19/07/2025
*MASOMO YA MISA YA JUMAPILI.*
*DOMINIKA YA KUMI NA SITA KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA MWAKA C.*
*JULAI 20 2025.*
*RANGI YA LITURUJIA: KIJANI π*
*MATENDO YA ROZARI πΏ: MATENDO YA UTUKUFU*
*MADA YA DOMINIKA:*
```UKARIMU NA USUKIVU WA NENO.```
*_Somo la kwanza na Injili vimehusishwa na mada ya ukarimu. Ukarimu ulio tayari na hiari ni ishara ya huduma kwa jirani zetu. Ukarimu ulioonyeshwa na Abrahamu kwa wageni wake ni mfano mzuri. Hadithi ya Martha na Maria inasisitiza kwamba huduma, hata huduma kwa Kristo, haiwezi kutenganishwa na usikivu wa Neno lake. Mtakatifu Paulo ni mfano wa huduma kwa wenzake. Hii ndio tunaweza kuchukua kutoka somo la pili._*
*ANTIFONA YA KUINGIA: Zab 54:6, 8*
_Tazama, Mungu ananisaidia, Bwana ananitegemeza mimi. Kwa moyo mkunjufu nitakutolea sadaka, nitalisifu jina lako, ee Bwana, maana ni jema._
*KOLEKTA*
```Ee Bwana, uwabariki watumishi wako, na uwaongezee kwa huruma vipaji vya neema yako, ili, wakiwa na ari katika matumaini, imani na mapendo, wadumu daima katika kuzishika kiaminifu amri zako. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao...```
*SOMO LA KWANZA*
Mwanzo 18:1-10a
_Bwana, usinipite mtumishi wako._
*Somo katika kitabu cha Mwanzo*
Siku ile: Bwana alimtokea Abrahamu kwenye mwaloni wa
Mamre. Abrahamu alikuwa amekaa mlangoni pa hema yake, saa ya joto la mchana. Akainua macho, akaona watu watatu wamesimama mbele yake. Alipowaona, alipiga mbio akatoka
mlangoni pa hema, akawakaribia, akainama mpaka chini. Akasema, "Bwana wangu, k**a nimekupendeza machoni pako, usinipite mtumishi wako bila kushinda kwangu. Nitaamuru walete maji kidogo, mpate kuosha miguu, na kupumzika
chini ya mti. Nami nitaleta mkate, mpate kuburudisha moyo, halafu mtaendelea na safari yenu, iliyowafikisha karibu na mtumishi wenu." Wakasema, "Vema, fanya k**a ulivyosema!" Abrahamu akaenda kwa haraka hemani kwa Sara, akasema,
"Twaa upesi vipimo vitatu vya unga, uukande, ufanye mikate." Kisha Abrahamu akaenda mbio kwenye kundi la wanyama
wake, akachukua ndama mchanga aliye mzuri; akampa
mtumishi, naye akafanya haraka kumwandaa. Akatwaa siagi.
na maziwa, na yule ndama aliyemwandaa, akawaandikia
vyote mbele yao; yeye akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala. Halafu wakasema, "Sara, bibi yako yupo wapi?" Akajibu, "Yumo hemani." Mgeni akamwambia, "Nitarudi kwako mwaka ujao, wakati huu huu; na hapo mkeo Sara atakuwa
na mtoto wa kiume."
*Neno la Bwana.*
*ZABURI YA KUITIKIZANA*
Zaburi 15:2-3a, 3bc-4ab, 5 (K. 1a)
*K. Ee Bwana, nani atakayekaa katika hema yako?*
Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, / atendaye haki, na asemaye ukweli kutoka moyoni;
hasingizii kwa ulimi wake.
*K.*
Hamtendei mwenzake uovu, /wala hamsengenyi jirani yake;
machoni pake fisadi hudharauliwa,
Bali huwaheshimu wamchao Bwana.
*K*
Hakopeshi fedha yake kwa riba,
ala hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na kosa.
Anayefanya hayo, hatatikisika milele.
*K.*
*SOMO LA PILI*
Wakolosai 1:24-28
_Fumbo lile lililofichwa tangu milele kuwa vizazi vyote sasa lakini limefunuliwa kwa watakatifu wake._
*Somo katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wakolosai*
Ndugu zangu: Sasa nafurahi kuvumilia mateso kwa ajili yenu. Hivyo ninatimiza katika mwili wangu yaliyopungua katika
mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani Kanisa, ambalo mimi nimefanywa mtumishi wake kwa kadiri ya agizo Mungu alilonipa kwa ajili yenu, ili nilitimilize neno la Mungu, yaani
fumbo lile lililofichwa tangu milele kwa vizazi vyote. Sasa
lakini limefunuliwa kwa watakatifu wake ambao ametaka
kuwaonyesha utajiri wa utukufu wa fumbo lenyewe kati ya watu wa mataifa; yaani Kristo ndani yenu, matumaini ya utukufu. Yeye tunamhubiri sisi, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumpeleka kila mmoja angali amekamilika katika Kristo.
*Neno la Bwana.*
*SHANGILIO LA INJILI*
Tazama Luka 8:15
*Aleluya. Aleluya.*
Heri watu wenye kulisikia neno, na kulishika kwa moyo
mzuri na mwema; wakatoa mavuno kwa uvumilivu.
*Aleluya.*
*INJILI*
Luka 10:38-42
_Martha alimkaribisha. Maria amelichagua fungu lililo jema._
*Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka*
Wakati ule: Yesu aliingia katika kijiji kimoja; huko mwanamke, Jina lake Martha, akamkaribisha nyumbani mwake. Naye alikuwa na dada, jina lake Maria aliyeketi miguuni pa Bwana, akisikiliza
maneno yake. Lakini Martha akishughulikia utumishi mwingi,
akamwendea akasema, "Bwana., hujali kwamba dada yangu ameniacha nitumikie peke yangu? Basi, umwambie anisaidie." Bwana akajibu, akamwambia, "Martha, Martha, unajishughulisha
na kujisumbua kwa mambo mengi. Lakini kuna jambo moja tu lahitajika. Maria amelichagua fungu lililo jema, nalo
halitaondolewa kwake."
Injili ya Bwana.