07/11/2022
Let's Talk about Hiphop.
Kwa wale wanaofuatilia sana mziki wa hiphop ukanda wa pwani ,msanii huyu kwa jina Jaykah Mtengwa sio mgeni kwao.
Msanii huyu Nguli anayesimama na misingi yake ya hiphop ukilinganiza na wasanii wengi wa sasa, aghalabu anatumia mziki kuelimisha jamii na kuwapasha ukweli badala ya kuufanya k**a biashara
Ukifuatilia sana mziki wake, jaykah anaonekana kuwa mwanaharakati kwa njia moja ama nyingine.
Baadhi ya ngoma alizowahi kutoa ni pamoja na Vipi nitatoka, kibao alichokitoa miaka ya nyuma kikigusia jinsi sanaa imekuwa biashara badala ya kupitisha mafunzo ili kuelimisha jamii, kiwango cha kwamba wasanii wako tayari kujiita mabachelor ilhali wameoa wako na watoto, msingi tu wavutie wafuasi
Mumiliki huyu wa studio ya Jah Records amewahi kufanya collabo na wasanii mbalimbali wa hiphop ikiwemo Kaa la moto, Masterr Kimbo ,Lai. Na. Wasanii wengine.
Hivi majuzi kaachilia kibao kwa jina Sijulikani, Fika kwenye mtandao wake wa youtube ama facebook upate kusikiza kazi zake nyingi.