29/07/2025
Kwakya kwa Thome Peter Mutinda Kasuva MKay Entertainment
Listen to THOME F.M - https://onlineradiobox.com/ke/thome/
MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 29, 2025
JUMA LA 17 LA MWAKA
Kumbukumbu ya Familia ya Martha, Maria na Lazaro
SOMO 1
K*t. 33 : 7-11; 34:5-9,28
Desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, Hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa Bwana, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye Bwana akasema na Musa. Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake.
Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso. k**a vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumish wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana hakutoka mle hemani.
Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimam; pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu. Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne. Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako. Naye alikuwa pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano. hizo amri kumi.
Neno la Mungu...Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 103 : 6-13 (K) 8
(K) Bwana amejaa huruma na neema.
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,
na hukumu kwa wote wanaoonewa.
Alimjulisha Musa njia yake,
wana wa Israeli matendo yake. (K)
Bwana amejaa huruma na neema,
haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Yeye hatateta sikuzote,
wala hatashika hasira yake milele. (K)
Hakututenda sawasawa na hatia zetu,
wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa wamchao. (K)
SHANGILIO
2Tim 1:10
Aleluya, aleluya,
Mwokozi wetu Yesu Kristu alibatili mauti,
na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
INJILI
Yn. 11:19-27
Watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, k**a ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; nave kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! unayasadiki hayo?
Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Au
INJILI
Lk. 10 : 38-42
Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamkw mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.