31/10/2025
sasa imagine wasee, ni usiku, baridi imevaa attitude 😭
tumetoka matanga ya baba na roomie juu lecturers wamefanya ile kitu, akili bado hazijarudi, Ivy ananiambia,
“mami tusirudi hostel kuboeka tunaneed a good vibe, wacha tuka refresh koo pale South B kidogo.”
niko zile za sawa, juu nani hataki chai ya usiku na ka uji kidogo 😅
tukifika joint, Ivy anaingia k**a boss — heels zinabisha greetings,
macho ya kila mtu zinamfuata.
dem ako 24 lakini ana confidence ya 40-year-old senator 💅🏾 lakini goosebumps don't lie
namuuliza, “si ungepigilia jumper ata kidogo?”
akasema, “mami, mwili ndio stock, siwezi funika goods k**a delivery ya unga” 😂😭
saa zinasonga, music iko loud, vibes zinachemka. Kumbe huku ndio madame hukuja kuteka mabudaa, Ki
ghafla bin vuu, dem mmoja anakorofishana na Ivy juu ya kiti —
kiti bana! si pesa, si drink, kiti! 😭
macho zikaangaza, watu wakahepa polepole
na mimi kwa akili nikaambia Mungu, hii usiku iishe tu peacefully.
lakini wapi 😭
nje ya joint tukiwa tunahepa drama, ndio hao mambanga na mariamu sema teke faster route 11 na hatujui why we're running but you can't wait upewe that mariamu ride juu utatafutiwa makosa mkiendaga 😂
Kiasi kiasi tunameet nduthi guy anatupiga bill ya Ksh 800
eti tumevaa supuu sana kuwa broke 😭💀
Ivy akampigisha smile akidaisha, “bro, kaa ukiona nangara elewa ni hustle, jua ni display.”
wakaanza kucheka na tukaingia topic ya discount hadi river road tuhepe uptown 😂
downtown sasa, tukijaribu kuchukua shortcut,
kwa corner kuna wasee wanabishana, kelele mob, msee mjamo anapasua machupa 💀
Ivy aka-whisper, “mami, hii si route ya story nzuri.”
tukageuka direction ingine,
tukapita kwa mtaro moja ilikua imejaa maji sijui ni sewage ama holy water ya ghetto 😭
sisi hao tukiruka drainage k**a wanariadha,
heels kwa mikono, 😂
Kucheki nyuma — Ivy hako 😳 sema
moyo kudunda.
nikaskia tu kelele, “run! run!” 😭
na vile nilikimbia bana, nilisahau hata nilivaa skirt, si short 😭💀
Kupiga kona moja, nikajipata nimeingia kwa zile vibandaski za 24/7,
jamaa wa hapo akaniuliza “madam unahitaji nini?”
nikasema “safe space.” 😂
After kaa 5 minutes hivi, Ivy anaingia akicheka hadi anashika tumbo 😭
anasema kuna chokosh alikuwa ameokota simu yake tukihepa, saa juu ya kumvuruga bure ilibaki amchunie fifty akamwachia... kumbe simu ilikuwa ndani ya wig yake 💀
kuitisha chai, inakam kitu moto brown huwezi tell kaa ni maji mbaya imechemshwa au juu hakuna stima ni generator Tu 😭 so kuko dim dim
Ivy kuchukua sip moja akasema,
“mami, hii chai mbona inaonja chumvi—
kabla amalize sentensi, generator ikazima 💀 ngataa haina, kila mtu kimya, then from outside tukasikia mtu analia
sisi wote tukashika breath 😳
Ivy kuchungulia kumbe ni ule chokosh wa fifty,
anasema “chai yangu nimeiacha hapa jana.” 😂😭
na hapo wote tukacheka hadi machozi, baridi inatupiga lakini roho iko warm. 🔥
Pahali uko Ivy next time I'm not buying into your bad decisions