28/11/2025
USAJILI WA ESTEVAO KUTUA CHELSEA
Dogo alijiunga na academy ya Palmeiras mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 14 pekee akitokea Cruzeiro zote za uko uko nchini Brazil, baada ya kujiunga na Palmeiras alianza kuvishawishi vilabu vingi sana kutokana na ubora wake .
Mwaka 2023 akiwa na umri wa miaka 16 na miezi 6 alienda kuiwakilisha Brazil U17 kwenye kombe la dunia, alionesha kipaji kikubwa sana cha soka akazidi kuonekana kwenye macho ya wengi na apo ndipo alipoanzwa kuzungumzwa ulaya.
Dogo alipohojiwa alisema ndoto yake ni kujiunga na FC Barcelona kwasababu ndio klabu ya ndoto yake, vilabu vilivyokua vikimfatilia ni Bayern Munich, Chelsea na Real Madrid.
Barça walitamani sana kumsajili ila shida waliangalia uwepo wa Lamine Yamal kwenye klabu iyo na wote umri wao ni sawa pia wote wanacheza eneo moja ( namba 7 au 10 ) inaweza kumuathiri mmoja kati yake kiwango chake kikashuka kwasababu italazimika mmoja asubirie nje ili mwingine apate nafasi .
Real Madrid walimtaka sana ila dogo alikataa mwenyewe kujiunga na Madrid kutokana na mapenzi yake kwa FC Barcelona, Madrid wakapita na Endrick pekee.
Chelsea wakatia mguu na ikawa rahisi kwao kumsajili dogo kwasababu klabu ya ndoto yake isingeweza kumsajili, walimsajili mapema akiwa na miaka 16 akawa anasubiriwa afikishe umri wa miaka 18 ili apewe kubali cha kufanyia kazi ulaya .
Baada ya World Cup U17 dogo akaanza kupewa nafasi ya kuaminiwa ndani ya Palmeiras na baadaye akawa nyote wa klabu akiwa na umri wa miaka 17 pekee.
Akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Brazil na mchezaji bora chipukizi.
Sifa nyingine ya dogo kwao ni watu wa dini sana na ata yeye ni mtu wa dini sana ndiomana ni ngumu kumuona kwenye maisha ya starehe.