19/11/2025
Kwa mara nyengine tena, gatizi la Kwale limetunukiwa fursa ya kuandaa mashindano ya kimataifa ya Baiskeli kuanzia tarehe 20 November Hadi tarehe 23 November 2025.
Mashindano hayo yanalwta washiriki kutoka zaidi ya mataifa 20 ya Africa huku wafebi tofauti kutoka Afrika na nje ya Africa wakitarajiwa kutua katika gatizi la Kwale.
Miongoni mwa vitengo vitakavyo kuwa katika mashindano haya ni pamoja na kitengo kwa washiriki chini ya miaka 23, wazoefu wa k**e na wakiume na pia kitengo jumuiya ambapo kila mmoja ataruhusiwa kuingia mashindano mradi ana Baiskeli yake (Fun Day)
Hatahivyo gatizi la Kwale limehakikishia wale watakaoshiriki katika mashindano hayo usalama wa kutosha kupitia vitengo vya usalama vya kitaifa na vile vya kaunti ya Kwale .
Barabara mbandala zimetengwa kwa wasafairi ambayo hawashiriki mashindano hayo kwa usaidizi wa maafisa wa trafiki.
Kilele Cha mashindano hayo tarehe 23 Novemba kitakuwa katika mji wa Kwale katika afisi za mstaiki gavana wa Kaunti ya Kwale ambapo watapokewa na gavana Fatuma Achani, Waziri wa michezo Salim Mvurya miongoni mwa viongozi wengine.