Sheshe News

Sheshe News Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Sheshe News, Media/News Company, Eldoret.

06/12/2022
WACHENI KUWADHULUMU WAFANYAKAZI WAKONGWE -EACC YAAMBIA MAGAVANA WATEULE.Tume ya maadili na inayopambana na visa vya ufis...
24/09/2022

WACHENI KUWADHULUMU WAFANYAKAZI WAKONGWE -EACC YAAMBIA MAGAVANA WATEULE.

Tume ya maadili na inayopambana na visa vya ufisadi nchini Kenya almaarufu EACC imewaonya magavana wateule dhidi ya kuwadhulumu wafanyakazi walioajiriwa na serikali iliyotangulia kuwa watachakuliwa hatua ya kisheria.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbaruk amesema kuwa tume hiyo imeshuhudia visa vingi vya dhuluma dhidi ya wafanyakazi hao.
"Visa hivi vimeongezeka kwenye kaunti ambazo magavana wapya wameshika hatamu za uongozi baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti tisa,"alisema Mbaruk.
Alihoji kuwa baadhi ya magavana wateule wameshindwa kufanya kazi na wahudumu hao wakongwe.
"Wakati mwingine wafanyakazi hao hutishiwa kufutwa au hata kulazimishwa kufanya adhabu kinyume na sheria ili kuwang'atua maofisini,"alisema Mbaruk.
Afisa huyo amewasihi magavana wote ambao huchukua sheria mikononi mwao kujisalimisha kwa kufuata sheria za kikatiba katika kudhibiti nidhamu ya wafanyakazi wa serikali.
"Hivyo tume hii inatoa rai Kwa magavana hao kushirikisha washikadau wote na kufuata kanuni zote panapotokea tuhuma za ufisadi dhidi ya wafanyakazi serikalini.

Address

Eldoret

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sheshe News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share