Habari 254 tv

Habari 254 tv Habari Tendeti Za Afrika Ya Mashariki News And Entertainment
(1)

NABII TITO MBARONI !Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Tito Onesmo Machibya, maarufu k**a “N...
15/08/2026

NABII TITO MBARONI !

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Tito Onesmo Machibya, maarufu k**a “Nabii Tito”, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo, matusi na uchochezi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, mtuhumiwa alik**atwa usiku wa Agosti 15, 2026 katika eneo la Sinza Makaburini, wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Polisi wamesema uchunguzi kuhusu tuhuma hizo unaendelea, huku taratibu za kisheria zikikamilishwa ili mtuhumiwa afikishwe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi.

UPINZANI NCHINI ZAMBIA INASHUTUMU TANZANIA KUINGILIA UCHAGUZI NCHINI HUMO  Mgombea urais wa chama cha NRPUP nchini Zambi...
15/08/2026

UPINZANI NCHINI ZAMBIA INASHUTUMU TANZANIA KUINGILIA UCHAGUZI NCHINI HUMO

Mgombea urais wa chama cha NRPUP nchini Zambia, Brian Mundubile, amewaonya Watanzania anaodai wamehusika katika siasa za Zambia, akiwataka kuondoka nchini humo.

Mundubile amesema Zambia si Tanzania na kwamba mbinu za kisiasa zinazoweza kufanya kazi Tanzania haziwezi kutumika nchini Zambia.

"Ndugu zangu Watanzania ambao mmekodiwa, tafadhali tokeni katika nchi yetu."

Amesema chama tawala cha UPND hakiwezi kushinda uchaguzi huo na kukituhumu kutumia kile alichokiita "mbinu ya Tanzania" ili kupata ushindi.

"UPND hawawezi kushinda uchaguzi huu, hakuna muujiza. Sasa wameamua kutumia mbinu ya Tanzania. Zambia si Tanzania. Hii ni Zambia. Wale wanaofikiri wanaweza kuingiza katika nchi hii mbinu inayofanya kazi Tanzania, hawawezi kufanikiwa kamwe."

Kauli ya Mundubile imekuja wakati mchakato wa kuhesabu kura katika uchaguzi wa Zambia ukiendelea chini ya ulinzi mkali, baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zambia kusimamisha kwa muda zoezi hilo kufuatia taarifa za mashambulizi dhidi ya maafisa wa uchaguzi na kuibwa kwa kura. Tume hiyo imesisitiza kuwa wagombea hawapaswi kujitangaza washindi kabla ya matokeo rasmi kutangazwa.

Mundubile, ambaye ni mmoja wa wagombea wakuu wa upinzani, tayari amejitangaza mshindi wa uchaguzi huo, licha ya Tume ya Uchaguzi ya Zambia kutokuwa imetangaza matokeo ya mwisho.

Jeshi La Polisi Limetoa Taarifa Kuhusu Kuk**atwa Kwake Wakili Wa Kujitegemea Peter Madeleka .Taarifa Inasema Wakili Husi...
15/08/2026

Jeshi La Polisi Limetoa Taarifa Kuhusu Kuk**atwa Kwake Wakili Wa Kujitegemea Peter Madeleka .

Taarifa Inasema Wakili Husika Alidhalilisha Na Kudharau Amri Ya Mahak**a Kuu

MKENYA AKAMATWA ZAMBIA ,UCHAGUZI Mamlaka nchini Zambia zinamshikilia raia wa Kenya, kati ya watu wanne wanaotuhumiwa kuh...
14/08/2026

MKENYA AKAMATWA ZAMBIA ,UCHAGUZI

Mamlaka nchini Zambia zinamshikilia raia wa Kenya, kati ya watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika mpango wa kuingilia mfumo wa uchaguzi nchini humo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa wa Zambia, Dickson Matembo amesema Mkenya huyo Michael Njuka (56), ambaye pia ametajwa na mamlaka k**a Michael Juga, alik**atwa Jumatano na vyombo vya usalama vya Zambia.

Mamlaka zimesema Njuka pamoja na watu wengine wawili, walikuwa wamepewa mkataba wa kufanya uhalifu wa kimtandao uliolenga Serikali na walikusudia kuhujumu miundombinu ya uchaguzi nchini humo.

“Katika tukio linalohusiana, Serikali imemk**ata raia wa Kenya, Michael Njuka, mwanamume mwenye umri wa miaka 56, anayedaiwa kupewa mkataba wa kufanya uhalifu wa kimtandao dhidi ya Serikali,” amesema Matembo katika taarifa hiyo.

Kuk**atwa kwake kulitokana na operesheni kubwa ya kiintelijensia iliyofanywa na kikosi cha pamoja cha vyombo vya ulinzi na usalama siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Zambia wa Agosti 13, 2026.

