Hujambo Mkatoliki

Hujambo Mkatoliki Pata habari tendeti na mafundisho kuhusu imani ya kanisa katoliki ndani na nje ya Kenya.

Matukio ya picha wakati wa ibada ya wafu na mazishi ya mtawa Sr. Ancilla Wasai katika kanisa la Our Lady of Good Hope Ca...
27/08/2026

Matukio ya picha wakati wa ibada ya wafu na mazishi ya mtawa Sr. Ancilla Wasai katika kanisa la Our Lady of Good Hope Catholic Church Bura.
Raha ya milele mpe ee bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.

SPIKA WA BUNGE LA KITAIFA CHINI KENYA MOSES WETANGULA  NA BAADHI YA WABUNGE WAKUTANA NA PAPA LEO XIV MJINI VATICANMatuki...
26/08/2026

SPIKA WA BUNGE LA KITAIFA CHINI KENYA MOSES WETANGULA NA BAADHI YA WABUNGE WAKUTANA NA PAPA LEO XIV MJINI VATICAN

Matukio ya picha wakati spika wa bunge la kitaifa na baadhi ya wabunge kutoka Kenya walikutana na baba mtakatifu Leo XIV mjini Vatican.
Wabunge waliokuwepo ni pamoja na
Mhe.Peter Kaluma, mhe. John Bwire, mhe. Lydia Haika, mhe. Katana Kahindi,Mhe. Paul Abuor na balozi Rose Sumbeiywo.

MWANAUME AJIFANYA PADRE, AONGOZA MISA NA HATA KUPEANA SAKRAMENTI TURKANAJimbo Katoliki la Lodwar limetoa taarifa kuhusu ...
21/08/2026

MWANAUME AJIFANYA PADRE, AONGOZA MISA NA HATA KUPEANA SAKRAMENTI TURKANA

Jimbo Katoliki la Lodwar limetoa taarifa kuhusu mwanaume mmoja kutoka Kisii ambaye alijifanya padre mmisionari na hata kupeana sakramenti katika jimbo hilo.
Inasemekana kwamba Jones Ochonga kutoka kisii ameshikwa na polisi baada ya kujifanya yeye ni padre ilhali ana mke na watoto nyumbani huko Kisii.
Inasemekana kwamba alikuwa na stakabadhi ghushi na Kanisa katoliki sasa limejitenga naye na kuambia waumini wake wawe makini.

MKENYA ATEULIWA NA PAPA LEO XIV KUFANYA KAZI KATIKA IDARA YA VATICAN YA KUKUZA MAENDELEO JUMUISHI YA BINADAMUMkenya Lucy...
20/08/2026

MKENYA ATEULIWA NA PAPA LEO XIV KUFANYA KAZI KATIKA IDARA YA VATICAN YA KUKUZA MAENDELEO JUMUISHI YA BINADAMU

Mkenya Lucy Afandi Esipila ameteuliwa na Papa Leo k**a mtaalam katika idara ya Vatican ya Kukuza Maendeleo Jumuishi ya Binadamu.
Idara hiyo ilianzishwa na Papa Francisko mwaka wa 2016 na kuanza rasmi kufanya kazi tarehe 1 Januari 2017.
Majukumu yake makuu ni pamoja na kukuza heshima na utu wa kila binadamu pamoja na maendeleo ya mtu kwa ukamilifu. Inashughulikia masuala k**a amani na haki,
haki za binadamu na utu wa binadamu,
kupambana na umaskini na kutengwa katika jamii.

RAIS AKUTANA NA MAASKOFU WAKUURais Dr. William Ruto akutana na kufanya mazungumzo na maaskofu wakuu wanne wa majimbo mak...
19/08/2026

RAIS AKUTANA NA MAASKOFU WAKUU

Rais Dr. William Ruto akutana na kufanya mazungumzo na maaskofu wakuu wanne wa majimbo makuu tofauti nchini Kenya.
Wanne hao ni Philip Anyolo (Nairobi), Maurice Muhatia (Kisumu), Anthony Muheria (Nyeri) na Dominic Kimengich (Mombasa).

Askofu wa tano wa jimbo katoliki la Kitui Mhashamu John Mbua Mwandi .Hongera baba askofu.
09/08/2026

Askofu wa tano wa jimbo katoliki la Kitui Mhashamu John Mbua Mwandi .
Hongera baba askofu.

MISA YA SAKRAMENTI YA DARAJA TAKATIFU YA UPADRE YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA KATIKA JIMBO KATOLIKI LA KAPSABET.
25/07/2026

MISA YA SAKRAMENTI YA DARAJA TAKATIFU YA UPADRE YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA KATIKA JIMBO KATOLIKI LA KAPSABET.

19/07/2026

Mkutano mkuu wa 21 wa AMECEA

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 21 WA AMECEAMatukio ya picha wakati wa adhimisho la sadaka ya Misa Takatifu ya ufunguzi wa M...
19/07/2026

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 21 WA AMECEA

Matukio ya picha wakati wa adhimisho la sadaka ya Misa Takatifu ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 21 wa AMECEA iliyofanyika leo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) jijini Nairobi.

Ibada hiyo ya misa takatifu iliongozwa na Mwadhama Michael Kardinali Czerny S.J, Mkuu wa Baraza la Kipapa la Kukuza Maendeleo Endelevu ya Binadamu.

Address

Opposite Kisii Main Stage
Kisii
40200

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hujambo Mkatoliki posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share