Radio Mabingwa

Radio Mabingwa Radio Mabingwa is an Online Sports and Entertainment Radio Station that broadcasts in Swahili language based in coastal city of Mombasa, Kenya.

Radio Mabingwa is an online sports and entertainment radio station that broadcasts in Swahili language based in coastal city of Mombasa, Kenya and was established in April 2019, owned and managed by Radio Mabingwa Media Company. We air informative, educative, entertainment, sports updates and analysis, talk shows, social issues and community based programmes.

29/11/2024

Taifa Stars ya Tanzania, ambayo imeshatinga kwenye Michuano ijayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025 itakayoandaliwa Morocco, imepanda kwa nafasi sita kutoka nafasi ya 112 hadi nafasi ya 106 duniani kwenye viwango vya Ubora wa soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Nao majirani zao Uganda Cranes na Harambee Stars ya Kenya ziliishuka viwango huku Uganda, ambayo pia imeshatinga kwenye Michuano ya AFCON, imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 87 mpaka 88 nayo Kenya, ambayo hapo awali ilikuwa katika nafasi ya 106 mwezi Oktoba sasa imeshuka kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya 108.
Kutokana na ushindi wa mechi mbili dhidi ya Sudan na Guinea ndio iliyochangia kwa Tanzania kupanda kwenye viwango hivyo vya ubora wa FIFA. Taifa Stars iliizaba Sudan bao 1-0 katika mechi ya kufuzu Kombe la CHAN 2025 kabla ya kuichapa Guinea bao 1-0 kwenye mchezo wa kufuzu katika Kombe la AFCON 2025 Uwanjani Benjamini Mkapa.
Kwa upande wa Uganda ilishuka viwango baada ya kupoteza mechi yake moja kati ya mbili za mwisho dhidi ya Congo Brazzavile na Afrika Kusini.
Na kushuka kwa viwango vya Kenya ilichangiwa na matokeo ya sare ilizopata katika mechi zake mbili za mwisho dhidi ya Namibia na Zimbabwe, yaliyowanyima tiketi ya kwenda kucheza kwenye Michuano ya Kombe la AFCON 2025 itakayoandaliwa nchini Morocco.
Kwa mujibu wa viwango hivyo vya mwezi Novemba 2024, Uganda ni ya 19 barani Afrika wakati Tanzania inashikilia nafasi ya 24 huku Kenya ikiwa katika nafasi ya 25.
Morocco ndio inayoongoza barani Afrika (duniani 14) ikifuatiwa na Senagal kwenye nafasi ya pili (duniani 17) huku Misri ni ya tatu (duniani 33). Algeria iko kwenye nafasi ya nne (duniani 37), Nigeria inashikilia nafasi ya tano (duniani 44). Kwenye viwango hivyo bado Argentina inaendelea kushikilia namba moja duniani ikifuatiwa na Ufaransa wakati Uhispania ikikamata nafasi ya tatu, nayo England ni ya nne.
Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia la FIFA Brazil wamekaa kwenye nafasi ya tano.

24/11/2024

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe atafanya ziara Afrika Mashariki atakapotembelea Kenya, Tanzania na Uganda mwezi Desemba, mwaka huu 2024.
Katika ziara hiyo Motsepe atathmini maendeleo na utayari wa viwanja na miundombinu mingine na vifaa kwa ajili ya kuandaa Michuano ya Wachezaji wanaocheza ligi za soka barani Afrika yaani Kombe la CHAN.
Kenya, Tanzania na Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo ya Kombe la CHAN, itakayoandaliwa kuanzia Jumamosi ya Februari Mosi hadi Ijumaa ya Februari 28, 2025. Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa michuano ya Kombe la CHAN kuandaliwa na nchi tatu kwa pamoja.
Kombe la CHAN, ambayo ilikuwa ifanyike mwaka huu 2024, inaandaliwa kwa mara ya pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na mara ya kwanza Rwanda ilikuwa mwenyeji kwenye michuano ya mwaka 2016.
Mabingwa watetezi wa Kombe la CHAN ni Senegal ambayo ilitwaa taji hilo baada ya kuwashinda Algeria mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti kufuatia timu hizo kutoka suluhu baada ya dakika 120 katika fainali.

24/11/2024

Check out Anthony Aroshee’s video.

RONALDO NAZARIO ALIVYOCHEZA AKIWA AMEVAA 'PAMPERS' UWANJANI
24/11/2024

RONALDO NAZARIO ALIVYOCHEZA AKIWA AMEVAA 'PAMPERS' UWANJANI

Check out Anthony Aroshee’s video.

07/11/2024

Taasisi ya Wakaguzi wa Mizani na Vipimo yaani Masoroveya nchini Kenya(ISK) imetangaza kwamba itawashughulikia vilivyo matapeli wanaojifanya kuwa ni masoroveya kwa kuwalaghai Wakenya huku wakiathiri pakubwa sekta ya ardhi nchini humo.
Rais wa Taasisi hiyo ya Masoroveya nchini Kenya(ISK) Eric Nyadimo alisema kwamba taasisi ya ISK inashirikiana na wadau mbalimbali katika jitihada za kutokomeza kabisa shughuli za masoroveya bandia nchini humo.
Rais Nyadimo alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Kimataifa linalokutanisha Wakaguzi wa Mizani na Vipimo yaani Masoroveya kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika, lililoanza siku ya Alhamisi ya Novemba 7, 2024.
Kongamano hilo limeandaliwa kwa dhamira ya kuja na mbinu za kisasa na endelevu za kuboresha utumizi wa ardhi, kuhifadhi mazingira na kukabilina na mabadiliko ya tabianchi.
“Tunafanya kazi pamoja na wadau wote wa Bodi za usajili kuhakikisha kuwa tumewakabili vilivyo matapeli. Tunahimiza umma kutoa taarifa za ulaghai kwa taasisi zetu za ISK, kwa Idara ya Upepelelezi na Makosa ya Jinai(DCI) ama tume ya madili na kupambana na ufisadi nchini Kenya(EACC) kuhusu visa vya wanakandarasi kukosa kutoa huduma halali kwa mujibu wa mkataba wa maafikiano ili hatua za haraka za kisheria zichukuliwe kukabili na kutatua masuala hayo.” Nyadimo alikariri.
Kongamano hilo la siku mbili linakamilika rasmi Ijumaa ya Novemba 8, 2024.

01/11/2024

HII NDIO SABABU YA VINICIUS JR. WA REAL MADRID KUKOSA TUZO YA BALLON D'OR YA 2024.

Address

Nyerere Road
Mombasa
80100

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio Mabingwa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio Mabingwa:

Share

Category