WAKILI MSOMI PETER MADELEKA AKAMATWA!Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo tarehe 14 Agosti, 2026, saa 9.30...
14/08/2026

WAKILI MSOMI PETER MADELEKA AKAMATWA!

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo tarehe 14 Agosti, 2026, saa 9.30 alasiri, limemk**ata Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, akiwa katika eneo la Mikocheni B, Kinondoni. Madeleka amek**atwa akiwa katika viunga vya Mahak**a ya Uhujumu Uchumi (maarufu k**a Mahak**a ya Mafisadi) wakati akitekeleza majukumu yake ya kitaaluma.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, Madeleka anashikiliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahak**a Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na tarehe 13 Agosti, 2026.

“Lilimk**ata na linamuhoji Peter Madeleka, kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahak**a Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi “Mahak**a ya Mafisadi” iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na 13 Agosti, 2026. Taratibu za kisheria zinatekelezwa ili kumfikisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi”, imeeleza polisi.

Kuk**atwa huku kumetokea saa chache baada ya Wakili Madeleka kufanya mkutano na waandishi wa habari akitangaza nia yake ya kufungua kesi kupinga zuio la Msajili wa Mahak**a Kuu linalowazuia mawakili kufanya mahojiano na vyombo vya habari mahak**ani.

Taarifa za awali kutoka kwa Wakili Gideon Mathew zilieleza kuwa wakati wa uk**ataji huo, watu waliojitambulisha k**a polisi walichukua pia gari la Madeleka, fedha, na nyaraka mbalimbali alizokuwa nazo.

Aidha, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilieleza kupokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kikitoa wito kwa mawakili waliopo Dar es Salaam na maeneo ya jirani kufika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) ili kutoa msaada wa kisheria na kuhakikisha Wakili Madeleka anapata usaidizi unaostahili

“Chama cha Wanasheria Tanganyika kinaendelea kusimamia na kutetea haki, utu na uhuru wa mawakili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma kwa mujibu wa sheria,” imeeleza taarifa ya TLS iliyotolewa na Baraza la Uongozi.

TUNAFANYA UCHUNGUZI, ARUSHA ! Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza Askari hao wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi kufuatia ...
14/08/2026

TUNAFANYA UCHUNGUZI, ARUSHA !

Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza Askari hao wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi kufuatia kifo cha fundi gereji Sefu M***a (25) na kujeruhiwa kwa Salimu Haji Chambega, Agosti 12, 2026, tukio lililotokea ndani ya hifadhi hiyo, ambapo kwa mujibu wa Abdallah Nuru Ngandana aliyekuwa pamoja na wenzake hao alisema walishikiliwa baada ya kupotea njia walipokuwa wakielekea msibani Babati.

WASIWASI, VIKUNDI VYA WAALIFU Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amee...
14/08/2026

WASIWASI, VIKUNDI VYA WAALIFU

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuibuka kwa vikundi na watu binafsi wanaojianzishia "vikosi" na wengine kutumia lugha za matusi na kashfa mitandaoni bila kukemewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 13, 2026, Padre Kitima amesema kuwa vitendo hivyo vinavuruga utamaduni wa Watanzania wa kupenda ukweli akisisitiza kuwa nchi tayari ina vyombo imara na vinavyofahamika kisheria kwa ajili ya ulinzi na usalama, vikiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Polisi, hivyo hakuna haja ya kuruhusu "vikosi" visivyo rasmi kuchukua nafasi hiyo.

“Nchi hii tunajua sisi tuna vikosi vya kuleta ulinzi na usalama. Tuna vyombo maalum... Sasa mtu mmoja anaamka tu huoni akikemewa huoni mwingine anaamua yaani kumtukana fulani tu. Mwingine anaamua yaani kutukana watu tu na anaachwa,” amesema Padre Kitima.

Amehoji kuhusu watu wanaofadhili vikundi hivyo ambavyo kazi yake ni kushambulia watu, viongozi, na taasisi akisema, “Ni wazi tunaona wapambe wa kwenye mitandao…tusipoangalia wanaweza wakavuruga zaidi utamaduni wa kuwa watu wa kweli. Eh kwasababu uongo mwingi unapita kwenye mitandao na tunajiuliza anayevigharamia hivyo ni nani?” amehoji kiongozi huyo.

Padre Kitima ametoa wito kwa serikali kujali sauti za wananchi na kukemea vikundi hivyo vinavyoonekana vimepangwa kwa malengo ya kisiasa. Amehimiza Watanzania washik**ane na serikali yao wakiongozwa na misingi ya ukweli na uadilifu ili kuliponya taifa kufuatia mivutano iliyojitokeza baada ya uchaguzi wa mwaka 2025.

SHAHIDI APATWA NA DHARURA YA AFYA Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...
14/08/2026

SHAHIDI APATWA NA DHARURA YA AFYA

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imeshindwa kusikilizwa leo Ijumaa, Agosti 14, 2026, baada ya shahidi wa 18 wa upande wa mashtaka kudaiwa amepata dharura ya kiafya na kushindwa kufika mahak**ani kutoa ushahidi wake.

