Kigoma Yetu

Kigoma Yetu Pata habari kemkem zilizojiri katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu na nje ya nchi kupitia KIGOMA H

21/10/2023

1. Kuchagiza Sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, uvuvi, usafirishaji na utalii kupitia kuimarisha miundombinu ya bandari zetu.

2. Kunufaika zaidi kibiashara kwa kuwa na uwezo wa kuhudumia soko kubwa la Afrika ya Kati hususani DRC.

3. Itakuza sekta ndogo ya usafiri kwa njia ya reli na barabara kwa kuongeza kiasi cha shehena kitakachokuwa kinapita katika bandari zetu

4. Tanzania itakuwa na mifumo ya TEHAMA ya kisasa, inayosomana, na hivyo kuondoa upotevu wa mapato bandarini

5. Mitambo ya kuhudumia meli na shehena na ujuzi vitakavyowezesha kuhudumia meli kubwa na za kisasa tofauti na sasa.

6. Kupungua kwa muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24.

7. Kupungua kwa muda wa ushushaji wa makontena kutoka siku 4.5 mpaka siku 2;

8. Kupungua kwa muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 kutokana na uboreshaji wa mifumo na miundombinu.

9. Kupungua kwa gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje kwenda nchi za Jirani kwa Zaidi ya nusu kutoka Dola za Marekani 12,000 mpaka Dola za Marekani 6,000 – 7,000.

10. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani 47.57 mwaka 2032/33.

11. Kuongezeka kwa Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya Forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini.

12. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33.

13. Kupungua kwa gharama za bidhaa zinazoingizwa nchini kutokana na kuwa na gharama ndogo za bandari; na

14. Kuongezeka kwa uwezo wa Serikali kuwekeza katika maeneo mengine kutokana na kuongezeka kwa mapato.

21/10/2023

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kwa waganga wa kianyeji pindi wanapoumwa na badala yake wawapeleke hospitali.

DC Nkumba ameyasema hayo wakati hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba katika zahanati ya Bulangwa iliyo wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo kampuni ya ESAP Mining Services imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni Sita.

“Watoto wanapopata changamoto yoyote ile tafadhali kabla ya kuwapeleka kwa waganga wa tiba asili tujitahidi sana maana watoto wana magojwa mengi nyemelezi tuwalete kwenye maeneo ambayo wanaweza kupata huduma za upimaji na wakajua matatizo yao ili waweze kupatiwa huduma.” - DC Said Nkumba

MCHUNGAJI WA KENYA ALIYEWAAMINISHA WAUMINI KUFUNGA HADI KUFA ILI WAKUTANE NA KRISTO!Historia fupi ya Mchungaji Paul Nthe...
26/04/2023

MCHUNGAJI WA KENYA ALIYEWAAMINISHA WAUMINI KUFUNGA HADI KUFA ILI WAKUTANE NA KRISTO!

Historia fupi ya Mchungaji Paul Nthenge ambaye aliwaanisha Waumini kufunga bila kula kwa siku kadhaa ili kumuona Yesu.

Huyu ni Paul McKenzie Nthenge wakati kanisa lake la Good News International huko Malindi lilipoimarika miaka michache iliyopita. Hakuwa mtu aliyechanganyikiwa, k**a alivyochanganyikiwa anavyoonekana katika runinga leo.

Alianza kanisa hili mwaka 2003 k**a kituo kidogo cha kiinjilisti pamoja na Mkewe Joyce Mwikamba.Kisha walihamia kijiji kiitwacho Migingo huko Malindi ambako alianzisha kanisa katika boma lililozungukwa na ukuta, ambamo familia yake bado inaishi hadi sasa. Mkewe Joyce anamsaidia katika kuhubiri k**a Mchungaji mwenza huku McKenzie akidai kuwa na uwezo wa kuzungumza na Mungu MOJA KWA MOJA. Katika mahubiri yake, alidai kutoa maneno k**a yalivyotolewa na Mungu mwenyewe. Ikiwa inamaana kwamba alitumia maneno ya Mungu katika mahubiri na fundisho yake.

