21/03/2025
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Amepiga goti wa Watanzania Akiomba Msaada wa kifedha kwa ajili ya Matibabu.
KWENYE Ujumbe aliouweka kwenye ukurasa wake wa
Instagram amesema kuwa amekuwa akiahidiwa mara kwa mara na watu Binafsi kusaidiwa lakini wamekuwa ni watu ambao hawatimizi Hilo.
Mbali na hivyo amesema kuwa matibabu yake ni zaidi ya Tsh.Milioni 13 hivyo anaomba Msaada.
Anjella amaendika hivi “Habari wa-Tanzania wenzangu, Mtoto wenu nimeona nichutame kwenu , Kwasababu nimefikia sehemu ya kukata tamaa kabisa na huu ugonjwa wangu, Nimehangaika na kuahidiwa sana na watu binafsi bila mafanikio, ingekuwa inawezekana kumtumia kila mtu maumivu ninayopitia naamini hakuna mtu yeyote angeweza kukaa nayo hata kwa sekunde, Nakosa confidence, natumia dawa nyingi sana bila mafanikio matibabu haya yakiisha bila mafanikio sina budi kumuachia Mungu mpaka pale wakati sahihi wa mimi kupona utakapofika, Kuna wakati naona wenzangu wakifanya mazoezi, Naalikwa kwenye marathon nyingi mno, Lakini naumia sana siwezi kushiriki mambo mengi hasa ya kimichezo, Najua MUNGU ndiye muamuzi wa mwisho nami naamini andiko langu limetoka kwake ndio maana nimekuwa nikimuomba sana anipe msaada wa hili,
NIMEKUJA KWENU LEO NAOMBA MSAADA WENU WA MATIBABU YA UHAKIKA AMBAYO MIMI BINAFSI SIWEZI KUMUDU KWANI NI ZAIDI YA MIL 13Tsh, NIMEPATA HOSPITAL YA HAPA HAPA NYUMBANI TANZANIA. MWENYE KUGUSWA NA HILI, ANAWEZA
KUNICHANGIA KUPITIA..!
0683658961
JINA: ANJELINA SAMSON
BANK ACCOUNT (CRDB)
0152709474600
JINA : ANGELINA GEORGE SAMSON
RADIO 26 FM