Akamba Press

Website

Akamba Press ◾ Factual & Clear ◾Kamba language
◾Trusted news ◾Advertise here
◾Akamba Culture
(1)

KUPOTEA KWA MY SIZ PART-11 (FINAL)Niliwatazama wale wanawake kwa makini, na hapo ndipo macho yangu yalipomfikia. Alikuwa...
20/09/2026

KUPOTEA KWA MY SIZ PART-11 (FINAL)

Niliwatazama wale wanawake kwa makini, na hapo ndipo macho yangu yalipomfikia. Alikuwa ni Mwende wetu. 😭😭😭

Mwili wake ulikuwa umejaa makovu na unyonge wa mateso ya muda mrefu, lakini ndani ya macho yake, mwanga wa matumaini ulikuwa umeanza kurudi. Mwende alikuwa hai.

Haikupita hata dakika tano, sauti za king'ora cha polisi zilitikisa msitu mzima. Magari ya kikosi maalumu yaliwasili kwa kasi, askari wakitanda kila pembe huku sauti za amri zikirindima: "Kila mtu chini! Chini haraka!"

Wakubwa wa lile boma la uhalifu walifungwa pingu mmoja baada ya mmoja na kupakizwa kwenye helikopta za kijeshi.

Taa zilimulika pande zote, na bila kupoteza muda, tukang'oa nanga kuondoka kwenye lile pango la mauti.

Kituo cha polisi kilifurika maofisa wakuu huku mahojiano makali yakianza usiku huo huo. Kila mshukiwa alipobanwa, siri nzito zilianza kuvuja.

Lakini katikati ya ushindi huo, kizaizai kipya kilizuka—MASTER hakuwa miongoni mwa waliok**atwa. Mtego wetu ulimpata kila mtu, lakini yeye alikuwa amepenya k**a msumari kwenye shimo la panya.

Kufikia asubuhi, nchi nzima ilikuwa kwenye mshtuko. Radio na Runinga zilikata vipindi na kutangaza operesheni hiyo ya hatari bila kukoma. Vijana, wazee, na kila pembe ya mtaa, hakuna kilichozungumziwa ila uokoaji huo wa miujiza.

Kesho yake, kurasa za mbele za magazeti makuu nchini zilipambwa na vichwa vya habari vilivyosisimua taifa zima:

* Daily Nation: MASTER MEETS SUPER 'MASTER' — How a daring 21-year-old outsmarted a cartel.

* Standard: MASTER ESCAPES TO THE EAST — manhunt intensifies as terror syndicate crumbles.

* The Star: CORNERED AT 21 — The mastermind behind the spine-chilling rescue operation.

Mwishowe, Mwende wetu alirudi nyumbani. Hata k**a Master alikuwa bado yuko mbioni, mchezo wake ulikuwa umefika mwisho, na damu ya familia yetu ilikuwa imeshinda giza.

Fast forward ⏩ ⏩
Sasa nafanya Kazi Na FBI coz Kenya haulipi poa..

Comments 🤣🤣

Vasongetwe ata vaaa?Nani MAKOSA??
20/09/2026

Vasongetwe ata vaaa?
Nani MAKOSA??

Munyuni ndyaakuna Kitingi maishanivaa Kala moto Ni UMO WAKWALekya commentss
19/09/2026

Munyuni ndyaakuna Kitingi maishani

vaa Kala moto Ni UMO WAKWA
Lekya commentss

KUPOTEA KWA MY SIZ PART-10 Asubuhi na mapema, sauti yangu ilikuwa inatetemeka nilipompigia babangu simu. "Dad, niko kari...
19/09/2026

KUPOTEA KWA MY SIZ PART-10

Asubuhi na mapema, sauti yangu ilikuwa inatetemeka nilipompigia babangu simu. "Dad, niko karibu sana kuona mwisho wa hii filamu. Nenda polisi haraka wajiandae!"

Lakini jibu lake lilinipiga na shockwave. "Mwanangu, fanya taratibu," alisema kwa sauti ya chini, "Nimefanya uchunguzi wangu nikagundua MASTER anamfuko mmoja mkubwa sana—OCPD mzima yuko ndani ya mfuko wake! Lakini usijali, OCS yuko upande wetu na tumechora ramani naye bila OCPD kujua. Mjulishe pia Mbunge wetu haraka!"

Mambo yalilipuka kwa kasi ya ajabu. Saa moja tu baadaye, Mzee alinipigia tena—sauti yake ikiwa imejaa msisimko na hofu. "Ujumbe umefika juu zaidi kuliko tulivyofikiria! Story imegusa OCS, County Commissioner, MP, Interior CS, NIS, na hata Mheshimiwa Rais mwenyewe!

