
18/09/2025
🚨TOLEO JIPYA~INK PEN PUBLISHERS🚨
NDOTO YA HAKI ~ NELSON FARISI
Imezuka hulka ya kutatua migogoro kwa 'kifua'. Katika karne hii, maelewano na diplomasia inaelekea kutupwa mbali na watu wengi sasa hasa vijana wanaamini katika 'mwenye nguvu mpishe'. Hivi basi, nafasi ya amani na mshik**ano inapotea. Kitabu hiki kimezamia suala hili. Kando na vurumai na ghasia, zipo mbinu gani zingine za kusuluhisha migogoro? Je, diplomasia na maelewano bado yana nafasi?
Chichita anajitoa kutetea haki za wanafunzi na wafanyakazi kupitia diplomasia. Je, atafanikiwa?