Mwaka wa 2016, Mckenzie alipata kituo cha televisheni baada ya mmoja wa wafuasi wake Kennedy Mwacharo kumuuzia mali yake huko Lamu yenye dhamani. Mali hiyo na biashara hiyo ya runinga inasemekana kwamba Mckencie alinuwa shilingi Milioni 20 na kumkabidhi pesa zote, huku muuzaji Kennedy Mwacharo akiacha familia na majukumu yake. Mali hiyo ilikuwa na thamani ya zaidi ya Milioni 100 wakati huo. Kennedy Mwacharo alifariki miezi miwili baadaye katika hali isiyoeleweka.

Kesi kadhaa za watu kuuza mali zao na kumpa McKenzie wakati wakingojea ujio na kukutana na Yesu zilizidi kuwa nyingi, moja ya hivi karibuni ikiwa Betty, Muhudumu wa ndege za usafiri ambaye aliacha kazi aliyokuwa ameifanya miaka 11.

Alimwacha Mumewe na kuuza mali na vitu alivyokuwa amenunua na kuwekeza wa maisha yote kwa bei chini ya milioni 7 na kuelekeza fedha hizo katika kanisa la McKenzie la Shakaola. Betty anashukiwa kuwa miongoni mwa maiti zinazookotwa kwenye makaburi huko Shakahola.

Inadaiwa kuwa McKenzie alitumia pesa ambazo Kennedy Mwacharo alimpa kununua vipande vya ardhi huko Malindi na Mombasa, magari mawili na kuanzisha kituo cha runinga. Kupitia kituo chake cha TV, Mckenzie aliwafikia watu wengi sana na mafundisho yake kimsingi yalikuwa juu ya nyakati za mwisho, uovu wa njia za maisha za kimagharibi k**a vile huduma za matibabu, elimu, chakula, michezo, muziki n.k.

Mackenzie alikaa juu ya ubatili wa maisha na alisisitiza juu ya maisha ya baadaye. Alihubiri kuhusu ujio wa pili wa Kristo ambao kulingana naye ulikuwa upesi sana - kalenda yake ya ujio wa mara ya pili wa Yesu Kristu ilikuwa daima chini ya mwaka mmoja. Pia alikazia fikira ghadhabu iliyowangojea wale ambao wangekuwa hai kufikia wakati huo. Hofu inayotokana na dhana hii potovu huenda ikawa chanzo cha wafuasi wake kutaka kufa ili siku hiyo isije ikawapata wakiwa hai.

Mwaka 2018 Dkt. Ezekiel Mutua kupitia Baraza la Kenya la kuainisha Filamu KFCB aliamuru kufungwa mara moja kwa kituo hicho cha runinga, hii ilikuwa mwaka mmoja baada ya Mckenzie na Mkewe kufikishwa mahak**ani kwa itikadi kali za kidini, kufunza visivyo na kukiuka uhalali mfumo wa imani uliokithiri kwa madhumuni ya kurahisisha itikadi na kuleta mabadiliko ya kidini na kijamii.

Haijafahamika ni jinsi gani kesi hii ilivyoendeshwa licha ya maagizo ya kufungwa kwa kituo cha hicho cha runinga, McKenzie aliendelea nayo jambo lililoonyesha jinsi alivyokuwa na usemi siku hizo. Kumbuka wakati fulani, alimtishia aliyekuwa Mbunge wa Kilifi wakati huo Aisha Jumwa alipotilia shaka baadhi ya mafundisho yake na jinsi alivyowaweka wagonjwa katika boma lake badala ya kuwapeleka hospitalini.
Mwaka 2019, McKenzie aligonga vichwa vya habari tena wakati ndugu wanne kutoka magharibi mwa Kenya sehemu ya Mumias walipoondoka nyumbani kujiunga na Mckenzie, watatu kati yao walirudi huku mmoja asijulikane aliko. Hili, pamoja na baadhi mashinikizo yaliyowekwa juu yake kufunga shule aliyokuwa akiendesha katika boma lake bila leseni, ikampelekea kuhama kutoka Migingo hadi Shakaola. Alifunga kanisa, akauza baadhi ya magari yake kisha akanunua shamba la Shakaola kwa jina la kuanzisha biashara ya kilimo.
Watu waliokwenda kumuona ambapo kanisa lake la awali lilikuwa Migingo walipewa rufaa ya kwenda shambani kwake Shakaola na kulingana na majirani, watu wengi walienda huko lakini wachache wangeoneka baadaye hukuwengi wao wakipotelea mbali.

