18/08/2026
🚨Anko Dozer Aibua Maswali Kuhusu Hatma ya Kamoti Junior Super Cup
Huku mashabiki na wafuataji wa Kamoti Junior Super Cup wakisubiri kwa hamu hatma ya mchezo wa nusu fainali kati ya Kaliangombe FC na Power FC, ambao ulitibuka na kusababisha mchezo huo kusimamishwa, maswali mapya yameibuka kuhusu k**ati inayoendesha mashindano hayo na mustakabali wa mashindano hayo kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Anko Dozer, Malenga wa Rabai na mkereketwa wa soka, ameeleza kusikitishwa na kuhuzunishwa na kile alichodai kuwa ni kauli iliyotolewa hadharani na mwanak**ati wa Football inayoongozwa na Mdzomba, akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja kupitia mtandao wake.
Dozer anadai kuwa katika maelezo hayo, ilielezwa kwamba k**ati hiyo inayotarajiwa kutoa uamuzi kuhusu sakata la mchezo wa Power FC dhidi ya Kaliangombe FC haipo tena kwenye Kamoti Junior Super Cup, baada ya kujitoa katika mashindano hayo tangu hatua ya 16 bora.
Kauli hiyo imeibua maswali mengi miongoni mwa wadau na mashabiki wa soka Rabai, hasa ikizingatiwa kuwa bado kuna mvutano kuhusu uamuzi wa mchezo huo wa nusu fainali.
Akizungumzia suala hilo, Anko Dozer ameibua maswali kadhaa yanayohitaji majibu kutoka kwa wahusika, ikiwemo:
Je, sababu ya kujiondoa ni kwa kuwa kuna mwanasiasa ambaye hawamkubali?
Je, k**ati haikupewa kile ilichostahili?
Je, vilabu vinavyoshiriki mashindano hayo vinafahamu kuhusu kujiondoa kwa k**ati hiyo?
Je, wamejiondoa kwenye mashindano yote yajayo au ni Kamoti Junior Super Cup pekee?
Au wamejiona kuwa majukumu yao yanaingiliwa na k**ati ndogo ya Kamoti?
Na k**a suala la Power FC na Kaliangombe FC lisingetokea, je, mashindano yangeendelea hadi fainali bila mashabiki kufahamu kwamba k**ati hiyo ilikuwa imejiuzulu au kujiondoa tangu hatua ya 16 bora?
Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Kamoti Junior Super Cup yanaendelea kuelekezwa kwa k**ati husika, wakisubiri ufafanuzi rasmi kuhusu hatma ya mchezo wa Power FC dhidi ya Kaliangombe FC pamoja na nafasi ya k**ati hiyo katika uendeshaji wa mashindano.
Maswali yaliyoibuliwa na Anko Dozer yameongeza mjadala miongoni mwa wadau wa soka Rabai, huku wengi wakisubiri kauli rasmi kutoka kwa k**ati ya maandalizi ili kuweka wazi hali halisi ya mambo na hatua zitakazofuata katika Kamoti Junior Super Cup, Toleo la Tatu.