21/08/2026
HEHA MOVERS STORY YANGU — NAOMBA MNIOMBELEE 🙏😔
Watu wangu, ngoja niwaambie kilichonipata tangu jana jioni.
Jana nilipatia Heha Movers kazi ya kunihamishia mzigo wangu. Nilifanya hivyo nikiwa na imani kwamba nitapata huduma nzuri na mzigo wangu utafika salama sehemu niliyokuwa nahamia.
Safari ikaendelea na kila kitu kilionekana kiko sawa. Lakini kabla hata hatujafika pale tulipokuwa tunaenda, wakaniambia, “Wewe tangulia, mzigo unafika saa hii.”
Kwa kuwa nilikuwa nimewaamini, sikuona sababu ya kubishana nao. Nikasema sawa, nikatangulia.
Sasa hapo ndipo story inaanza kuwa ndefu. 😔
Nilifika na kuanza kusubiri mzigo. Nikajiambia, “Labda ni dakika chache tu, utafika.” Dakika zikawa muda, muda ukawa masaa… lakini mzigo hauonekani.
Nikaamua kuwasiliana nao. Jibu nikapewa ni, “Tulia, mzigo utafika saa hii.”
Nikajituliza.
Muda mwingine unapita… bado hakuna mzigo.
Nawasiliana tena, naambiwa tena, “Tulia, mzigo utafika saa hii.”
Mpaka sasa bado niko hapa nasubiri. 😔
Kwa kweli, ukiwa kwenye situation k**a hii, mawazo yanaweza kuwa mengi. Unaweza kuanza kujiuliza maswali mengi, hasa kwa sababu ni mzigo wako, vitu vyako na vitu ambavyo umevifanyia kazi.
Lakini pamoja na yote haya, nimeamua kutokuwa na haraka ya kuhukumu mtu. Bado nimechagua kuwa na subira kwa sababu nawatrust Heha Movers na naamini watatimiza walichoniambia.
Mimi kwa sasa nimeamua kuweka kila kitu mikononi mwa Mungu. 🙏
Kwa hiyo watu wangu, naomba mnishikie kwa maombi. 🤲