McKenzie alikuwa na Wasaidizi ambao wangewafutilizia watu waliokuwa wamefunga kula kwa sababu za ujio wa Yesu mfungo ambao wangefuatilia roho za watu masikini msituni. Hawa pia ni watu wale wale wanaofanya kazi ya kuzika kwa ajili yake. Inadaiwa kuwa wakati akitoka Migingo na kufunga kanisa lake, aliuza kituo cha TV (vifaa) na gari lake moja kwa Mchungaji Ezekiel wa New Life na hata baadhi ya zana zake za uinjilisti. Kumbuka kuwa Mchungaji McKenzie haishi na familia yake huko Shakaola, familia hiyo inaishi katika kijiji cha Migingo katika eneo la lango alimokuwa na kanisa lake na amekuwa na nyumba nyingine nzuri ya familia umbali mfupi kutoka mji wa Malindi.

Huku akiwaongoza watu na watoto wao kufa ili kukutana na Yesu, familia yake inaishi bora zaidi kutokana na wanachompa wanapojitayarisha kwa Safari 'takatifu'. Kumbuka wengi wa watu hawa wanafunga porini mchana na usiku, huku wakikabiliwa na hali mbaya ya hewa na hatari nyinginezo.

 Unapolitaja jina la Sumbawanga nje ya maeneo ya mkoa wa Rukwa, tena kwa mtu ambaye hajawahi kufika, wazi kwamba fikra z...
18/11/2020



Unapolitaja jina la Sumbawanga nje ya maeneo ya mkoa wa Rukwa, tena kwa mtu ambaye hajawahi kufika, wazi kwamba fikra za mtu huyo zinakwenda moja kwa moja kuhusu uchawi na ushirikina.

Matukio ya ushirikina yaliyokuwa yakiripotiwa kutokea yamefanya Sumbawanga kutizamwa kwa mtizamo hasi, kwamba ni eneo la ajabu ambalo watu hawapaswi kuishi.
Zamani kuwapo kwa baadhi ya matukia fulani yaliyokuwa yakihusisha ushirikina

Matukio hayo yalikuwa yakitokea kutokana na sababu mbalimbali moja wapo ikiwa ni baadhi ya wageni kukiuka taratibu na mila na desturi za wenyeji wa Sumbawanga ambao wana sifa ya ukarimu na upendo wa hali ya juu.

(Kinyume na hayo) Pia sifa ya kabila la kifipa ni wachapakazi hodari waliojikita katika shughuli za uzalishaji mali kupitia kilimo, ufugaji na uwindaji.

HISTORIA YA NENO SUMBU-WANGA NA WATAWALA WAKE.

Kabla sijaanza kuchambua kwa kina yale yaliyokwaza wenyeji wa mji huo wa kabila la Kifipa na kusababisha kuwaadhibu wale waliokiuka mila na desturi zao, nijielekeze kueleza maana ya neno Sumbu- Wanga sio Sumbawanga k**a tulivyozoea kulitamka.

Sumbu - Wanga, maana yake ni tupa uchawi, na lilianzishwa na mtawala mmoja wa zamani wa eneo hilo Mwene Ngalu.

