21/09/2026
Poleni sana kwa wakaazi wa Tarasaa Kwa kuzikwa wapendwa watatu ndani ya siku mbili juzi na jana na tunawatakia makiwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao. Hapo jana ndo ilikua safari ya mwisho ya Sally ambae alipoteza maisha yake Mjini Hola kwa kujitia kitanzi na kuacha wengi wakitamauka na kifo chake. Waheshimiwa kadhaa walijumuika na familia na kulia nayo ikiwemo ; speaker wa county Hon Osman Galole Deputy speaker na ambae ni mca garsen South ward@ Katisha Na Mgombea Kiti cha mca Chewani ward John Bahola na mgombea mwenza wa kiti cha women rep Rehema Namasa na pamoja na Engineer Mungatana.