16/09/2026
Tume Maalumu iliyoundwa na M***i na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali, imebaini kuwepo kwa makosa ya kimaadili na kiuongozi yanayowahusu aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa, pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Sheikh Issa Nassor Issa, na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Sheikh Hassan Idi Kiburwa.
Akisoma ripoti ya Tume hiyo leo, Katibu wa Tume, Dkt. Abdallah Tego, amesema uchunguzi ulihusisha kupitia nyaraka mbalimbali, taarifa za mitandaoni, mahojiano na mashahidi pamoja na kusikiliza utetezi wa viongozi waliotakiwa mbele ya Tume.
Kwa mujibu wa Tume, Sheikh Walid hakufika mbele ya Tume kutoa utetezi wake licha ya juhudi zilizofanywa kumtafuta.
Wakati huo huo, Sheikh Issa Nassor Issa na Sheikh Hassan Idi Kiburwa walifika mbele ya Tume na kutoa maelezo yao, ambayo Tume imesema yalisaidia kupunguza uzito wa baadhi ya makosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Miongoni mwa tuhuma zilizochunguzwa dhidi ya Sheikh Walid ni pamoja na:
1️⃣ Kuteua viongozi kinyume na Katiba ya Baraza.
2️⃣ Kukosekana kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa Baraza mkoani Dar es Salaam.
3️⃣ Kudaiwa kupanga safu ya viongozi kwa ajili ya Uchaguzi wa 2026 kinyume na kanuni na miongozo ya Baraza.
4️⃣ Kujihusisha na masuala ya kifedha nje ya utaratibu na miongozo ya Baraza.
5️⃣ Tuhuma nyingine za kimaadili zilizowasilishwa kupitia nyaraka na taarifa za mitandaoni.
Tume imewasihi masheikh hao kuheshimu na kusikiliza uamuzi wa mwisho utakaotolewa na Baraza la Ulamaa, ikisisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kulinda maslahi ya umma wa Kiislamu.
📌 Kwa sasa, uamuzi wa mwisho bado unasubiriwa kutoka kwa Baraza la Ulamaa.
𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗙𝗕 𝗣𝗔𝗚𝗘 DAAWA TV