01/01/2026
Mwaka uliopita haukuwa rahisi, lakini Mungu alituwezesha kuvuka tukiwa na afya njema. Nilipitia mambo mengi yaliyonifurahisha na yenye changamoto lakini yote yamenijenga na kunifanya kuwa imara zaidi.
Nawashukuru sana marafiki wangu wote kwa kuwa nami na kunipa motisha na matumaini ya maisha. Kwa wote mlioamini kazi zangu katika filamu, uelekezaji wa video, pamoja na matukio kwenye sherehe nilizohusika nazo, asanteni sana kwa kuniamini.
Vilevile, nawathamini sana wote wanaonipa moyo na motisha kila wakati. Shukrani zangu za dhati ziende kwenu. Mungu awabariki na awe nanyi siku zote.
Nawatakia heri njema ya Mwaka Mpya 2026. 🎉✨
Regards Naitaled Edwin -Director NTL MEDIA Creations