Kumbe serikali ilikuwa kwenye msako mkali wa siri kufuatia wimbi la kutisha la kupotea kwa wasichana wadogo wa miaka 18-25 nchi nzima!"

Moyo wangu ulipiga k**a ngoma ya vita. Saa tatu kamili, sauti ya mtangazaji wa redio ilivuma angani:

“Taarifa ya Hivi Punde: Uchunguzi mzito wa kitaifa kuhusu kutoweka kwa mamia ya wanawake nchini umeingia hatua mpya…”

Saa tano kamili, simu yangu iliita. Alikuwa OCS. "Kijana, tuko tayari. Tupe ishara tu!"
Hapa ndipo kiwewe kilipopanda ghorofa ya mia moja!

Nilichukua binoculars zangu, nikatazama mjengo wa MASTER. Kila kitu kilikuwa shwari, hakuna kiumbe kilichoonekana nje. Nilishuka kutoka juu ya mti ule k**a kivuli, nikatembea polepole kuelekea kwenye rundo la taka.

Nilijitupa chini, nikaanza kutambaa kwa tumbo—polepole, hatua kwa hatua. Nilipaswa kuepuka makucha ya CCTV, sensor lights, na pua kali za sniffer dogs zilizokuwa zikizunguka.

Pumzi yangu ilikuwa ndogo sana.
Muda ulienda mbio. Saa 11:55 mchana, nilikuwa nimegusa ukuta wa Master! Kwa vidole vinavyotetemeka, nilipin location na kuituma kwa makomando.

Iliyofuata saa 12:00 kamili mchana ilikuwa k**a sinema ya Hollywood!
Anga ilipasuka kwa ghurudumu kubwa la helikopta! Ndege zilitokea kila pembe zikizunguka mjengo wa Master:

* Ndege 3 za kutisha za KENYA POLICE

* Ndege 2 za uokoaji za AMREF

* Na ndege 5 za siri, hazina majina wala nambari—nyeusi tititi!

KIMEUMANA!

King'ora cha hatari kililipuka kwa sauti ya kukata masikio mjengoni! Mbwa walianza kubweka kwa ukali, na walinzi wa Master waliingiwa na kiwewe, wakitimua mbio na kujifungia ndani.

Anga ilijaa msukosuko, miti mikubwa ikitetemeka kwa upepo wa mapanga ya ndege! Huko nje, ving'ora vya magari ya polisi na ambulansi vililiza mji mzima vikizingira gate kuu na barabara zote za akiba.

Kabla hawajajua kinachoendelea, ndege mbili zilining'inia hewani juu ya uwanja wa Master, na makomando wenye silaha nzito wakaanza kushuka chini kwa minyororo kwa kasi ya ajabu!

Ndege zilitua kwa kishindo, zikitimua vumbi zito na upepo mkali uliotaka kunipeperusha mbali. Mimi nikiwa bado nimejikunyata chini ya vumbi lile, sauti ya radi ilivuma kutoka kwa makomando:

"KILA MTU MIKONO JUU! TUPA SILAAHAAAA!"

Walivunja gate kuu kwa kishindo kikubwa mno. Mipaka ya umeme ikakatwa kwa risasi! Nilisimama haraka nikainua mikono juu huku nikipiga kofi la kifua: "Ni mimi! Ni mimi niliyewatumia location!"

Afisa wa kikosi maalumu aliniangalia, akainua mkono kunipa njia. "Ingieni! Vunja kila mlango!" aliamuru.

Tuliingia ndani k**a dhoruba. Afisa mkuu alipiga yowe lililotikisa nyumba nzima: "KILA MTU TOKA NJE AU TUTAFUNGULIA MOTO!"

Mlango wa basement ulifunguka... na kilichotoka huko kilifanya damu yangu igande.
Watu wengi ajabu walitoka. Wanawake zaidi ya 20—wakiwa wametepeta, wamejaa hofu, na wamevaa nguo za ndani tu—walitoka nje wakilia na kutetemeka kwa baridi na hofu.

Moyo wangu uliruka kitanzi... Je, dada yangu alikuwa mmoja wao?

PART 11 LOADING...

MUSEVENI🤣🤣🤣Musumbi Wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni eesie umanya e muselee kana anachongewa Kiritiri Ni Minaa ya Kenya k...
19/09/2026

MUSEVENI🤣🤣🤣

Musumbi Wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni eesie umanya e muselee kana anachongewa Kiritiri Ni Minaa ya Kenya kwisila G to G conmanship....

WIONA NUU USU INOYAA MBESA SYA ĨSELE?

KATENDE FM VS KWITU FM Yu Radio Ila tutuaa tutambuite Ni KWITU FM nayu ve kangi kekwitwa KATENDE FM we utambuaa yiva? Ka...
19/09/2026

KATENDE FM VS KWITU FM

Yu Radio Ila tutuaa tutambuite Ni KWITU FM nayu ve kangi kekwitwa KATENDE FM

we utambuaa yiva?
Katende or Kwitu?

