27/07/2025
Kumbukumbu la torati 18:
(Deuteronomy)
2. Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, k**a alivyowaambia.
---------------
Therefore they shall have no inheritance among their brethren; the Lord is their inheritance, as He said to them.
3. Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.
---------------
"And this shall be the priest's due from the people, from those who offer a sacrifice, whether it is bull or sheep: they shall give to the priest the shoulder, the cheeks, and the stomach.
4. Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe.
---------------
The firstfruits of your grain and your new wine and your oil, and the first of the fleece of your sheep, you shall give him.
5. Kwani Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele.
---------------
For the Lord your God has chosen him out of all your tribes to stand to minister in the name of the Lord, him and his sons forever.
6. Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua Bwana;
---------------
"So if a Levite comes from any of your gates, from where he dwells among all Israel, and comes with all the desire of his mind to the place which the Lord chooses,
7. na atumike kwa jina la Bwana, Mungu wake, k**a wafanyavyo ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za Bwana.
---------------
then he may serve in the name of the Lord his God as all his brethren the Levites do, who stand there before the Lord.