12/09/2026
MASOMO YA MISA, DOMINIKA YA ISHIRINI NA NNE KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA A, SEPTEMBA 13, 2026
RANGI YA KILITURJIA: KIJANI KIBICHI 💚
SOMO LA KWANZA
YOSHUA BIN SIRA 27: 30—28:1—7
"Msamehe jirani yako kosa lake, na hapo uombapo dhambi zako zitafunguliwa"
Somo katika kitabu cha Yoshua bin Sira
Hasira na ghadhabu, hayo pia ni chukuzo, na mtu mwenye dhambi atashikwa nayo. Mwenye kulipiza kisasi ataona kisasi kutoka kwa Bwana, naye hakika atazishika dhambi zake. Msamehe jirani yako kosa lake; na hapo uombapo dhambi zako zitafunguliwa. wakati utakaposali. Mwanadamu anamtunzia hasira mwanadamu naye atatafuta kuponywa na Bwana? Hana rehema kwa mwanadamu aliye sawa naye, naye anaomba kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe? Mwenyewe ni nyama tu, naye hushika hasira; Nani atamsamehe dhambi zake? Kumbuka siku za mwisho na uiache chuki; kumbuka uozo na mauti na udumu katika amri! Kumbuka amri na usimkasirikie jirani; Kumbuka agano la Aliye juu na usijali ujinga.
NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU
ZABURI YA KUITIKIZANA
ZABURI 103:1—2, 3—4, 9—10, 11—12 (K. 😎
K. Bwana ni mwenye huruma na neema, ni mwingi wa fadhili.
Umsifu Bwana ee nafsi yangu;
Na yote yaliyo ndani yangu,
yalisifu jina lake takatifu!
Umsifu Bwana ee nafsi yangu;
Wala usizisahau fadhili zake zote. K.
Yeye anasamehe dhambi zako zote,
Anaponya magonjwa yako yote,
Yeye anaukomboa uhai wako na kaburi,
Anakuvika taji la fadhili na rehema. K.
Mungu haendelei daima kukaripia,
Wala hadimishi hasira yake milele,
Hatutendi kadiri ya dhambi zetu,
Wala hatulipi kadiri ya makosa yetu. K.
Maana k**a vile mbingu zinavyoinuka juu ya nchi,
Ndivyo wema wake ulivyo mkuu kwa wamchao.
K**a mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. K.
SOMO LA PILI
WARUMI 14:7—9
"Ikiwa tunaishi au tunakufa, sisi ni mali ya Bwana"
Somo katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi
Ndugu zangu: Hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe. Tukiishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana; Tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, ikiwa tunaishi au tunakufa, sisi ni mali ya Bwana. Kwa maana Kristo alikufa, akafufuka ili awatawale wafu na wazima.
NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU
SHANGILIO LA INJILI
YOHANE 13:34
K. Aleluya. W. Aleluya.
Amri mpya nawapeni, asema Bwana. K**a mimi nilivyowapenda, nanyi pia mpendane.
W. Aleluya.
SOMO LA INJILI
MATHAYO 18:21—35
"Sikuambii hata mara saba bali hata saba mara sabini."
† Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Mathayo
Wakati ule: Petro alimwendea Yesu akamwuliza, "Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?" Yesu akamwambia, "Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Kwa hiyo ufalme wa mbingu umefanana na mfalme aliyetaka kufanya mahesabu na watumishi wake. Alipoanza kufanya mahesabu, walimletea mtu mwenye deni kubwa. Lakini hakuwa na kitu cha kulipa. Kwa hiyo bwana akaamuru auzwe, yeye pamoja na mke na watoto wake na mali yake yote, ili kulipa deni. Hapo yule mtumishi akamwangukia, akamwomba akisema, 'Bwana, unipe muda, nami nitakulipa yote.' Bwana wa mtumishi yule akamhurumia, akamfungua, akamfutia deni. Mtumishi yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wenzake, aliyemdai dinari mia. Akamk**ata, akamkaba koo akisema, 'Lipa deni lako lote.' Mtumishi mwenzake akamwangukia, akamwomba akisema, 'Unipe muda, nami nitakulipa.' Lakini yule hakutaka, akaenda, akamtupa gerezani mpaka alipe lile deni. Watumishi wenzake walipoona mambo hayo, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, "Ewe mtumishi mbaya, nilikufutia deni lile lote, kwa sababu uliniomba. Je, haikukupasa wewe pia kumsamehe mtumishi mwenzako k**a mimi nilivyokusamehe wewe?' Bwana wake akakasirika, akamweka mikononi mwa watesi mpaka alipe deni lote. Hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatendea ninyi, msipomsamehe kwa moyo kila mmoja ndugu yake.
INJILI YA BWANA... SIFA KWAKO EE KRISTO