Sumbawanga ni makao makuu ya mkoani Rukwa, uliopo nyanda za Juu Kusini Magharibi mwa Tanzania, ulioanzishwa mwaka 1972, mkoa huo una makabila mbalimbali ila kabila kubwa na la asili ni Wafipa ambao ndiyo asili ya jina Sumbawanga.

Mji huo ulianzishwa mwaka 1803, chini ya chifu wa kwanza wa Ufipa aliyeitwa Kapufi ambaye alitawala miaka ya 1885.

Katibu wa Mila na Desturi za kabila la Wafipa (Midekawa), Domisian Mtuka (62) anaeleza kwamba Chifu Kapufi wa Kwanza alianza miliki yake ndani ya Ufipa yote na makao yake makuu yalikuwa Kijiji cha Kisumba nje kidogo ya mji wa Sumbawanga.

Mke wake aliitwa Mwene Wakulosi ambaye walijaliwa kupata watoto watatu, wa kwanza wa kiume na wawili waliofuata wa k**e ambao ni Mwene Kiatu wa pili aliitwa Mwene Ngalu Chinsi chanfipa’ (jina la utawala) na wa tatu aliitwa Mwene Mwati.

Anaeleza kuwa, Baada ya kifo cha Chifu Kapufi wa Kwanza, miliki ilitawazwa kwa mwanae wa kwanza, Mwene Kiatu ambaye alihamia kijiji cha Lwiche ambako kwa mila na desturi za kiutawala, ukitawazwa kuwa chifu kwakuwa enzi hizo ilikuwa lazima uhame sehemu unayoishi awali na kwenda kuanzisha kijiji chako k**a alivyofanya Mwene Kiatu.

Inadaiwa katika kipindi chake cha utawala wa eneo la Ufipa, chifu Mwene Kiatu hakujaliwa kupata watoto na alipokufa, miliki ilichukuliwa na dada yake, Mwene Ngalu ambaye ndiye mwanzilishi wa Sumbawanga.

Chifu Mwene Ngalu alikuwa mtu mwenye upendo na hakupenda uchafu wa aina yoyote ukiwamo uchawi, hivyo kabla ya kuingia kijiji cha Sumbawanga alichokianzisha, aliwataka wananchi waliomfuata watupe uchafu wote kwenye mto Lwiche pamoja na uchawi kisha waingie wakiwa safi.

Kutokana na imani hiyo watu walitupa uchawi wote na taka nyingine kisha wakaingia kijiji cha Sumbawanga wakiwa wasafi.

Aliyekiuka amri hiyo na kuvuka mto Lwiche kutaka kuingia kijiji kipya cha Sumbawanga alikufa wakati akijaribu kuvuka katika mto huo.

"Hapo ndipo ikawa asili ya Sumbawanga na kijiji kikawa na watu walio wasafi na hakukuwa na matatizo katika utawala wa Mwene Ngalu." anasema Katibu huyo

Mtuka anasema kuwa alipendwa na kila ilipotokea ishara ya matatizo ndani ya Ufipa ilikuwa rahisi kutatuliwa kwa kuwa Chifu Mwene Ngalu aliomba na majibu yalipatikana haraka, hasa kwa imani ya usafi waliokuwa nao.

Hata hivyo, Chifu Mwene Ngalu alijaliwa kupata watoto saba ambao wote aliwazalia katika nyumba yake ya utawala iliyojengwa kwa kipindi cha miaka miwili katika mwaka 1918 hadi 1920 chini ya usimamizi wa Mabruda wa dhehebu la Romani Katoliki ambao walikuwa Wajerumani.

Nyumba hiyo hivi sasa imebomoka na limebaki gofu ambalo kwa nje kuna sehemu ya makaburi yanayotumika kuzika kizazi cha utawala huo, na jambo la ajabu kwenye gofu hilo wapo nyuki waliojenga kwenye pango na wapo kwa muda mrefu tangu kipindi cha uhai wa baadhi ya watawala wa kizazi hicho.

