Sports kitaa

Sports kitaa Sportskitaa.com: Football News, Live Scores, Results and Transfers

Sportskitaa.com is a purely up-to-date sports and entertainment website.
The East African based website, is professionally run by a seasoned East African sports fans and proudly using Swahili language.

23/05/2025

PARIS vs MILAN ⚽🎉

Ni vita ya mabingwa, mechi kubwa, Timu kali.💥🏆

Furahia Ch. 222 ndani ya kifurushi cha COMPACT, kuanzia tarehe 15 Mei hadi 10 Juni. Hivyo fainali za unaziangalia kiulaini😍📺 📣

Piga *150*53 # kulipia mapema ili usipitwe.

⚽🏆🔥💥
🔌⚡️

SIMBA SC Yajibu mapigo baada yakuambiwa WALIPE MILLIONI 256/ Hiki ndicho walichoandika
04/01/2025

SIMBA SC Yajibu mapigo baada yakuambiwa WALIPE MILLIONI 256/ Hiki ndicho walichoandika

DIAMOND Achukizwa Na Shabiki Aliyemuita P-DIDY Aongea kwa Uchungu mbele ya MASHABIKI/ nimefanikiwa
04/01/2025

DIAMOND Achukizwa Na Shabiki Aliyemuita P-DIDY Aongea kwa Uchungu mbele ya MASHABIKI/ nimefanikiwa

04/01/2025

🗣️Zinchenko: "Siku moja, Pep alikosoa pasi yangu katika mazoezi. Nikasema: ‘Mr Nilikosa pasi moja tu, unajua?’ Na itikio lake lilikuwa la ajabu. "Oh, sawa, samahani, samahani, Bwana Zinchenko. Pole. Sawa, asante, kila mtu hapa ndani (mazoezini).’
"Mazoezi yalisitishwa kwa sababu nilimjibu. Nilijua niko kwenye matatizo.”
Zinchenko aliwekwa benchi katika mechi yake iliyofuata.
Follow Gazeti la Championi

04/01/2025

Emmanuel Okwi ametimiza miaka 32 juzi kwenye Krismasi.
Ukifanya rejea ndogo utaona Okwi alianza kucheza Ligi Kuu akiwa na miaka 16 na aliingia Bongo akiwa na miaka 17 pekee kucheza Simba SC!
Huenda ni kipaji cha ajabu miaka 16 uwe ligi Kuu! Maana yake hakupoteza sana muda kujisaka mtaani na kwa Sasa akiwa na miaka 32 huenda ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza ligi Kuu barani Afrika!
Baadhi ya timu alizopita ni pamoja na
2008–2009 SC Villa
2009–2013 Simba SC
2013 Étoile du Sahel
2013 SC Villa
2013–2014 Yanga SC
2014–2015 Simba
2015–2017 SønderjyskE
2017 SC Villa
2017–2019Simba SC
2019–2021 Al Ittihad
2021–2022 Kiyovu Sports
2022–2023 Al-Zawra’a
2023–2024 Erbil SC
2024– Kiyovu Sports
Sijui tunaelewana!? Kuna mchezaji mnaymkumbuka Afrika kacheza ligi Kuu akiwa na miaka 16!?

04/01/2025

BONDIA wa ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo amerusha jiwe kwa wadau wa ngumi kwa kusema kuwa kila anaposimamia maslahi makubwa kwa mabondia wanaonekana kunguru waoga kutaka hela nyingi.
-
Wakati huo huo, ametoa pole kwa familia ya bondia aliyepoteza maisha hivi karibuni akiwa ulingoni Hassan Mgaya akisema ni mara ya tatu wanazika watu kwa vifo vya aina hiyo.
-
Mwakinyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram, amesema “Leo kiasi cha malipo ya sh 60,000 ndio kimekatisha safari ya ndugu yetu…. na wengine wana pigania mpaka magari yaliyotumika. Huu ni ujinga tunapaswa kuwa mifano kwa maslahi ya wengi,”
“Binafsi mimi nasimama na promota wa hilo pambano ya kuwa yeye hana makosa amelipa mabondia kulingana na uwezo wake, wengi wakubwa hawathamini mabondia wadogo,”
-
Ametoa rai na kusema serikali ingetoa macho kupitia ngumi kuhakikisha kunapatikana wadhamini hata kwa mapambano madogo ya mitaani ili mabondia wadogo wanufaike.
“Hili liwe fundisho kwa mabondia wengine na sasa waachane na ngumi za mkali nani, ukifa haufi na unaowafurahisha unakufa peke yako,”alisema.
-
Mgaya alipoteza maisha Desemba 29 mwaka jana katika Hospitali ya Mwananyamala kufuatia kupigwa kwa TKO na mpinzani wake Paulo Elias katika pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Dunia ndogo uliopo Tandale kwa mtogole.
-
Imeandaliwa na Grace Mkojera

04/01/2025

“Hatuna wasiwasi…! Tutamfunga Yanga hapa hapa na mashabiki waje wakiwa wengi…! Tuna uwezo huo na huu ni mchezo mwingine ambao hatuhitaji kupoteza…! Tulisare nyumbani na hatukuwa na furaha…! Tutashinda hapa hapa Dar Es Salaam,” Lamine N’diaye, Kocha wa TP Mazembe kuelekea mchezo vs Yanga SC.
Ripota:

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sports kitaa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sports kitaa:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share