Upande wa Jamhuri umeiomba Mahak**a kuahirisha kesi hiyo hadi siku nyingine, ukidai kuwa shahidi huyo amepata changamoto ya kiafya na kwenda hospitalini.

Hata hivyo, Lissu amepinga ombi hilo akisema tayari Mahak**a ilitoa amri kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi wasiopungua wawili kila siku kesi inapokuwa inasikilizwa. Hivyo, aliiomba Mahak**a isikubali ombi la Jamhuri.

Lissu almesisitiza kuwa yupo tayari kuendelea na kesi hiyo siku ya leo na kutaka upande wa mashtaka ulete mashahidi wen gine mahak**ani. Amesema iwapo Jamhuri imeshindwa kuendelea na ushahidi, basi ifunge ushahidi na kesi iende kwenye hatua nyingine, akidai upande huo "umekata pumzi."

Hata hivyo, Jopo la majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiana na James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, limekubali ombi la upande wa Jamhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.

PADRE KITIMA AFICHUA SIRI NZITO YA KIKAO CHA TEC NA RAISI SAMIA Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeweka wazi...
13/08/2026

PADRE KITIMA AFICHUA SIRI NZITO YA KIKAO CHA TEC NA RAISI SAMIA

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeweka wazi kuwa lengo kuu la kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutoa mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa nchini na kushauri njia bora ya kuiponya nchi kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kufuatia kikao hicho kilichofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, Agosti 10, 2026, Katibu Mkuu wa TEC, Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa mkutano huo ulitokana na ombi la maaskofu wenyewe waliotaka kumshirikisha Rais maoni yao.

Padre Kitima ameeleza kuwa maaskofu wamewasilisha andiko rasmi lenye kurasa nne ambalo linasisitiza umuhimu wa kusimamia ukweli na msamaha ili kurejesha utulivu wa kweli nchini.

“Kutokana pia na kwamba waliweka eh bayana kwamba ili tutoke katika hali hii inabidi kwenda katika kusimamia ukweli na vile vile kutakana msamaha, kusameheana na hata kuponya nchi. Kwa hiyo kwa kiingereza tunasema ‘to admit the truth then reconciliation healing the nation’,” amesema Padre Kitima.

Padre Kitima amewataka Watanzania kuwa na imani na ujumbe uliowasilishwa na maaskofu na kuwa na utulivu wakati serikali ikielekea katika kutatua mkwamo wa kisiasa uliopo nchini.

Ujumbe Wa Mange Kimambi Akificuhua Mpango Mzima Wa Kuwahonga Wana CHADEMA '' Kuna habari nimeipata  ila kwa vile sina ev...
12/08/2026

Ujumbe Wa Mange Kimambi Akificuhua Mpango Mzima Wa Kuwahonga Wana CHADEMA

'' Kuna habari nimeipata ila kwa vile sina evidence ya 100% basi sitotaja majina directly ila issue iko hivi, JK has come up with a plan ya kuitawanya Chadema k**a alivyofanya kwenye Urais wake kwa kuanzisha ACT Wazalendo na kimama kaanza kuitekeleza plan hii.

Abdul na mama yake kwa sasa wanafanya big financial investment kwa viongozi wa Chadema kupitia business mpya.

Nimeambiwa Kuna Bank inaitwa Bank M itatangaza kufilisika kisha watainunua wao kina Abdul k**a taasisi ya pesa yenye leseni, watainunua kwa bei ndogo sana na kuiendesha k**a Bank binafsi- yenye udhamini wa BoT.

Wanajipanga kufungua bank ya kifisadi ambayo itatumika kupitisha pesa zao za wizi endapo USA wanaweka sanctions kwenye mfumo wa fedha, inorder to by pass possible coming sanctions. Wanatengeneza hiyo shadow banking network and some viongozi wa Chadema wamepewa shares kwenye huu uharamia ili kusaliti wananchi……

Bank M iko chini ya mfilisi ila soon Bank M itakuwa activated with “foreign owners” na itakuwa foreign bank yenye wateja TZ. Hao “foreign owners” ndio mpaka some viongozi ndani ya Chadema wako. Kuna kiongozi mmoja ndani ya Chadema huyu mpaka katoa maelekezo kuwa hii bank iwe na HQ nchi flani.

Nimeambiwa Mbowe keshaanza kujenga majengo Dodoma ambayo atawakodishia hii bank.

Yani its a network made up of some viongozi wa Chadema wakishirikiana na wauwaji wa October 29. Yani CCM wamekubali kula na viongozi ndani ya Chadema ili mradi haki isipatikane Tanzania.

Naomba kila mtu asave hii posti coz kuna siku nitarudi ku refer to this post. Please save this post.''

Address

Kileleshwa

Telephone

+254704000104

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari 254 tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Habari 254 tv:

Shortcuts

Share