Anataja watoto wa Mwene Ngalu ambao ni Maria wa Ngao, Joseph Kapufi wa Ngao, Thadeo wa Ngao, Teresia wa Ngao, Jacob wa Ngao, Victoria wa Ngao na Antony wa Ngao, ambao baada ya kifo cha mama yao, mtoto wa kwanza Joseph wa Ngao alitawazwa kuwa Chifu wa kizazi hicho na kupewa jina la Joseph wa Ngao-Kapufi wa Pili.

Chifu huyo aliyejaliwa watoto wanne, ambao ni Olanda Joseph, Adolf Joseph, Veneranda Joseph na Yovita Joseph na alipofariki dunia nduguye ambaye ni mdogo wake wa mwisho, Antony wa Ngao alitawazwa mwaka 1989, kuwa Chifu wa Ufipa na kupewa jina la Kapufi wa Tatu.

Kapufi huyo wa tatu, Antony wa Ngao, alitawala ufipa tangu mwaka 1989 hadi Desemba 6 mwaka jana alipofariki dunia na kuzikwa kwenye eneo la makaburi ya kizazi cha utawala huo, karibu na jengo la Mwene Ngalu ambalo hivi sasa limebaki gofu tu.

Katika kipindi cha utawala wake, Chifu Kapufi wa Tatu, alijaliwa kupata watoto watatu ambako mkewe wa kwanza alijaliwa kupata mtoto mmoja wa k**e aliyeitwa Ntalu na mke mdogo alijaliwa kupata watoto wawili wa kiume ambao ni Oscar na Apolinary.

Hata hivyo baada ya kifo cha Kapufi wa Tatu, hivi sasa ukoo huo wa kichifu uko kwenye mchakato wa kutafiti mrithi wa kiti hicho.

Aidha, baadhi ya maandiko yaliyohifadhi historia ya Sumbawanga na machifu wake, akinukuliwa msemaji wa familia ya akina Kapufi ambaye kwa sasa ni marehemu, Adolf Joseph aliyekuwa mtoto wa Chifu Joseph wa Ngao wa Pili.

Alidai wazee wa mji huo (wa zamani) walio hai hivi sasa pamoja na wale wa vijiji vya karibu hushirikishwa katika mchakato wa namna ya kumpata mrithi huyo kwa njia ya kuwashirikisha kuteua majina kadhaa na kuyachambua kupata anayestahili.

Anafafanua kuwa jina la mrithi likipatikana sherehe za kumsimika kuwa Chifu wa kabila hilo huanza kufanyiwa maandalizi, na kwa kawaida hufanywa nje ya mji kwa kutengeneza sehemu maalumu ya kumpitishia ambayo huiita 'Mzingo'.

Moja ya jaribio lake la kwanza ni kuvuka mto Lwiche kwa imani kuwa ni moja ya hatua za kudhihirisha kiwango cha usafi wake kabla ya chifu mtarajiwa kutawazwa.

Baada ya sehemu hiyo kukamilika kutengenezwa chifu mtarajiwa hupitishwa kwa nyuma kuingia kwenye mzingo huo huku akipuliza filimbi tatu, ya kwanza ikikataa kulia hupewa ya pili nayo ikigoma hupewa ya tatu ambayo nayo ikigoma ni dalili kuwa hafai kuwa chifu, hivyo huenguliwa na mchakato wa kumtafuta Chifu mwingine unaanza upya.

Adolf anasema ikiwa filimbi moja au mbili zikilia na moja kugoma watampa utawala wa muda huku wakijiandaa kumtafuta chifu mwingine, kwa imani kuwa filimbi zote lazima zilie kwa sababu ni ishara ya sifa njema za utawala za kiongozi anazopaswa kuwa nazo ndipo apewe mamlaka.

Wakati mchakato huo ukiendelea, wa kumpata mrithi wa kiti hicho, mavazi ya Chifu Kapufi wa Tatu, Antony wa Ngao amepewa Vicent Kafumu ambaye ni mjukuu wa Chifu Mwene Ngalu kwa mzaliwa wake wa kwanza aliyeitwa Maria wa Ngao.