KUPOTEA KWA MY SIZ-Part 9Niliokota zile nguo pamoja na kile kipande cha karatasi, kisha nikaondoka haraka kuelekea kweny...
19/09/2026

KUPOTEA KWA MY SIZ-Part 9

Niliokota zile nguo pamoja na kile kipande cha karatasi, kisha nikaondoka haraka kuelekea kwenye ule mti.

Mambo mawili yalinikaa akilini vizuri sana:
* Mwende yuko mikononi mwa Master.
* Yuko HIV negative—maana ile lebo iliandikwa A. MWENDE, jina la dada yangu, Ann Mwende.

Lakini ngoja! Kwa nini alipimwa? Je, Master ana tabia ya kuteka wasichana na kuwatumia vibaya kingono? Mbona ana siri nyingi hivi? Na zile chupi nyingi nilizoziona zikitumika zilitoka wapi? Kwani kuna wasichana wengi humu ndani ya boma? Wanafanya nini?

Hata hivyo, sikuona kondomu yoyote iliyotumika. Hiyo ilimaanisha hawezi kumpima mtu leo, amwamini papo hapo, na afanye naye mapenzi bila kinga—lazima asubiri angalau miezi mitatu. Kwa hiyo, kwa sasa Mwende yuko salama

Nilipanda juu ya mti wangu, nikatoa simu na kumtumia babangu ujumbe kumfahamisha kinachoendelea:
"Mwende anaweza kuwa salama, nimeona nguo zake. Tulieni."

Kisha nikaanza kumfanyia utafiti huyo MASTER. Nilianza na gari lake, ile Discovery. Lilikuwa halina namba za usajili mbele wala nyuma—badala yake lilikuwa limeandikwa 'MASTER'. Lakini kuna wakati nililikeribia na kusoma namba yake halisi kwenye vioo: KCU...
Nilipochunguza namba hiyo, nikagundua mmiliki wa gari hilo ni JOHN KORIR.

Nilipotafuta jina la John Korir kwenye Mtandao wa Google, nikagundua kuwa ni daktari wa matibabu—kwa hiyo ni DR. KORIR.
Utafiti wangu ulionyesha maelezo haya kumhusu:

* Aliwahi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji mjini Boston.

* Alikabiliwa na kesi za ubakaji, unajisi, na uuzaji wa dawa za kulevya nchini Marekani kabla ya kurudishwa Kenya (deported).

* Alikuwa na akili nyingi sana alipokuwa shule ya sekondari.

* Alisomea Shule ya Upondaji ya Kapsabet Boys.

* Anajiita 'MASTER', ni mla rushwa mkubwa, na ana hasira za haraka.

* Ameachana na mkewe (divorced).

* Anamiliki silaha nyingi za moto. Fireamrms

Habari hizo zilinitosha kabisa! Nilielewa wazi kuwa Mwende yuko kwenye hatari kubwa na kwamba Master ni mtu tajiri sana na hatari kupindukia.

Siku hiyo iliisha, nikajifungia na kulala kileleni mwa ule mti. Nilifanya uamuzi thabiti kuwa kesho yake ndiyo siku ya kuportusha vita—iwe kufa au kupona, ni lazima nimwone Mwende!

PART 10 LOADING...

KUPOTEA KWA MY SIZ PART 8Nilizinduka kitu saa moja asubuhi nikapata nilikuwa umezirai...nilikuwa na majeraha kwa miguu n...
18/09/2026

KUPOTEA KWA MY SIZ PART 8

Nilizinduka kitu saa moja asubuhi nikapata nilikuwa umezirai...nilikuwa na majeraha kwa miguu na mgongo.

Nilikuwa nasikia njaa sana. Nilikula jana. Maji ya lita moja yalikuwa yamebaki nusu. Ah..nilikumbuka niko na manati...najua kuwinda...

Niliishika vizuri, nikangoja ndege wakaribie...huko msituni ndege hawaogopi...mmoja, njiwa alikaribia, nikamlenga nikampiga jiwe akaanguka...nilimtayarisha kisha nikatengeneza moto kwa kupekecha miti (friction) nikamchoma nikamla...kisha nikatafuta matunda ya msituni nikala...nikanywa maji nikashiba...hayo yakawa maisha ya bushman.

Nilikumbuka agenda yangu. Nikachukua simu nikaenda kwa Google Maps nikaangalia location yangu...nikaona niko kilomita tatu (3km) kwenda kwa boma ya Master...nilifuata njia za nyani na za nguruwe mwitu...polepole...niliangalia simu tena nikaona niko kilomita moja (1km)!!

