11/12/2025
Mwisho wa mwaka unakaribia, na ninauangalia mwaka huu k**a Almasi niliyopewa na Mungu—imechongwa na safari, mapito na neema zake. Shukrani za dhati kwa Ndugu, Rafiki na Mashabiki wangu kwa kunisimamia, kuniamini na kuniombea.
Najua wapo wanaodhani tayari nimeshatoboa… lakini ukweli ni kwamba bado napambana kimya kimya na changamoto zangu. Ukimya wangu haukuwa mwisho, bali ulikuwa hatua ya kukusanya nguvu.
Hata baada ya kutoa vibao k**a na niliyomshirikisha msanii wangu wa kwanza chini ya label yangu Digo Talent, Lapozey—moyo wangu bado upo kwenye muziki, na matumaini yangu ni makubwa kuliko ilivyowahi kuwa.
Nimerudi tena, nikiwa na njaa mpya ya ubunifu na juhudi. 💯🔥🎼
Kwa mashabiki wangu: Endeleeni kuwa na imani—mwaka ujao tunawasha moto zaidi.🔥🙏🏽❤️✨ fans