30/10/2025
Kaunti ya Marsabit imesajili idadi ndogo sana ya wapigaji kura wapya kufikia sasa tangu zoezi hili lilipoanza mwezi mmoja uliopita.
Kufikia sasa ni wapigaji kura wapya 274 pekee wamesajiliwa.
Msimamizi wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kaunti ya Marsabit, Sanchan Lokadio amesema tume hiyo inanuia kusajili wapigaji kura wapya alfu 40 ili idadi ya wapigaji kura jimboni kuwa alfu mia mbili kufikia mwaka wa 2027.
Kaunti ya Marsabit ina jumla ya wapigaji kura 166,000 waliosajiliwa.
Lokadio anahoji kuwa changamoto kubwa wanayoshuhudia ni kwamba zoezi la usajili linafanyika mijini katika afisi za IEBC ili hali idadi kubwa ya wananchi wanapatikana sehemu za mashinani.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi waliona vitambulisho kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa.
Meneja huyo wa IEBC Marsabit pia amewahamasisha wale wanataka kubadilisha vituo vyao vya kupiga kura kufanya hivyo katika afisi za IEBC katika maeneo bunge yote 4 ya kaunti hii ya Marsabit.
Mapema mwezi huu, naibu gavana wa Marsabit, Solomon Gubo na viongozi wengine walitoa wito kwa tume ya IEBC kuelekea maeneo ya mashinani ili kusajili wapigaji wapya badala ya kuendesha zoezi hilo katika afisi zao mijini.