Pamoja na hayo yote pia enzi za utawala wa viongozi hao walitumia silaha mbalimbali ambazo hadi leo baadhi yake zimehifadhiwa ili mtawala ajaye akabidhiwe kwa ajili ya kudumisha mila.

Zana hizo ni upinde (ulapwa), mishale (ncheto), fimbo (wasi), mkuki (ilawa) na chombo cha kubebea mishale (untontowaancheto).

Silaha nyingine ni shanga (inkasi) zinazovaliwa mikononi na shingoni kwa chifu, kiti cha miguu mitatu (kisumbi) na vazi la kujifunga kiunoni na mabegani (seketa) ambayo husukwa kwa pamba.

Kigoma
23/05/2020

Kigoma

05/07/2019

Makanisa, Misikiti itakayokwepa kuhakikiwa kuchukuliwa hatua kali - Waziri Lugola

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Makanisa na Misikiti nchini ambayo itashindwa kwenda kufanyiwa uhakiki itachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Waziri Lugola ameyazungumza hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo alifafanua kuwa; uhakiki huo ni lazima na unalenga kuzifuatilia taasisi hizo za dini kujua utendaji wake wa kazi k**a unaendana na sheria za usajili.

Lugola amesema Serikali haikuweza kuendelea na usajili wa Makanisa na Misikiti pamoja na Taasisi za kiroho nchini, wakati kwa hivyo ikaona ifanye uhakiki kwanza kwa lengo la kujua taasisi hizo zinaweza sawa na sheria za usajili.

“Tuhakikishe tunaendesha Makanisa na Misikiti na hizi taasisi za kiroho na kijamii kwa mujibu wa masharti ambayo mmesajiliwa kufanya, na pale ambapo utakuta, Kanisa lolote, Msikiti wowote,
taasisi ya kiroho yoyote inafanya shughuli zake kinyume na kusajiliwa kwake, kujihusisha na mambo ambayo hawaruhusiwi, sisi k**a Wizara tumeapa kumsaidia Mhe. Rais tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria na utaratibu,” alisema Lugola.

04/07/2019

NCHINI UGANDA MKE AMKATA MUMEWE UUME KWA MADAI YA KUKOSA UNYUMBA

Moses Okot(46) anauguza jeraha baada ya mkewe, Beatrice Acen(35) kumkata uume kwa madai ya kukosa unyumba

Okot amesema siku ya tukio, Juni 30 mkewe alirudi nyumbani akiwa amelewa na kumkata uume wake yeye akiwa usingizini

Rais Kenyatta kesho kukutana na Rais Magufuli Chato kwa mazungumzoRais Kenyatta kesho kukutana na Rais Magufuli Chato kw...
04/07/2019

Rais Kenyatta kesho kukutana na Rais Magufuli Chato kwa mazungumzo

Rais Kenyatta kesho kukutana na Rais Magufuli Chato kwa mazungumzo
Rais wa nchini Kenya Uhuru Kenyatta kesho kukutana na Rais John Magufuli nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mazungumzo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa, imeelesa kuwa Rais Kenyatta atafanya ziara ya siku mbili kuanzia Ijumaa Julai 5, 2019 kwa mwaliko wa Rais Magufuli.

“Rais Kenyatta atatua katika kiwanja cha ndege cha Chato mkoani Geita saa 4:00 asubuhi na kisha kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato,” Taarifa ilieleza.

Ilielezwa kuwa akiwa Chato Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.

04/07/2019

Habari zenu
Wanakigoma

 Mara ya Mwisho Kupata Baraka Hizi ilikuwa Mwaka Gani Kwako !!!
27/06/2019



Mara ya Mwisho Kupata Baraka Hizi ilikuwa Mwaka Gani Kwako !!!

Address

Malindi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kigoma Yetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share