Folz.
Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumteua Romuald Rakotondrabe, kocha wa Timu ya Taifa ya Madagascar, kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Romain Folz raia wa Ufaransa.
Romuald Rakotondrabe Kocha Mpya wa Yanga
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika, Rakotondrabe, mwenye umri wa miaka 60, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili na kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha huyo ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, hasa kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa na Barea, timu ya taifa ya Madagascar, ambayo aliiongoza kufuzu hatua muhimu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Uwezo wake wa kujenga timu zenye nidhamu na kucheza soka la ushindani umekuwa sababu kuu ya kuvutia uongozi wa Yanga SC.
Romuald Rakotondrabe Kocha Mpya wa Yanga
Romuald Rakotondrabe Kocha Mpya wa Yanga
Wakati huo huo, Romain Folz (35) anatarajiwa kuvunjiwa rasmi mkataba wake na klabu hiyo, hatua itakayofunga ukurasa wake wa muda mfupi ndani ya Yanga SC. Folz, ambaye aliwahi kufundisha klabu kadhaa barani Afrika ikiwemo AmaZulu FC na Azam FC, ameshindwa kufikia matarajio ya mashabiki na uongozi wa klabu hiyo kongwe ya Jangwani.
Uongozi wa Yanga SC una matumaini kuwa ujio wa Rakotondrabe utaleta mwelekeo mpya na kuongeza nguvu ya ushindani wa timu katika mashindano ya ndani na kimataifa, hususan katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na NBC Premier League.