06/09/2026
Picha moja inayoweza kuandika kurasa elfu moja za kitabu. Baba Askofu Yuda Thadeus Ruwaichi, OFM Cap (nyuma) akiongozana na wasaidizi wake wawili, Askofu Henry Mchamungu (kushoto) na Askofu Vincent Mpwaji (kulia) katika Misa takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vincent Mpwaji, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki DSM, katika Viwanja vya Msimbazi Center.
Kwanini picha hii ina maana kubwa? Mwaka 1995 wakati Vincent Mpwaji akiwa mwanafunzi wa kidato cha 3 shule ya seminary Visiga, Henry Mchamungu alikuwa Mwalimu wake wa Biology.
Askofu Mchamungu baada ya kuhitimu shahada ya kwanza ya falsafa (Bachelor degree in Philosophy) na shahada ya theolojia (Bachelor degree in Theology), alitumwa kusomea shahada ya ualimu (Bachelor degree in education) akijiegemeza katika masomo ya Biology na Chemistry.
Mwaka 1995 alitumwa seminary ndogo ya Visiga kufundisha Somo la Biology. Kati ya wanafunzi aliowafundisha ni Baba Askofu Vincent Mpwaji akiwa kidato cha tatu. Leo wote wawili (Mwalimu na mwanafunzi wake) ni Maaskofu wasaidizi (Auxiliary Bishops) wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam.
Hii ni neema kubwa, mwalimu na mwanafunzi wake kufanya kazi kwa pamoja shambani mwa BWANA. Mhashamu Henry Mchamungu aliteuliwa July 07, 2021 kuwa Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Mhashamu Vincent Mpwaji aliteuliwa July 11, 2026.
Hivyo basi kwa sasa Jimbo Kuu katoliki Dar es Salaam linaongozwa na Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwaichi, OFM Cap, akisaidiwa na Askofu Msaidizi Henry Mchamungu na Vincent Mpwaji. Tuwatakie heri katika utume wao. Roma locuta, causa finita est 🙏🏽
NB: Swali la kizushi: Wewe na Mwalimu wako wa Form 3 mko wapi sasa hivi??🤣