Hiyo ni safe...nilitafuta mti wenye majani mengi nikapanda polepole nikiwa makini nisipatane na nyoka..

Nilitafuta nafasi nzuri (position) nikawa ninaona kwa Master lakini si kwa uwazi (clearly)...nikichukua darubini yangu (binoculars) nikaangalia...nikaona vizuri...

Kuna nyumba kubwa ya kifahari, iko na kuta mbili na mageti ya chuma.
* Ukiingia gate moja iko upande wa West...
* Ukuta wa ndani gate iko East...

So ukiingia gate ya kwanza unaenda round ndio uingie ya pili...SECURITY NI TIGHT.

Pia kuna shamba hapo kando ya boma,, nikizoom niliona imepandwa bangi nyingi na iko na automated irrigation system.

Niliona kutoka kwa gate around mita 200 kuna dumping site...actually side niko...kwa hivyo hiyo site iko mita 800 kutoka kwa mti wangu.
Niliona msichana amefunguliwa gate na mlinzi, akasimama akamwangalia, akaenda akamwaga takataka kisha akarudi akafungua akaenda ndani.

Nilipata idea....niende polepole nifike kwa hiyo dumping site...

Nilienda polepole nikafika...nikajificha nikachokora takataka...nikaokota:
* Mkate karibu expired
* Kiberiti nusu

Ghafla nikaona kitu kinachofahamika: nguo za Mwende wetu!!! Zimetupwa!! Mwende ako hapo!!!! Amenyang'anywa nguo!!

Niliona kitu kingine...strip ya kutest HIV...ilikuwa labeled AMWENDE.🥹🥹🥹🥹
Tupatane part 9

KUPOTEA KWA MY SIZ - PART 7(big snake just above my head🤣🤣Ghafla, mwangaza mwangavu ukanimlika direct machoni! Nikasikia...
17/09/2026

KUPOTEA KWA MY SIZ - PART 7

(big snake just above my head🤣🤣

Ghafla, mwangaza mwangavu ukanimlika direct machoni! Nikasikia mmoja wao akiongea kwa sauti ya chini, "Kuja uone! What's that...?"
Mwenzake akajibu, "Mbona mimi sioni kitu?" Mara hiyo hiyo, nikasikia PAH!!

Alikuwa amenilenga kwa manati! Mungu wangu, karibu anigonge na gololi ya kichwa 🥺🥺. Licha ya uoga, nilijikaza sikutingisika hata kidogo.

"Kujeni twende! Mnafanya nini huko?" Dereva akafoka kwa ukali.

Wale majamaa wakachukulia poa, "Aah, si mtu bwana, ni majani tu..." Wakatoka mbio na kuondoka. Niliponea chupuchupu!

Bila kupoteza muda, nilijizoa haraka na kupanda juu ya mti mmoja mkubwa. Nikajifunga vizuri na kamba kwenye tawi ili nisianguke nikipitiwa na usingizi.

Masaa ya usiku yalisogea, na mara kwa mara nilisikia milio ya fisi kwa mbali. Bahati nzuri nilijua fisi hawawezi kupanda mti.

Ila ilipofika saa tisa za usiku, niliamka ili nimtumie father text. Ghafla, nikasikia mshindo chini ya mti—alikuwa chui! Alikuwa anataka kupanda, na macho yake yaling'aa gizani yakitazama juu nilipokuwa. Wasiwasi ulinishika sana!!

Nilifikiria kumlika na tochi, lakini nikaona mwanga huo ungetoa ishara kwa wale walinzi waliokuwa mbali. Kwa polepole, nilichukua manati yangu, nikaweka jiwe zito, kisha nikamlenga direct kwa pua... PWAH!! Jiwe lilimfika sawasawa, na akatimua mbio za kuokoa maisha yake 😀.

Asubuhi na mapema, ndege walijaza anga kwa nyimbo zao na kukaingia nuru.

Nilitazama chini nikaona kuko shwari. Hata hivyo, pale mtini majani yalikuwa mengi sana. Nilianza kujifungua kamba polepole nikiwa na mpango wa kushuka chini niishiwe na haja—njaa ilikuwa inaniuma hatari na hakuna hata chai!

Ghafla, nikasikia sauti ya ajabu juu yangu. Kugeuka tu... NYOKA MKUBWA NA WA HATARI alikuwa amejipinda kwenye matawi, inchi chache kutoka kwa kichwa changu!

Bila kufikiria mara mbili, nilijirusha chini papo hapo! Nilianguka chini k**a gunia la viazi na ghafla kiza kinene kikaniingia...nilizirai😭😭😭

Tupatane PART 8...

comments please... story ikoje

Read the other parts here Akamba Press

17/09/2026

HII Maua kwenu munaiitaje....very beautiful Na inamea wakati wa kiangazi

Address

Kitui

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Akamba Press posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share