07/01/2026
𝐀𝐘𝐀𝐍𝐀 𝟕𝐓𝐇 𝐉𝐀𝐍 𝟐𝟎𝟐𝟔 𝐖𝐑𝐈𝐓𝐓𝐄𝐍 𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒
𝐅𝐈𝐑𝐒𝐓 𝐄𝐏𝐈𝐒𝐎𝐃𝐄
Ni mwendo wa saa mbili na nusu usiku nyumbani kwa Tyrone. Saida anahisi Asha hayuko sawa, na kweli Asha ana msongo wa mawazo kwa sababu hataki mambo ya Ray. Asha analazimishwa kuwa karibu na Ray ili Ray awasaidie kupata pesa za wakili; na si kwamba Ray ni tajiri fulani, la hasha, yeye ni mwizi tu k**a mpenzi wako, lakini kwa sababu anataka kukufurahisha, ndiyo maana anaiba.
Ray na Jemimah wamefika mahali kazi ilipo, na ungejiuliza sana ni mpango gani wanaoendesha, lakini usijali, nawaeleza sasa hivi. Hivi ndivyo mambo yanavyokwenda:
Jemimah na Ray waingie kwenye baa, kisha wajifanye ni wapenzi. Walipoingia, kumbe lengo lao liko huko—kuna mwanamume mmoja tajiri ambaye anapenda sana wanawake. Mpango ni Ray ajifanye Jemimah ni mpenzi wake lakini Jemimah amkatae ili huyu tajiri aone fursa ya kumnyakua 🤣🤣.
Na kweli, wakaona yule mzee anawatazama sana hadi Ray akamwambia Jemimah, "Wallahi wewe ni mrembo sana," kisha akasema anataka kwenda nje kidogo ili mzee huyo aje kumtongoza Jemimah.
Hapo hapo! Ray alipotoka tu, kana kwamba ilikuwa imepangwa, mzee huyo akaja na divai pale Jemimah alipoketi na kumuuliza, "Mrembo k**a wewe mbona unakaa na vijana wadogo wakati mimi niko hapa? Kwa majina naitwa Paul." Wakaanza kupiga gumzo, na hapa ndipo mpango ulipoanza... Ray akarudi na kumuuliza Paul, "Unafanya nini na mpenzi wangu?" Paul akasema, "Kijana tulia, tunazungumza tu." Ray akakasirika na kusema hata halipi bili hiyo kisha akaondoka. Paul akamwambia Jemimah, "Tulia mrembo, mimi nitagharamia kila kitu" 🤣🤣🤣.
Paul akidhani amepata bahati, hajui tayari ameshanaswa.
Ilimchukua Jemimah dakika ishirini tu akawa ameshamuibia Paul pesa kiasi cha shilingi laki moja na hamsini elfu, kisha akatoka nje ya baa, akakutana na Ray na wakaenda zao. Ilikuwa ni mbinu iliyopangwa vyema.
Muda ulienda hadi saa saba ya usiku na ndipo Jemimah anarudi kwake. Kumbuka alitoka kwa siri bila Chris kujua 🤣🤣 lakini siku za mwizi ni arobaini. Kumbe Chris aliamka, akagundua mke wake hayupo, akaketi kitandani kumngoja 🤣🤣.
Jemimah kufika tu, akakutana na Chris mbele yake! Chris akamuuliza, "Umetoka wapi saa hizi?" Jemimah akadanganya, "Nimetoka nje kutembea kidogo." Chris akamwambia, "Usinifanye mjinga, unataka kunidhalilisha, sivyo?" Chris alikuwa amekasirika sana, karibu ampige Jemimah, k**a si mtoto wao kusikia kelele na kuja, Jemimah angekiona cha mtema kuni 🤣🤣.
𝐒𝐄𝐂𝐎𝐍𝐃 𝐄𝐏𝐈𝐒𝐎𝐃𝐄
Becka naye alikuja kumuuliza Sabina hali ya Tinah, lakini Sabina akamwambia, "Usinifanye mjinga, najua unashirikiana na Saida." Becka akajitetea, "Hapana mama, mimi nakuheshimu tu, sishirikiani na Saida hata kidogo."
Sabina akamwambia Becka, "Sikiliza, aliyekukubalia uishi hapa yuko gerezani, huyo ni Tyrone. Aliyekuleta hapa yuko chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), huyo ni Celestine. Hivyo basi, mambo ni mawili: uende gerezani kwa Tyrone au uende ICU kwa Celestine. Hapa kwangu nakupa dakika tano tu uwe umeondoka." Maskini Bakari! 🤣🤣
Chris naye alikuwa hajui yanayojiri hospitalini. Alipofika huko, akamkuta Robert na kumwambia, "Tafadhali ndugu yangu, nataka kuongea na Tyrone anikopeshe pesa kidogo, mambo si mazuri huku." Robert akamjibu, "Tyrone yuko gerezani kwa kumpiga risasi Tinah, hivyo hutapata msaada."
Chris alishangaa sana; alifika na kumwona Tinah akiwa katika hali ya kupoteza fahamu (coma), lakini kabla hajakaa sana, Sabina akafika akiwa na hasira kali. Akamfukuza Chris na kumwambia Robert asiwahi kumruhusu huyu mtu kumkaribia mtoto wake.
Kumbe Ray naye, katika zile pesa walizomuibia yule mzee, alipewa laki moja. Mapema asubuhi, Ray alienda kwa Saida, akampa pesa hizo na kumwambia ni laki moja. Lakini kosa walilofanya au jambo wasilolijua ni kwamba Flora, yule mfanyakazi wa ndani, ni mja wa Sabina. Hivyo kila kitu walichozungumza na pesa alizopewa Saida, Flora alisikia na kuona. Kosa kubwa sana! 🤣🤣 Saida aligundua Flora anawachungulia, akamwambia, "Ole wako mtu asikie jambo hili, utaona cha moto."
Robert, baada ya kusikia Chris amefilisika, alimpigia simu Jemimah na kumuuliza, "Shida iko wapi? Nasikia Chris amekwama sana." Jemimah akamwambia, "Ndiyo, yuko kwenye matatizo kidogo, alinaswa na sakata la utapeli." Robert akamwambia, "Basi ondoka hapo, wewe na Ivy." Jemimah akamjibu, "Mimi si k**a wewe ambaye naweza kuwaacha watu ninaowapenda." Robert akamuuliza, "Hivyo unajaribu kusema nini?" Jemimah hakumficha, akamwambia, "Mimi si msaliti k**a wewe ambaye unaweza kuwageuka marafiki zako. K**a unataka kumsaidia Chris msaidie, k**a sivyo, usijiingize kwenye mambo ya familia yangu." Lo! Hali ni mbaya...
Saida na Annaliz wanajitahidi kutafuta wakili atakayekwenda kumtoa Tyrone gerezani.
Huku nje, Ray alikuja kumuomba Asha msamaha kwa jinsi alivyomtendea vibaya, lakini Asha akamwambia, "Usijali, nilishakusamehe tayari, usikuwe na wasiwasi." Ray anashangaa imekuwaje amesamehewa haraka hivyo 🤣🤣 hajui kuwa ni mchezo tu Asha anacheza kwa sababu wanahitaji msaada wake. Maskini Ray! 🤣🤣
Mwisho tufollow The Two Cast for daily updates